Hii ilinitokea mimi,kipindi nikiwa Mvulana tu! Kati ya miaka 16-20,nilikuwa nikiishi nyumbani kwenye nyumba ndogo mfano wa servant quoter yenye chumba kimoja na sebule,mwanzo nilikuwa nikiishi hapo na kaka yangu ambaye baadaye alihamia mji mwingine! Sasa siku moja nikiwa nimetoka nyumba kubwa kupata mlo wa usiku nikafika kwenye kitanda changu na kukaa hapo kwa muda nikiwaza kitu ambacho sikuwahi kukikumbuka hata,,lakini obviously nilikuwa in a deep absorption!! Sasa baada ya muda kidogo nikaanza kuhisi kama ninaota kwenye mazingira hayo hayo!nilianza kusikia mtu akisukuma mlango wa kuingia sebuleni,nilisikia mkwaruzo wa bawaba wakati mlango unafunguka hadi ulipogonga kwenye frame ya mlango wa chumbani,nikapata hisia za kutoka nione nani anayeingia,muda huo ilikuwa ni mishale ya saa nne au zaidi kidogo,nikanyanyuka,kwenda sebuleni huku nikihisi kizunguzungu kikali! Mlango wa kutoka chumbani ulikuwa wazi,nilipofika tu katikati ya mlango wa kutoka chumbani nikaona Mwanga mkali ukitokea sebuleni,na mlango wa sebuleni ulikuwa wazi Japo nilikumbuka kama niliufunga wakati naingia, nikaogopa na kuamua kurudi chumbani huku nikiacha mlango wa nje ukiwa wazi,Sikufanikiwa kufika chumbani kwani ghafla tu nilipofika katikati ya mlango wa ndani nilihisi kumwagikiwa na kitu cha majimaji! Niilipojitazama nikaona damu nyingi ikimiminika kutoka kwenye Tundu dogo lililopo juu kwenye ceiling board,muda wote huo nilikuwa siwezi hata kuinua mguu!!nilikuwa ganzi mwili mzima! Nikawa nasali kimoyo moyo!ghafla Nikahisi nguvu zikinirudia na ufahamu kuanza kkurejea. Taratibu! Sekunde chache baadaye nikajikuta nikiwa na ufahamu kamili huku nikiwa nimekaa palepale kitandani huku nikiwa nimechoka sana na jasho likinitoka kwa wingi! Nikatoka na kurudi nyumba kubwa (kwa mshua) nikagonga mlango! Mama akauliza "nani?" nikajibu "mimi fulani" akauliza tena kuna nini? Nikamwambia "Nimekuja kulala huku" aliivyofungua nikaangalia saa ya ukutani!! Ilikuwa saa saba na zaidi! Baada ya kumwadithia mama asubuhi yake akanipeleka hospitali,nikapimwa malaria nk! Sikuwa na ugonjwa wowote!!
Hiyo ndoto naikumbuka hadi leo ninapoelekea Uzeeni!