Kutawaliwa na Chama kimoja toka Uhuru ni udikteta, lakini tumejifanya hatuoni

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Toka uhuru mpaka sasa tumetawaliwa na mfumo wa chama kimoja, na bado watu wanaita ni Nchi ya Demokrasia.

Uchaguzi unaofanyika Nchini ni kama bosheni tu, na uchaguzi halali ni ule unaofanyika katika kamati kuu ya chama tawala kumpitisha mgombea. Mgombea akishapitishwa na chama tawala tayari huyo anakuwa ndio Rais. Walioko huku nje ni wapiga kura za chakalamu tu.

Chama tawala kuvinyamazisha vyama vingine vya kisiasa ni kuonesha Dunia kwamba Raia wanaridhika na utawala wa chama hiki kilichopo madarakani kitu ambacho sio kweli.

Ni kama tuko kwenye Udikteka wa chama kimoja ila wananchi wanajifanya hawaoni. Chama kimeingiza Mamluki wa kila Aina katika Sekta mbalimbali za serikali ili kuhakikisha zinawanyamazisha wapinzani na kushinda uchaguzi kwa wizi.

Wananchi tuamke katika hili wimbi wa udikteta
 
Kulalamika tuu bila kutoa solution ni sababu nyingine ya kubariki unachokilalamikia. Leta mikakati tunasolve vipi tatizo au wote tuendelee kulalamika?
 
Back
Top Bottom