Salaam, Shalom!!
SHERIA zetu ziko wazi kuwa, miaka sitini ni umri wa kustaafu, inaaminika baada ya miaka 60, uwezo na nguvu za kufanya KAZI Huwa unakuwa umefika KIKOMO na kuanza kupungua Polepole. Mzee mwenye umri wa miaka sitini , ndoto zake Huwa amezihamishia Kwa watoto na wajukuu zake.
Chama hiki kina miaka 62 sasa, uwezo wake katika kusikilizia na kutatua changamoto za wananchi umeenda ukipungua siku Hadi siku ,hivi sasa hakuna tena vision ya miaka ya mbele zaidi.
Kushindwa kutatua matatizo ya nchi yakaisha ni dalili za uzee,
1. Utaona Hadi sasa tangu uhuru tunanunua madawati Kila mwaka watoto wasikae chini. Madawati hayajawahi kutosha.
2.Kila mwaka tunajenga shule na hatujawahi kumaliza. Walimu hawajawahi kutosha, Wala hatujawahi kupata pesa za kuwalipa overtime walimu nk nk
3. Kila mwaka tunajenga na kukarabati barabara, na hatujawahi kujenga barabara ya kudumu Kwa miaka hata 20 bila matengenezo.
4. Kila mwaka kipindi Cha kiangazi lazima Kuna mgao wa umeme, na imeshakuwa Rasmi. Mwaka huu, pamoja na mvua za kutosha kuwepo, na mabwawa kujaa, Bado tunapitia mgao mkali wa umeme, uwezo wa kununua token ya luku Bado Si kigezo Cha kupata umeme.
5. Dalili za uzee ni kuambiwa kuwa wingi wetu ndiyo sababu kuu ya Serikali kushindwa kutuhudumia, maji jijini Dar ni mtihani mkubwa, unaweza kumiliki choo Cha kuflash lakini usiwe na HAKIKA ya maji ya kuflash choo chako hata kama una pesa ya kulipa bills zako.
6. Chama kizee hakiwezi tena kukamata Wala kutisha wezi wa raslimali za umma, Kila mtu ala Kwa urefu wa Kamba yake.
7. Kila mwaka, lazima pawepo na upungufu wa Sukari, na lazima vitolewe vibali kuagiza nje, mwaka huu umetisha, pamoja na vibali kutolewa, Bado sukari haipo. Tumetangaziwa, wauzaji sukari wote wajisajili Kwa DC na RC, tumerudi enzi za 1984, wakati haya yakitokea, hapo Zambia Kuna sukari ya kutosha, tungetumia ndege zetu kununua fasta na kujaza soko ndani ya wiki tatizo likaisha, uzee umetamalaki.
Matatizo ya nchi ni lukuki, shime ndugu Watanzania wenzangu, chama hiki kikongwe pamoja na Uzee wake, Bado kimegoma kutaja mrithi wake, kinasubiri siku ya kufa ndipo litaje mrithi.
Kuepuka sintofahamu hiyo,
TUKIPUMZISHE KWA MASLAHI YA UMMA.
Karibuni 🙏