Mie naona sababu ni kushindwa tu. Hakuna sababu nyingine. Vinginevyo kama ipo basi anaijua Romney ambaye hata hivyo kwa sasa kwa alivyopigika hawezi kuiweka hapa JF tuijadili. Nampa hongera Romney kwa kuangukia pua. Maana kama angeangukia mgogo huenda angejinyonga. Bloodies as he is, he needs time to recuperate.
romney kashindwa kwa mambo mengi lakini kubwa ni kuwa sera zake hazikuwavutia wapiga kura ,amefuata siasa katili ya republican ya ubepari mkali bila ya kuzingatia wananchi wanaoumia kwa muanguko wa uchumina kuwafagilia mabilionea na trilionea wazidi kutesa bila ya kulipa kodi stahiki na walala hou kuendelea kubeba mzigo wa kodi huo ndio ubaya wa ubepari ,vita visivyokwisha ambavyo vinasababisha vijana wengi wafe nchi za nje ,tishio la kwenda muflisi na madeni makubwa ya serikali .ndio maana unaona makundi yote haya kumunguka mkono na kabakia na wazee weupe na vijana kiduchu waliomuunga mkono hata wanawake pia kawa udhi kwani nani anafurahi kuona kazi ilio sawa mwanamke analipwa tofauti na mwanamme chini ya mwanamme hata mama clinton na majitambo yake bado kimshara anapata kidogo na mwanaume angekuwa yupo wakati ule.Pia masuala ya kubakwa na upataji wa kinga za kuzuia mimba na dawa za bure za cancer yote haya hakuyaunga mkono wanawake wameona wamedharauliwa na bw Romney. ila amejitahidi sana na kamtoa jasho Mhe Obama.kubwa zaidi na la kujifunza ni maandalizi ya uchaguzi huanza mara baada ya uchaguzi kwisha hapo ndipo alipopata ushindi mnono Obama kwani timu yake ya wagonga milango kuhimiza kupiga kura walimaliza kazi kitambo na iliobakia ilikuwa ni mazoezi tu hdi kufikia ushindi .jee mnajifunza nini wana TZ Clinton kasema its all mathematics
Alidhani anaweza kushinda kwa white votes tu...imekula kwake lazima wabadilike ili kuwa inclusive to US' demographic changes
Siwezi kuongeza chochote hapo mkuu!! hayo ndio zaidi ya majibu yenyewe. WATU USA WANAISHI KWA MATUMAINI...Huu ni mjadala wa kubadilishana mawazo kitaaluma. Hivyo kama unataka kumpa ongera Baraka Obama, nakushauri fanya hivyo kwenye thread nyingine.
Jana nilipokuwa naangalia matangazo kutoka katika Boston na Chicago niliona vitu viwili muhimu. Kitu cha kwanza kwenye kambi Romney waliokuwa wanasubiri matokeo wengi walikuwa wazee na wazungu. Kitu cha pili katika kambi iliyokuwepo Chicago, wengi walikuwa ni vijana na vilevile kutoka jamii mbalimbali.
Ukichunguza vitu hivi viwili kwa makini, unaweza kusema kuwa Obama amechaguliwa sio kwa sababu anamzidi Romney kiutendaji wa kazi. Amechaguliwa kwa sababu ya muundo wa jamii zilizopo Marekani. Hii ni sababu moja na zinaweza kuwepo zingine.
Ningeomba tuzichambue hizo sababu hili tujifunze.
Z10
Taaluma gani? Wewe una taaluma gani?Huu ni mjadala wa kubadilishana mawazo kitaaluma.
Hivi kwa kuangalia kura za watu (forget the electoral college for a minute) ni kweli unaweza kusema sera za republicans hazina mashabiki sana Marekani?.......
Hivi kwa kuangalia kura za watu (forget the electoral college for a minute) ni kweli unaweza kusema sera za republicans hazina mashabiki sana Marekani?........
Sera Republican zina mashiko pia ila tu wenzetu hawana tension ya demokrasia kama sisi, kwani mtu akikosa hamna kulalamika na kukataa kusaini matokea kuwa ameshindwa.
Kama unakumbuka Obama amedeclare kuwa ataonana na mpinzani wake ili aweze kupata mawazo yake ambayo anaona yanafaa kwa maendeleo ya Marekani, vivyo hivyo hataka 2008 alimchukua mpinzani wake kichama Hillary Clintoni ili wafanye kazi pamoja na wameweza.
So wenzetu hawana tension ya demokrasia kwamba ukikosa uongozi basi umepoteza kila kitu. Kwetu sisi bado sana, nikiwa mbunge nikipoteza leo basi hata ile nyumba niliyokuwa naishi Mikocheni ninaweza nikaiuza. Hebu tafakari Maige kukosa uwaziri na nyumba anauza! So what?.......
Hata Democrats waliposhindwa chaguzi mbili mfululizo kuna watu walidhani kuwa labda huo ndiyo mwisho wao. GOP wana nafasi kubwa sana ya kushinda uraisi 2016.......
He wasn't cute enough :whistle:.......
......Our results provide strong evidence that facial appearance has important effects on choice of leader. We have
shown that differences in facial shape alone between candidates can predict who wins or loses in an election.....
Facial appearance affects voting decision , Journal of Evolution and Human Behavior (2007)........