nzalendo
Platinum Member
- May 26, 2009
- 12,901
- 14,611
Naam vijana wetu na watoto wetu pia wajukuu huamua kufunga safari na kwenda nchi za mbali katika kujitafutia riziki,
Wengi huenda kwa njia ya kupata Elimu na baadae huamua kufanya kazi,,,wengine huenda kama kutembea na kujilipua nk nk wengine hupata Green Card kwa wale wa magharibi ya mbali.
Sasa ukweli ni kwamba,,wengi wana maisha magumu sana sana tofauti na tunavyodhani,
NItajaribu kutoa simulizi chache......
Kuna kijana mmoja alifika magharibi ya mbali kama mwanafunzi akapata degree yake akaunga na Masters na kupata kibarua saafi cha kumuwezesha kumudu maisha.
KIjana kwa bakhti mbaya alipata mtihani katika mahusiano,,,kapata mwanamke...na katika nchi ya magharibi ya mbali...mwanamke ni adui namba moja ya mwanaume.
Wakajaaliwa mtoto.....mwanamke katunga ya kutunga baada ya kumchoka jamaa.....jamaa akazushiwa ya kuzushiwa kesi juu ya kesi.....mwishowe.....mahakama ikaamuru jamaa awe analipa kila mwezi matumizi ya mtoto(wenyewe wanaita child support)
Huku na kule akapata mwanamke mwingine wa kupooza....ghafla nae akajaaliwa kupata mtoto,,,,,,yakamkuta ya kumkuta nae kwa amri ya mahakama akalazimika kutoa child support.
kutokana na hali ya mazingira pengine upweke n.k kijana akawa na kitu kama depression akatumbukia kwenye ulevi wa kupindukia akapoteza kazi,,
Kurudi nyumbani anaona aibu,,maana hana kitu,,,,kula yake ni food bank(misosi ya bure) kulala kwake ni shelter,,,inatia uchungu lakini ndio hali halisi,,,huku nyumbani,,,,,,"Tuna kijana wetu yupo magharibi ya mbali".....