Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
!Kuna wanaume wanayo taabia ya KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU.
Kuna kasumba moja imetawala vichwa vya tulio wengi:
Sasa uchunguzi umedhihirisha wazi kwamba MWANAUME anae chukua mke wa mtu ndiye huonekana MKOSAJI SANA,na pengine hunyooshewa sana mikono mtaani!
Sasa mimi nashindwa kuelewa,kwanini yule mwanamke aliyechukuliwa ASINYOOSHEWE KIDOLE?au asionekane mkosaji kwa kiwango kile kile?ukizingatia walikubaliana?
Hii dhana inaanzia wapi jamani?
Ukweli hata kama ukiuma ni kiherehere cha mwanamke, maana mwanamke akizidiwa ni ugonjwa usioponyeka. Na kabisa self control isipokuwepo ni sawa na aliyechanganyikiwa. Atakuwa tayari hata kukumbatia kisichotegemewa hadi watu wamwonee huruma, basi samahani kama nimefika mbali mno.
Kwamba kwa kuweka kwenye mizani hakuna kinachomzidi mwenzake kati ya wawili hao si kweli. Ingawa mwanaume ana nafasi ya kutumia utashi zaidi na mwanamke vionjo zaidi. Mwenye utashi na mwenye vionjo hapo kazi ipo.
Mbona mie nimefikia kiwango cha kuvuliwa nguo kabisa lakini sijadiriki kumgusa? Nina ushahidi wa kiherehere cha baadhi ya wanawake, lakini mwanaume ukiwa na ustahimilivu na kutojali hawezi kukulazimisha. Hapa unaona nani mwenye kosa zaidi kwa vile mwingine ni ugonjwa na mmoja kukosa kutumia utashi wake.