Kutembea ukiwa usingizini

Kutembea ukiwa usingizini

1e7761d954f8c945a4d62ec22c410c19.jpg

Wengi wetu tumeshakumbana na hili tatizo aidha sisi wenyewe ama kupitia ndugu jamaa au hata rafiki, ni tatizo la kiufahamu ambalo husababishwa na matatizo mengine mwilini kama mfumo wa upumuaji kutokuwa sawa, shida kwenye mfumo wa kusukuma damu, madawa msongo wa mawazo uchovu fikra za kufikirika nk

Kiroho pia ina tafsiri yake kwamba hata unapokuwa umelala na hujitambui ufahamu wako huwa active na kufanya mengine yote bila wewe mwenyewe kwenye nafsi ya utashi ukishindwa kutambua lolote.

Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa hata wale wanga na wachawi wanaochukua watu usiku hutumia formula ya ufahamu kuchukua watu kwenda kuwafanyisha kazi kisha kuwarudisha bila wao kujitambua
70ae5819adbbc390a659e7b1670ca3ec.jpg

Dalili za tatizo hili kwa baadhi huanza utotoni ambalo wala mtoto hana stress nk, na utakuta mtoto anaongea pekeyake bila kutoa sauti anakunjua sura ama kukunja na wakati mwingine kushtuka,(hapa mambo ya kishirikina pia huhusika sana)

Hali hii hutokea masaa takibran matatu baada ya kulala ama kwenye usingizi mzito usiku wa manane na huweza kudumu kuanzia sekunde 30 mpaka nususaa.

Tatizo hili hutofautiana ukubwa, wengine huamka tu kitandani na kuzunguka ndani ya chumba na kurudi kulala! Ila wengine huamka na kama ni mwanafunzi huvaa uniform kabisa na kutoka mpaka nje hata wafanyakazi pia!

Akiwa katika hali hiyo huweza kutembea mpaka hatua kadhaa kisha kurejea ndani na kulala tena huku mwenyewe kwenye hali ya utashi akiwa hajui lolote
Nimekutana na kesi za namna hiyo na watu wakitibiwa kwa kitunguu saumu ama ndimu(hii ni tiba mbadala)kwakuwa kwa hospitali hizi za kizungu hili halina tiba bali hupotea lenyewe au kwa njia ya kutibu chanzo, hasa kama limesababishwa na viashiria vya wazi kama madawa msukumo wa damu stress nk

Kiafrika haishauriwi kabisa kumshtua mtu anayetembea usingizini kwakuwa kile kitendo si utashi wake bali ni command ya ufahamu ambalo haukuwalisiana na nafsi ya utashi (kutenda kwa uamuzi)kinachotakiwa ni kumshika mkono na kumrudisha kitandani taratibu na mara nyingi ufahamu hutii....!

Si wote wanaoamka asubuhi wakiwa wachovu au wamechafuka miguu nk ni matendo ya kishirikina, wengine ni hili tatizo la kutembea usingizini.
Kuna Bwana mmoja yeye alikua tatizo hilo. Siku moja kaamka kaenda jikoni kapika chai na akanywa, wakati anarudi kitandani akajigonga kwenye mbao ya mlango kichwani akazimia, alipopata fahamu nakuelezwa alichokifanya akakataa.
 
Inawezekana kabisa kwakuwa hafanyi kwa fahamu za utashi wake
 
Kwa baadhi ambao hawana tatizo lingine lolote lakini huwa mahiri na waliobobea kwenye fikra za kufikirika hufikia kutengeneza matendo halisi kwenye ufahamu na kujikuta wanayatekeleza usingizini bila utashi wa nafsi
2012cab92a1a91bfd312924a2ca2dc92.jpg
Kwa mfano kama umelala ww na mkeo mmoja kulia mwingine kushoto,alafu unastuka katikati ya usiku na kujikuta ww umelala kushoto mkeo kulia,yani mmebadilishana maeneo bila kujua,je,hili nalo linahusiana na mada hii?
 
Mmh nipe muda
 
Kwa baadhi ambao hawana tatizo lingine lolote lakini huwa mahiri na waliobobea kwenye fikra za kufikirika hufikia kutengeneza matendo halisi kwenye ufahamu na kujikuta wanayatekeleza usingizini bila utashi wa nafsi
2012cab92a1a91bfd312924a2ca2dc92.jpg
Kihospitali wanahusishasha na ugonjwa wa kifafa cha usingizi kwahiyo mtu anayesumbuliwa na hali hiyo anashauriwa kumuona tabibu wa magonjwa ya ndani
 
Kihospitali wanahusishasha na ugonjwa wa kifafa cha usingizi kwahiyo mtu anayesumbuliwa na hali hiyo anashauriwa kumuona tabibu wa magonjwa ya ndani
Yeah lakini sidhani kama ni kesi zote
 
Hii haina uhusiano kabisa na kutembea ukiwa usingizi, wewe ilikuwa ni michezo ya kichawi au wanga
Matendo ya kutembea usingizini hutendeka kwa mpangio na bila kelele na mhusika huenda na kurudi bila kujitambua na kuendelea na usingizi wake
Je yule ambaye alikua anamchungulia pengine anaweza kua Mwanga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom