Mamlaka za vitambulisho vya Taifa (NIDA) waichunguze link inayotoa softcopy ya ID

Nedd Ludd

Senior Member
May 16, 2023
135
245
Habari wana JF, kumekuwa na link ikisambaa ikijieleza hivi JE WAJUA?

Mamilioni ya Watanzania wana namba za vitambilisho vya NIDA lakini hawana vitambulisho vya NIDA. Tembelea: NIDA Online Copy sasa ujitapatie online copy ya kitambulisho chako bure

Hii link hata mimi nimekuwa mhanga maana ukijaza taarifa zako unapata hiyo softcopy ya Kutambulisho.
Chakushangaza Mamlaka wametoa taarifa tupuuze hiyo link, sasa najiuliza wao huo mfumo wa kupata taarifa za mtu na kumpatia softcopy ya Kitambulisho kikiwa na taarifa zote za mhusika wameutoa wapi?

Screenshot_20231116-205533.jpg
 
Hao wanaosimamia hiyo system wanapaswa kutengeneza checking point kuangalia all related activities maana kwa namna hii kila mtu atajipatia huduma mwenyewe bila monitoring yoyote
 
Habari wana JF, kumekuwa na link ikisambaa ikijieleza hivi JE WAJUA?

Mamilioni ya Watanzania wana namba za vitambilisho vya NIDA lakini hawana vitambulisho vya NIDA. Tembelea: NIDA Online Copy sasa ujitapatie online copy ya kitambulisho chako bure

Hii link hata mimi nimekuwa mhanga maana ukijaza taarifa zako unapata hiyo softcopy ya Kutambulisho.
Chakushangaza Mamlaka wametoa taarifa tupuuze hiyo link, sasa najiuliza wao huo mfumo wa kupata taarifa za mtu na kumpatia softcopy ya Kitambulisho kikiwa na taarifa zote za mhusika wameutoa wapi?

View attachment 2815909
Hiyo link naona kama imefungwa au network yangu ndio dhaifu?
 
Back
Top Bottom