Sorry out of topic, mkuu mshana nowdays sikumbuki kabisa nilichoota ucku. Is it normal,?? msaada tafadhali
![]()
Wengi wetu tumeshakumbana na hili tatizo aidha sisi wenyewe ama kupitia ndugu jamaa au hata rafiki, ni tatizo la kiufahamu ambalo husababishwa na matatizo mengine mwilini kama mfumo wa upumuaji kutokuwa sawa, shida kwenye mfumo wa kusukuma damu, madawa msongo wa mawazo uchovu fikra za kufikirika nk
Kiroho pia ina tafsiri yake kwamba hata unapokuwa umelala na hujitambui ufahamu wako huwa active na kufanya mengine yote bila wewe mwenyewe kwenye nafsi ya utashi ukishindwa kutambua lolote.
Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa hata wale wanga na wachawi wanaochukua watu usiku hutumia formula ya ufahamu kuchukua watu kwenda kuwafanyisha kazi kisha kuwarudisha bila wao kujitambua
![]()
Dalili za tatizo hili kwa baadhi huanza utotoni ambalo wala mtoto hana stress nk, na utakuta mtoto anaongea pekeyake bila kutoa sauti anakunjua sura ama kukunja na wakati mwingine kushtuka,(hapa mambo ya kishirikina pia huhusika sana)
Hali hii hutokea masaa takibran matatu baada ya kulala ama kwenye usingizi mzito usiku wa manane na huweza kudumu kuanzia sekunde 30 mpaka nususaa.
Tatizo hili hutofautiana ukubwa, wengine huamka tu kitandani na kuzunguka ndani ya chumba na kurudi kulala! Ila wengine huamka na kama ni mwanafunzi huvaa uniform kabisa na kutoka mpaka nje hata wafanyakazi pia!
Akiwa katika hali hiyo huweza kutembea mpaka hatua kadhaa kisha kurejea ndani na kulala tena huku mwenyewe kwenye hali ya utashi akiwa hajui lolote
Nimekutana na kesi za namna hiyo na watu wakitibiwa kwa kitunguu saumu ama ndimu(hii ni tiba mbadala)kwakuwa kwa hospitali hizi za kizungu hili halina tiba bali hupotea lenyewe au kwa njia ya kutibu chanzo, hasa kama limesababishwa na viashiria vya wazi kama madawa msukumo wa damu stress nk
Kiafrika haishauriwi kabisa kumshtua mtu anayetembea usingizini kwakuwa kile kitendo si utashi wake bali ni command ya ufahamu ambalo haukuwalisiana na nafsi ya utashi (kutenda kwa uamuzi)kinachotakiwa ni kumshika mkono na kumrudisha kitandani taratibu na mara nyingi ufahamu hutii....!
Si wote wanaoamka asubuhi wakiwa wachovu au wamechafuka miguu nk ni matendo ya kishirikina, wengine ni hili tatizo la kutembea usingizini.
Aaaaaaaaah, mkuu acha bhanaNafikiri wanga wanAkufunga usikumbuke ukawawahi kuharibu mAmbo yao ili yakupate vizuri
Hata mimhilo tatizo ninalo sikuhiZi
Jaribu kulala mapema ili uondoe msongo wa mawazo ambayo ndio Vitendo vyake huwa vinajirudia pale ulalapo!Mim kipind ambacho bad nasoma ilikuwa kila ifikapo usiku mwingi naongea mnoo yaani lakin naongea maneno ambayo hayaeleweki yaani naongea kilugha ndani ya usingizi hapo nawakati nikiwa na ufaham wangu yaani nikiwa macho ukiniambia niongee hicho kikwetu sijui hata moja zaidi ya salam tu nikiinuka asubuh ndo nahadithiwa Kama niliongea usiku mpk muda mwengine nainuka nakaa kabisa kitandani Ile hali ikawa ni mazoea yangu kabisa yaani kila nikifika usiku mpka niongee lkn nashangaa sasa hivi nashukuru mungu sinayo tena hali ile
Hali hii hata mimi inanitokeaga,naweza kupita mahali hata kama ni mkoa au wilaya ambayo cjawahi kufika nikaona mtaa au baadhi ya mpangilio wa nyumba au mazingira machache ambayo naona kama nayajua na naweza kuhisi hata kabla sijaumaliza kama ni mtaa mwisho utakuwaje na ukawa hivyo,nakosaga majibu kwa kweli.Hii inahusuka na reincarnation, kuna topic yake ngoja nikiipata takutag
Mdogo wangu wakike alikuwaga anatatizo kama hili usiku anaongea kwa sauti huku yy kalala Akinogewa anaamka anakuja hadi sebuleni anataka kutoka nje,ilivyozidi tukawa tunatoa ufunguo mlangoni ili ashindwe kutoka na mda huo ukimuona anakuwa kafumba macho na hajigongi popote anapita kama anaona vile.Atashtuka usingizini na nafsi ya utashi italeta mvurugano kwenye ufahamu kamili kitu kinachoweza kusababisha kifo kutokana na mshtuko
Haya kwangu huwa yananitokea mara kadhaa!Hivi mshana jr mm kuna matukio mengine huwa yanapotokea katika maisha yangu ya kila siku mala nyingine huwa nayaona kama si mageni yani nililiona kabla. Ila nakuwa sikumbuki nililiona wapi. Hivi ni kweli huwa huenda nililiona au nin kinahusika.
Mshana hata kwa webu nyingine pia haifunguki. Kama solution ni kuwa tagged naomba unitag tafadhari kwani inanihusuHapana mimi sio mchawi nimeacha![]()
![]()
![]()
Naomba kuuliza, hawa wenye kuzungumza wakiwa wamelala, hii iko je?. Niliwahi kuishi na jamaa kutoka Ethiopia, ikifika usiku kwenye saa nane huwa anaonge kama vile yupo na mtu , inaweza kuchukuwa hata saa nzima,kama uko nje unaweza kusema yumacho anamgeni wanzungumza, lakini amekuwa amelala usingizi kabisa.Unakitafuna na kujipaka kwenye paji la uso na vijaganjani bila kusahau kifuani
Tukiondoka kwenye dhana ya reincarnation, ufahamu wetu husafiri ni kitu kama kile tunaita kutoka nje ya mwiliHali hii hata mimi inanitokeaga,naweza kupita mahali hata kama ni mkoa au wilaya ambayo cjawahi kufika nikaona mtaa au baadhi ya mpangilio wa nyumba au mazingira machache ambayo naona kama nayajua na naweza kuhisi hata kabla sijaumaliza kama ni mtaa mwisho utakuwaje na ukawa hivyo,nakosaga majibu kwa kweli.
Kinachofanya kazi hapo ni ufahamu na anaona kupitia jicho la tatuMdogo wangu wakike alikuwaga anatatizo kama hili usiku anaongea kwa sauti huku yy kalala Akinogewa anaamka anakuja hadi sebuleni anataka kutoka nje,ilivyozidi tukawa tunatoa ufunguo mlangoni ili ashindwe kutoka na mda huo ukimuona anakuwa kafumba macho na hajigongi popote anapita kama anaona vile.
Mkuu unarudi au unajiandaa kwenda?Kupitia Google inafunguka jaribu, takutag pia
Kwa huyu jamaa wako wa Ethiopia inawezekana kabisa ni maradhi yanayohusiana na hii mada lakini Kwa huyo mzee wako ni mmojawapo wa watu wanaomiliki supernatural powers, ana uwezo wa kusafiri popote kula chochote ama kufanya chochote bila kujulikana na wengine na hafanyi Kwa kificho, kwenye hili wengine huchanganya na ushirikinaNaomba kuuliza, hawa wenye kuzungumza wakiwa wamelala, hii iko je?. Niliwahi kuishi na jamaa kutoka Ethiopia, ikifika usiku kwenye saa nane huwa anaonge kama vile yupo na mtu , inaweza kuchukuwa hata saa nzima,kama uko nje unaweza kusema yumacho anamgeni wanzungumza, lakini amekuwa amelala usingizi kabisa.
Vilele niliwahi kuishi kwa mzee mmoja shamba, zamani, huyu mzee ikifika usiku wa saa sita huwa anamka na kuongea, lakini yule anaengea nae hutumuoni, tulikuwa tumeshamzoea wala hatuogopi, tukimuliza asubuhi anasema alikuwa na mgeni. Jenginine alikuwa na shamba lake kama umbali wa maili mbili kutoka nyumbani, tukichukuwa chochote, embe, karanga.tukifika nyumbani anakuwa ameshajua. Chengine kilichonishangaza zaidi, nikiwa Form 1 miaka hiyo aliniambia alienda Istambul, huyu mzee hana passport, hata kusoma na kuandika hajui.mimi niliijua istambul kwa atlas tu, kulikuwa hakuna tv wala video. Baada ya kama miaka nane mimi mwenyewe nilienda Istambul. cha ajabu mambo mengi aliyonieleza aliyoyaona Istambul ni ya kweli. Hebu nambie kweli huyu mtu alisafiri kwenda Istambul kwa njia za kichawi au vipi?