kutana na BABU wa Eritrea

Am waiting miss Judith, natamani ungetoa hayo majumuhisho leo.

Atawaletea majumuisho kutoka Eritrea
Mi nadhani MJ anataka awapotezee muda wenu tu
Jana alidai ataleta ya Eritrea, tumeyaona ndio haya yamejaa upupu zaidi
Sasa hayo majumuisho si yatakuwa takataka kabisa
Maana yatakuwa majumuisho ya sredi zake zote alizomwanzishia Babu hapa JF
Leo Mwakasege aka Mzee wa Upako kawaumbua wale wote waliosema yupo against huduma za Babu
Tena kawaonya waache kuchezea kazi za Mungu anazofanya Babu Mwasapile
Sasa hawa wenzetu ndo bado wanavijidonge vyao mioyoni mwao na 500/- za Babu
 
Hadi muda huu ninapopost hii maneno, miss judith hajafanya majumuisho yake,

Bila shaka atakuwa ameenda kujichimbia eritrea, ama la yuko mahali na rafiki yake wanaandaa majumuisho.

Kwa ujumla judith na the likes hawana hoja yoyote ya msingi dhidi ya huduma ya babu, nadhani tumpongeze kwa kufanikiwa kutupotezea muda lakini pia kujifunua kwetu tumemfahamu yeye ni mtu wa namna gani.
 
Wapendwa,

Kama nilivyowaahidi ndio namaliza mazungumzo na rafiki yangu kutoka Eritrea kuhusu “babu” wa huko kwao na shughuli zake. Kimsingi hatofautiani sana na babu wetu huyu wa TZ. Mambo ya “babu” wa Eritrea kwa mujibu wa huyu rafiki ni kuwa:

1.
Alijulikana kwa jina la Armalakha na alikuwa muinjilisti na mhubiri hodari katika nchi za Ethiopia na Eritrea hata kabla Eritrea haijajitenga kutoka Ethiopia.

2.
Aliwahi kuingia katika migogoro kadhaa na makanisa ya kikatoliki na orthodoxy (amabyo ndiyo makubwa na yanaheshimika sana nchini humo) ya Eritrea na Ethiopia kwa sababu makanisa hayo yalipinga utaratibu wa tiba yake kwa kuhusianisha uganga wake na mafundisho ya biblia.

3.
Mwaka 1996 alianza kudai kuwa mungu amemuotesha mchanganyiko wa madawa asilia ambayo huyachanganya na kuyachemsha na kasha maji yake kuwanywesha wagonjwa wake na makapi ya maji yake kuwafungia wagonjwa wake kwenye mkono wa kuume na kuuning’iniza mkono huo kama POP. Hiyo ni baada ya kusema mungu kamtokea katika ndoto na kumfunulia kuwa maradhi yote yanayowasumbua watu yako tumboni na hutokea mwilini kupitia mkono wa kuume.

4.
Watu wa kwanza kunywa dawa zake walikuwa wakiongea kwa lugha za ajabu na yeye akawa anadai ndizo lugha mpya zilizotabiriwa na nabii Yoeli!
5.
Alidai anatibu magonjwa makuu kama kansa, ukimwi, kisukari na kutoa mapepo ya aina zote kwa dawa zake hizo!

6.
Alidai mungu kamwagiza atibu kwa Nakfa 8/- tu (nakfa ni sarafu ya Eritrea na nakfa moja ni sawa na senti kama 30 za USD)

7.
Alipata umaarufu mkubwa sana na wa ghafla sambamba na kutajirika sana katika kipindi kifupi sana na kulikuwa na shuhuda nyingi sana kuwa watu wengi walipona maradhi yao kwa muda mfupi sana na kimiujiza japo hospitali za Ethiopia na Eritrea hazikuwahi kuthibitisha uponyaji wake hata mara moja!

8.
kutokana na uhasama ulioibika baada ya Eritrea kujitenga na Ethiopia (baada ya eritrea kujitangazia uhuru), alituhumiwa kuwa alikuwa wakala wa intelijensia ya Ethiopia (yaani alikuwa anaipatia serikali ya Ethiopia taarifa za siri za kijasusi) na kufuatia kuandamwa sana na vyombo vya dola aliuawa kwa kupigwa risasi June mwaka 2006.

Hayo ndiyo niliyopata kwa rafiki yangu huyu.

Wapendwa tusiache kuzijaribu kila roho ili tujiridhishe kuwa zimetokana na Mungu. Neno la mungu ni taa na mwangaza wa maisha yetu, liyumulikie kila tuendapo. Amina.

Nawatakia tafakari njema

Glory to God

Judy mimi nataka kujifunza jambo na ni tabia yangu kuuliza sana hata kuonekana ovyo ili mradi nielewe

Kwa hoja yako nadhani unataka kujustify babu ni fake kwa kuwa kuna ma-fake wengine maeneo mengine duniani

Swali langu ni Je, kutamalaki kwa manabii wa Mungu kunamaanisha manabii wote wa Shetani na Baali hawako kazini wakati huo?

Au kutamalaki kwa manabii wa Shetani kunamaanisha manabii wote wa Mungu wako likizo?

Is this the right reason to justify kuwa babu ni fake kwa kuwa wako wengine ambao nao ni fake (kama wapo)?
 
Hivi ni waafrika peke yao ndio wanaletewa ufunuo wa kutibu kwa mizizi..?
Shetani anajuwa wazungu hawakubaliani na upmbazu kama huu, eti mtu kalala anajamba tu! asubuhi anatuambia nimetumwa na Mungu. huu sio ulimwengu wa ndoto jamani.
 
Judy mimi nataka kujifunza jambo na ni tabia yangu kuuliza sana hata kuonekana ovyo ili mradi nielewe

Kwa hoja yako nadhani unataka kujustify babu ni fake kwa kuwa kuna ma-fake wengine maeneo mengine duniani

Swali langu ni Je, kutamalaki kwa manabii wa Mungu kunamaanisha manabii wote wa Shetani na Baali hawako kazini wakati huo?

Au kutamalaki kwa manabii wa Shetani kunamaanisha manabii wote wa Mungu wako likizo?

Is this the right reason to justify kuwa babu ni fake kwa kuwa wako wengine ambao nao ni fake (kama wapo)?
nini kitatujulisha kuwa hutu ni nabii?. mbona hili deal la unabii naona kama limeibuka tu juzi juzi, na wale wanaojiita manabii wanaoneka mambo ya swafiii baada ya kujitangazia unabii, hakuna nabii hao ni wajanja tu!,
 
Wapendwa katika Bwana,

Naamini kila mmoja wetu anaufahamu vizuri mjadala unaoendelea juu ya Mch. Mwasapile. Maelezo ya baadhi ya mambo yalijitokeza katika mada yangu ile ni kama ifuatavyo:
1. Ni bora tukamwacha babu aendelee na kazi zake
kimsingi mimi na wote tunaohoji shughuli za uganga wa babu hatuna nia ya kumzuia babu kufanya shughuli zake hizo za kutibu kwa mitishamba, bali tunahoji uhalali wa madai yake kuwa shughuli hizo zimetokana na ufunuo wa Mungu. Na hii ni kwa sababu tukimpima kimaandiko, tunapata kila sababu ya kusema kuwa kama ni kweli kafunuliwa na Mungu, basi si Mungu huyu tunayemuabudu wakristo na aliyemtuma Bwana Yesu kuja duniani kutuokoa dhambini (kumbukeni kuwa kuna miungu mingine ya uongo hujiinua na kudai kuabudiwa kama Mungu aliye hai). Sababu zetu ni pamoja na kuwa
· Babu hafundishi neno la Mungu na hivyo hiyo huduma yake imelenga kuponya mwili pekee na si roho
· uponyaji wake umefungamana na mti Fulani na siyo Yesu Kristo (uponyaji ni
· Tiba yake imo ndani ya mipaka ya kijiji cha samunge pekee (karama za Mungu
· tiba yake haimuinui na kumtukuza Mungu bali anajiinua yeye mwenyewe na mti wake wa mrigariga
· Maono yake yaliambatana na agizo la kutoza sh.500/- kwa kila atakayehitaji uponyaji (Mungu wetu hatozi wala hahitaji hata senti yetu moja)
· Anataka dunia nzima isafiri kwenda kijijini kwake kupata hiyo huduma yake
Majibu ya haya yote yametolewa kwa kina kwenye thread husika

2. Tumwache kila mtu afuate imani yake
Kama wakristo, ni wajibu wetu kupima kila roho na kujiridhisha kuwa imetokana na Mungu (1Watehsalonike 5:18 na 1 Yohana 4:1). Katika Ezekiel 33:8-9 tunaambiwa ukimwona mtu anapotea nawe usiseme neno kumuokoa, ataangamia lakini damu yake itadaiwa mkono mwako. Kwa hiyo ni wajibu utokanao na upendo wa undugu katika mwili wa Kristo kuwa tusiwaache watu waelekee upotevuni. Kama mitume wa Bwana na wamissionari wangeacha kila mtu afuate imani yake, hakika hakuna mtu angemjua Yesu na kuzijua Baraka za Mungu za rohoni nje ya Galilaya, Samaria na Yudea, mikoa alikohudumu Bwana enzi za huduma yake hapa duniani.

Kamwe hatutanyamaza wala kumwacha kila mtu afuate imani yake. Bali katika kila neno, kila ndoto na kila ishara/muujiza, tutachunguza na kupima kama liko sawa na limetokana na injili ya Bwana na kuonya, kukaripia na kufundisha njia sahihi bila kuchoka (2 Timotheo 4:1-5).

3. Tusihukumu tusije tukahukumiwa
kupima na kuhoji aina ya roho aitumiayo babu kuponya na kama imetokana na Mungu au la, sio kuhukumu. Kuhoji tunakofanya ni kwa mujibu wa maandiko matakatifu na sio nje yake. Ndugu yako akiwa na mwenendo usiofaa na ukamkanya au kumpa angalizo ili abadili mwenendo wake sio kumhukumu.
Babu ni ndugu yangu katika Bwana na kama kuna shaka yoyote katika shughuli zake, ni wajibu wangu na wa mkristo yoyote kumrejeza katika kweli yote. Hatutaacha kufundisha, kuonya, kukemea na kazi nyingine za mhubiri wa injili (2 Timotheo 4:1-5)

4. Mambo ya imani magumu kueleweka
imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo. Kwa maneno mengine, imani isiyotokana na uelewa wa injili si imani ya Kikristo. Imani ya kikristo lazima itokane na neno na hupimwa kwa neno na hivyo twaweza kusema kwa hakika kabisa kuwa imani fulani ni sahihi au sio sahihi kwa kuzingatia msingi wa neno la Mungu.
Ugumu wengi wanaousema ni wa imani tofauti na za kikriso kwa sababu hazijafunuliwa. Zimefumbwa na kuachwa kama MYSTERY, ila ya kikristo iko wazi na ITS NO LONGER A MYSTERY. Nawashauri wapengwa tusiwe wazito kusoma neno la Mungu lenye ufunuo wa kila kitu tunachopaswa kujua kuhusu imani yetu.

5. Tuiache huduma ya babu itajidhihirisha mbele ya safari kwani kama ni ya uongo atakwama tu
Wale wanaojua misingi ya Total Quality Management, hawawezi kusema kauli kama hii. Ni sawa na kusema tuache ndege iruke na abiria angani bila kujiridhisha kama ina mafuta ya kutosha kwa safari ili kama haina mafuta ya kutosha itaanguka na ndipo tutakapojua ukweli kama ilikuwa na mafuta ya kutosha au la! Haya ni mawazo mabaya sana na kwa kweli ni ya ajabu! Learning from mistake doesnt always work!

Kama nilivyosema katika namba 2, 3 na 4 hapo juu haiwezekani kumuacha babu aendelee tu na huduma yake bila kuhoji uhalali wake kimaandiko. Kama asingedai kuwa ni ufunuo wa Mungu uliokuwa juu yake, basi ingeeleweka kuwa ni mganga wa mitishamba kama wengine na tungemchukulia hivyo. Kwa kuwa kasema ni ufunuo wa Mungu basi tunawajibu wa kuupima ufunuo wenyewe na kuhoji usahihi wake kimaandiko kabla ya kuuamini. Isitoshe kama ni wa uongo, atawadanganya na kuwapoteza watu wengi sana na anaweza hata kusababisha mauti ya kutisha hata kuzidi ya kibwetere wa Uganda na mwisho enzi kuangamiza ndugu zetu wengi zaidi katika jehanamu.

6. Hata Yesu aliponya watu kwa kutumia tope, naaman aliponywa kwa kujichovya mara saba mto yordani
hatuna shina na mti autumiao kuponya, bali chanzo cha ufunuo wake na utaratibu mzima wa tiba yake vinatia shaka kwani haviendani na imani ya kikristo kwa mujibu wa maandiko. Bwana wetu ni Bwana wa vitu vyote. Alipokuwa duniani alidhihirisha mambo mengi sana kwa namna ya kipekee sana na ilikuwa inalenga kuonyesha kuwa alikuwa na malaka juu ya kila kitu na kuwa ndiye atokaye kwa Baba. Kila miujiza aliyoifanya ilikuwa unique na ishara kuwa yeye ndiye. Aliweza hata kufufua wafu na kusamehe dhambi na aliweka wazi kuwa ana mamlaka ya kusamehe dhambi (Mathayo 9:6).
Kwa nyakati zote miujiza ilikuwa si kwa kila mtu aliyekuwa dhaifu. Enzi za naaman kulikuwa na wakoma wengi sana duniani, lakini ni naaman pekee aliyeponywa, enzi za Yesu kulikuwa na wagonjwa wengi sana wa kila aina, lakini ni hakuwaponya wote. Miujiza ya huyu babu inamtukuza mwenyewe na mti wake na si Mungu.

7. uponyaji ni suala la imani ya mponywaji
Yesu aliposema kuwa "imani yako imekuponya" alikuwa anadokeza tu nini kilichoponya. Naomba nieleweke hapa kuwa
· si mara zote Yesu alikuwa akisema kilichoponya
· si kila uponyaji ni kwa sababu ya imani ya mponywaji
· Imani ya mponyaji pia yaweza kuponya hata kama mponywaji hana imani
Kitabu cha matendo ya mitume kina mifano mingi sana ju ya ukweli huu.

8. Watu wameteseka sana na maradhi na Mungu amekuja kuwafariji na kuwarejeshea matumaini ya afya njema
lengo kubwa la Mungu ni kuokoa kutoka katika dhambi na sio kuondoa mateso ya mwili na faraja ya Bwana iko rohoni zaidi na sio mwilini.
Hata waganga watumiao pepo wachafu nao huwapa faraja wateja wao kwa hiyo, faraja pekee wapatayo wateja wa babu haituzuii kuhoji usahihi wa roho atumiayo babu kuponya.

9. Sh. 500/- anazotoza babu si kitu ukilinganisha na baraka na faraja ya uponyaji wa magonjwa sugu kama ukimwi, kansa, kisukari, shinikizo la damu nk wanayopata. tena wengi wako tayari kutoa zaidi ila babu ndiye anawazuia
Karama ya Mungu ni bure na haitozwi hata senti moja, tumepewa bure na tutoe bure . Watumishi wanaweza kuomba au kuchagiza sadaka na michango mingine ya hiyari kulingana na uwezo na mapenzi ya mtoaji.
Huduma a neno la Mungu ni bure kabisa, yoyote atozae fedha (nyingi au chache, awe babu, mwakasege, judith au nani mwingine) yuko kinyume na injili.

10. Kwa nini hatupingi huduma za wengine?
Inafahamika kuwa akina kakobe, mwingira, rwakatale, fernandes, lusekelo, gwajima gamnywa nk hutoza pesa nyingi sana kwa kisingizio cha sadaka na michango mbalimbali kama mafungu ya kumi, ujenzi, shukrani nk. Hapa ikumbukwe kuwa hawa hawakuwa mada na hakuna aliyeleta mada juu yao tukakataa kuchangia au tukachangia kwa kuwaunga mkono na ilipofika kwa babu tu ndiyo tukageukia kumlaumu babu.
hapa sitasema juu yao na kama kuna haja basi mimi mwenyewe au yoyote mwingine alete mada inayowahusu nitachangia na naamini na wapendwa wote wanaolitumaini neno la uzima wachangia kwa kadiri ya neema ya Mungu.
Ila napenda kusema kwa kifupi kuwa babu hawezi kuwa sawa kwa vile tu wengine hao tuliotaja nao wanafanya. Huduma ya Mungu haina cha kufuata mkumbo na wala hatuwezi kuipima roho ya babu na shughuli zake kwa roho na shughuli za watu wengine. Kila roho na shughuli ya kiroho hupimwa kwa maandiko matakatifu pekee ambayo ni maneno ya Mungu mwenyewe, basi.

11. Sisi tunaotilia shaka huduma hii tuna wivu.
Hapa hakuna wivu, kuna neno la Mungu na shughuli za babu, basi. Kama zisingepingana na maandiko, tungepata wapi sababu ya kuihoji au kuipinga huduma yake? Mimi sio kiongozi wala wakala wa huduma yoyote pinzani ya kiroho bali ni mkristo wa kawaida.

12. Tunatilia shaka huduma hii kwa sababu hatujapatwa na magonjwa sugu na kujua jinsi yanavyowatesa watu
nadhani nimeishaafafnua kwa kirefu ni kwa nini tunahoji hii huduma ya babu na si vyema ku-duplicate material bila sababu za msingi. Tunalopinga ni jinsi huduma yenyewe ilivyo kwa msingi wa neno la Mungu. Ayubu alipata mateso makubwa sana ya kufilisika mali, misiba nyumbani kwake, majipu nk lakini hakumkufuru Mungu wala kugeukia imani zisizo sahihi.

Kwa hiyo na sisi hatuna sababu ya kuacha kuwahimiza hata wapendwa wetu wenye mateso ya magonjwa kuendelea kumuamini Mungu wa kweli hata ikibidi kumtukuza Mungu kwa njia ya kifo bila kuikana imani. HUU NDIO UKRISTO NINAOUFAHAMU MMI.
Ukristo wa kumwamini Mungu wakati wa afya na raha peke yake na ujapo wakati wa maradhi na shida nyingine ukaruhusu kujishirikisha na roho zisizoeleweka vyema tena bila kuzipima eti kwa sababu tu "umeteseka sana na wanahitaji uponyaji", hakika sio ukristo wa kweli uliojengwa juu ya neno la Mungu na mimi si MMOJA WAO.

13. Muhimu ni kupona na sio zaidi
ni kweli muhimu ni kupona, tena kupona roho sio mwili. Ni heri tuingie mbinguni na chongo au vilema kuliko kutupwa jehanum tukiwa na macho wakamilifu wa mwili. Kwa hiyo watu watafute kupona roho zao kabla ya kitu kingine chochote.
Mwenye ukimwi, kansa, kisukari, pumu, BP nk atafute kwanza uponyajiwa roho yake na atakuwa amepata faida kubwa sana ya kuingia mbinguni hata akifa kutokana na maradhi yake hayo, kuliko aponywe hayo maradhi bila kutengeneza maisha yeke na Mungu na hatimaye kuishia jehanum.

14. Ubikira wa Miss Judith
hii haikuwa mada lakini iliingizwa kwenye mjadala baada ya mimi mwenyewe kulazimika kujieleza baada ya watu kuhusisha AVATAR yangu na maisha yangu binafsi wakidai kuwa kama avatar inavyoonekana inawezekana na mimi ni mhuni tu na mambo mengine mengi.

Ubikira wangu unatokana na neema ya Mungu pamoja na kutembea katika mwanga wa neno la Mungu toka nikiwa mdogo. SIWEZI KUONA HAYA KUSHUHUDIA JAMBO HILI. Kama waasherati hawaoni haya kujisifia ufundi wao wa kufanya uzinzi, kwa nini mie nione haya kuliinua neno la Mungu? Huu ni ushahidi mwingine kuwa neno la Mungu lina nguvu na linaweza kubadili mienendo yetu na tukaishi maisha yenye Baraka za Mungu kama tutaliamini na kuliacha liongoze maisha yetu.

Ni vizuri wote (hata waliobeza) wakajua kuwa ubikira ni jambo la kawaida kimaumbile lakini jiulize kuwa ukiitisha mabikira wenye umri wa miaka 26 kutoka mtaa unaoishi utapata wangapi? Sijasema hawapo, nauliza unategemea kupata wangapi? Najua hamjasahau, juzijuzi tu hapa JF ilikuwa inajadiliwa mada ya watu kutamani wangerudi kuwa mabikira!

Ni kizazi kilichopotoka tu ndicho kitakachoweza kuchefuliwa na ubikira. Bikira Maria alipotokewa na malaika na kupewa ujumbe kuwa atapata mimba, alisema bila haya wala kutafuna maneno kuwa yeye yu bikira. Huko uyahudi enzi zile kila atajwapo mwanamke ama binti ambaye hajamjua mume bado ilikuwa ni kawaida kusisitiza kuwa yu bikira. Hata baba akiwatambulisha wabinti zake ilikuwa kawaida kusema, mwanangu huyu ni bikira anaitwa Fulani.

Mtu akijisifia hapa masuala ya ufundi wa mapenzi halaumiwi kuwa ana-attract attention. Kuna mtu aliwahi kuanzisha thread kuwa anatafuta infidelity na ilichangamkiwa na watu wengi na ilipita kurasa 150! Wapendwa tutafakari kwa pamoja haja ya kuyarudia maneno ya Mungu na kuyategemea yatuongoze njia zetu.

15. Mwenendo wa Miss Judith hapa JF kikristo unatia shaka
Hebu kuweni positive. Kutongoza si lazima kuishie kwenye ngono, bali kunalenga kuanzisha urafiki na mawasiliano. Mimi ni mpenzi na mwerevu wa saikolojia na sosholojia. Baadhi ya majukumu yangu yanahusisha utafiti wa masuala yanayoangukia katika Nyanja hizo. Sanaa nzima ya kutongoza na kila kitu kinachoendelea huko "at your own risk" ninakifahamu vizuri japo sijawahi ku-practice ngono maishani mwangu. Kama kuna mtu ana swali akaulize kwenye ile thread inayohusika nitamjibu kadiri nitakavyoweza.
Sioni tatizo la kutembelea huko"at your own risk", kwani yaliyoko huko ndiyo yanayofanyika kila siku hapa duniani. Pia kwa nafasi yangu kikazi na kijamii, nawajibika kuyajua kiundani, kisayansi na kwa ufasaha na ninayafanyia kazi kila siku.

16. Thread kuhamishiwa chit-chat forum
Japo sikuwaunga mkono moderators katika hili lakini naamini walijitahidi kuwa wavumilivu manake kuna kila dalili kuwa baadhi ya members humu wana nguvu ya ajabu juu ya moderators na inawezekana nao ni moderators pia. Dada yangu Michele amewahi kutofautiana na baadhi ya watu hapa tena kwa jambo la kawaida kabisa kwa watu kutofautiana akaishia kupewa ban. So hata mimi najua naweza kukabiliwa na hatari ya ban.
Siwezi kunyamaza nikaacha kusema neno la kweli iwe juu ya babu au mtu mwingine yoyote eti kwa kuogopa ban. Mungu ndiye Muweza wa yote na hatimaye Kweli itashinda.

poleni kwa maelezo marefu japo nimeedit sana hadi nikachelewa kupost. Nimalizie kwa kusema kuwa kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo (1Wakorintho 15:10)

Mungu awabariki nyote

ONE-MAN-SHOW BUSINESS!....!
What i have discovered so far is, unapenda sana attention!...in "glory-to-god- comouflage"!, ...asante, tumekuelewa!
 
Wapendwa,

Kama nilivyowaahidi ndio namaliza mazungumzo na rafiki yangu kutoka Eritrea kuhusu "babu" wa huko kwao na shughuli zake. Kimsingi hatofautiani sana na babu wetu huyu wa TZ. Mambo ya "babu" wa Eritrea kwa mujibu wa huyu rafiki ni kuwa:

1.
Alijulikana kwa jina la Armalakha na alikuwa muinjilisti na mhubiri hodari katika nchi za Ethiopia na Eritrea hata kabla Eritrea haijajitenga kutoka Ethiopia.

2.
Aliwahi kuingia katika migogoro kadhaa na makanisa ya kikatoliki na orthodoxy (amabyo ndiyo makubwa na yanaheshimika sana nchini humo) ya Eritrea na Ethiopia kwa sababu makanisa hayo yalipinga utaratibu wa tiba yake kwa kuhusianisha uganga wake na mafundisho ya biblia.

3.
Mwaka 1996 alianza kudai kuwa mungu amemuotesha mchanganyiko wa madawa asilia ambayo huyachanganya na kuyachemsha na kasha maji yake kuwanywesha wagonjwa wake na makapi ya maji yake kuwafungia wagonjwa wake kwenye mkono wa kuume na kuuning'iniza mkono huo kama POP. Hiyo ni baada ya kusema mungu kamtokea katika ndoto na kumfunulia kuwa maradhi yote yanayowasumbua watu yako tumboni na hutokea mwilini kupitia mkono wa kuume.

4.
Watu wa kwanza kunywa dawa zake walikuwa wakiongea kwa lugha za ajabu na yeye akawa anadai ndizo lugha mpya zilizotabiriwa na nabii Yoeli!
5.
Alidai anatibu magonjwa makuu kama kansa, ukimwi, kisukari na kutoa mapepo ya aina zote kwa dawa zake hizo!

6.
Alidai mungu kamwagiza atibu kwa Nakfa 8/- tu (nakfa ni sarafu ya Eritrea na nakfa moja ni sawa na senti kama 30 za USD)

7.
Alipata umaarufu mkubwa sana na wa ghafla sambamba na kutajirika sana katika kipindi kifupi sana na kulikuwa na shuhuda nyingi sana kuwa watu wengi walipona maradhi yao kwa muda mfupi sana na kimiujiza japo hospitali za Ethiopia na Eritrea hazikuwahi kuthibitisha uponyaji wake hata mara moja!

8.
kutokana na uhasama ulioibika baada ya Eritrea kujitenga na Ethiopia (baada ya eritrea kujitangazia uhuru), alituhumiwa kuwa alikuwa wakala wa intelijensia ya Ethiopia (yaani alikuwa anaipatia serikali ya Ethiopia taarifa za siri za kijasusi) na kufuatia kuandamwa sana na vyombo vya dola aliuawa kwa kupigwa risasi June mwaka 2006.

Hayo ndiyo niliyopata kwa rafiki yangu huyu.

Wapendwa tusiache kuzijaribu kila roho ili tujiridhishe kuwa zimetokana na Mungu. Neno la mungu ni taa na mwangaza wa maisha yetu, liyumulikie kila tuendapo. Amina.

Nawatakia tafakari njema

Glory to God

Wewwe kweli Ajenti wa Shetani.
 
Mi sijawaelewa mnaomsakama Miss Judy kwa kutueleza babu mwingine wa Eritrea.
Kosa lake ni nini?
Mbona Tarakea ameibuka babu mwingine na yeye naye ameoteshwa kama alivyo wa Loliondo.
Hamwamini kama babu wa Loiondo ni marudio tuu?(awe ametumwa na Mungu au hajatumwa)

Yule wa Tarakea ni Mchaga.
 
Back
Top Bottom