Je, Kilio cha Haki Kitasikika?
Inaonekana ukosefu wa haki umeenea kila mahali. Fikiria mifano miwili ya watu waliohukumiwa isivyo haki:
- Mnamo Januari 2018, hakimu nchini Marekani aliamuru mwanamume fulani aliyefungwa miaka 38 hivi iliyopita awekwe huru. Ilionekana hakuwa na hatia kwa msingi wa uthibitisho wa chembe za urithi (DNA).
- Mnamo Septemba 1994, vijana watatu katika nchi moja ya Afrika walifungwa kwa sababu walikataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Kufikia Septemba 2020, walikuwa wamefungwa gerezani kwa miaka 26 bila hata kushtakiwa au kufikishwa mahakamani kwa uhalifu wanaodaiwa kuwa walifanya.
Ikiwa umekabili ukosefu wa haki, huenda ukahisi kama Ayubu aliyeishi katika nyakati za Biblia aliyesema: “Naendelea kulilia msaada, lakini hakuna haki.” (
Ayubu 19:7) Hata hivyo, ingawa huenda ikaonekana kwamba kupata haki ya kweli ni ndoto, Biblia inaahidi wakati ambapo kilio cha haki
kitasikika. Isitoshe, hekima yake inaweza kukusaidia kukabiliana na ukosefu wa haki sasa hivi.
Ni nini husababisha ukosefu wa haki?
Ukosefu wa haki husababishwa na wale wanaokataa mwongozo wa Mungu. Biblia inaonyesha kwamba haki ya kweli inatoka kwa Mungu. (
Isaya 51:4) Katika Biblia, maneno yanayotafsiriwa “haki” na “uadilifu” yana uhusiano wa karibu. (
Zaburi 33:5) Matendo ya uadilifu, au yaliyo mema na yanayofaa kulingana na viwango vya Mungu, hutokeza haki. Tofauti na hilo, ukosefu wa haki hutokana na dhambi, ambayo ni kuvunja viwango vya uadilifu vya Mungu. F