BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Watanzania tunaofanya marekebisho ya Taarifa za Kitambulisho cha NIDA kuna mlolongo mrefu na gharama kubwa lakini bado pia taarifa hazirekebishwi kwa zaidi ya miezi mitatu.
Wengi tunafahamu kuwa kuwa na kitambisho cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ni jambo muhimu na linarahisisha shughuli nyingi kwenye kazi mbalimbali pamoja na masuala ya masomo na hata binafsi.
Kwanza kabisa ukitaka kurekebisha taarifa binafsi za kitambulisho au zilizopo NIDA unatakiwa kujipanga kisaikolojia kutokana na kesho utakazozipata za usumbufu pamoja na kujiandaa kiuchumi kwa kuwa utalazimika ‘kutoboka’ mfukoni ili kupata kitu.
Mfano nijitolee mfano mimi binafsi, nilipohitaji kurekebisha taarifa nilitumia kiasi cha Tsh. 20,000 kwa ajili ya Hati ya Kiapo (Deep Poll), Tsh. 33,000 kwa ajili ya kulipia kwenye katika Ofisi ya Msajili, nikatangaza katika Gazeti la Serikali 20,000, nilipokamilisha hapo nikalipia Tsh. 20,000 kwenye ofisi zao za NIDA.
Jumla ilikuwa Shilingi 93,000 lakini hapo bado kuna gharama za nenda rudi, njoo kesho, nenga kule, rudi huku.
Baada ya kukamilisha hayo ndipo unaanza mchakato wa kusubiri muda wa marekebisho hayo.
Nina zaidi ya miezi mitatu sijafanyiwa marekebisho.
Mfano kuna Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wanao ripoti vyuoni na ili usajiliwe unatakiwa uwe na NIDA au taarifa zao ziendane pamoja na zile zilizopo kwenye nyaraka zake nyingine.
Asilimia kubwa ya Wanafunzi wanaohitaji kufanyiwa mabadiliko kwenye NIDA ili yaendane sawa na taarifa zilizopo kwenye nyaraka zao wanazowasilisha chuo, wamekuwa wakiitia katika wakati mgumu.
Wito wangu kwa Serikali ya Tanzania na Mamlaka yenyewe ya NIDA, katika Dunia ya sasa ambayo kuna maendeleo makubwa ya Teknolojia, kweli unalazimika kusubiri miezi mitatu kufanyiwa marekebisho ya taarifa za NIDA hata kama ukiwa na kila kitu? Hii si sawa, tuko nyuma sana.