Kusaini kwenye vitabu getini

Kusaini kwenye vitabu getini

CHIKIRA MTABARI kuna siku usioijua huo utaratibu unaweza kukusaidia. Labda ulikwenda ofisi fulani ukakaa kuanzia saa nne hadi sita. Bahati mbaya ukahusishwa na tukio la kihalifu muda huo huo. Hio saini yako kwenye hicho kitabu inaweza kukuokoa kama alibi.
 
Ahsante sana PRONDO
 
Hakina maana yoyote! Labda kile cha ndani guest register lakini hivi vya walinzi waviondoe tu,waweke cctv getini tosha.kama mtu anania mbaya ataingia halmashauri kufanya nini?
Nimevutiwa na mawazo yako ahsante
 
mimi naona lengo lao na utaratibu ni mzuri sana sema vifaa, vitendea kazi vyao ndo viko duni sana pale palitakiwa pawepo mashine za kisasa kabisa.
Tatizo hali ya uchumi sio nzuri kuweka hivyo vifaa!!!
 
Pale PPF na NSSF nao wanautaratibu huo tena wao unakaguliwa na mashine kabisa. Nzuri kwa usalama
 
Hakina maana yoyote! Labda kile cha ndani guest register lakini hivi vya walinzi waviondoe tu,waweke cctv getini tosha.kama mtu anania mbaya ataingia halmashauri kufanya nini?
kaka ukiingia kwenye jengo la mtu bila ruhusa ni kuvunja sheria
 
Wakati mwingine inasaidia inapotokea maafa. Kuporomoka kwa jengo. Inasaidia kujua idadi ya watu walokuwa ndani ya jengo
 
Pale PPF na NSSF nao wanautaratibu huo tena wao unakaguliwa na mashine kabisa. Nzuri kwa usalama
Hata hapa Mwanza nina baadhi ya majengo marefu wana huo utaratibu mfano hotel ya Gold Crest, Ecaclif na mengineyo. Natamani ofisi na mejengo mengine hata kama sio marefu wawe na huo utaratibu kwa ajili ya usalama. Isije ikawa kama huko MANCHESTER waliokuwa wanaserebuka halafu magaidi wakaharibu hali ya hewa
 
Habarini wana JF.

Mie huwa sielewi utaratibu unaotumiwa na ofisi mbalimbali za umma, kwa mfano hapa Mwanza nimeona utaratibu huo unatumika mageti ya kuingilia ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

Unapoingia getini (mgeni), walinzi wanataka uandike kwenye "kauntabuku" ukionyesha majina yako kamili, sehemu unapotoka, namba yako ya simu, ofisi unayokwenda, muda wa kuingia na kutoka.

Huwa najiuliza hivi utaratibu huu ni kutaka kupata idadi ya wageni waliotembelea ofisi hizo au ni kwa ajili ya usalama. Na kama ni kwa ajili ya usalama hivi mgeni ambaye ana nia ovu ataweka details zake za ukweli?!!

Ofisi za umma mnaotumia huu utaratibu huu, badilikeni. Tumieni mitambo ya kisasa kuwakagua wageni kubaini kama wana silaha za kudhuru au la!!

Ni kukulinda pia na wewe mwenyewe itakapotokea kuna madhara. Hilo kaunta buku liliwahi kumuokoa mtu asiende jela kwa kuwa kithibitisho cha yeye kutokuwepo eneo la mauwaji kama alivyosingiziwa!
 
Ni kukulinda pia na wewe mwenyewe itakapotokea kuna madhara. Hilo kaunta buku liliwahi kumuokoa mtu asiende jela kwa kuwa kithibitisho cha yeye kutokuwepo eneo la mauwaji kama alivyosingiziwa!
Aiseee!! kweli nimekubali kuanzia sasa nitasaini bila kinyongo
 
Huu utaratibu hauna hata maana mkuu! Maana siyo kweli kwamba taarifa zote ni sahihi kuhusiana na hao wageni.

Labda wanataka tu kujua traficking ya watu katika hizo ofc
 
Back
Top Bottom