Kusaini kwenye vitabu getini

Kusaini kwenye vitabu getini

Tatizo watanzania wengi hasa wakina baba hawakipendi kale kadude ka "kupapasa" wanasema kana mionz ambayo INA athari, ya kupunguza nguvu ya kusaka "watoto"

Heeeeee, kumbe!!!!!
 
Utaratibu wa wizara ya nishati na madini makao makuu ni mzuri, ungeigwa kwenye ofisi zote.

Kwao unaandika majina na kuwaachia identity card yako, then wanakupa electronic card ambayo ndio itakupa access kuingia ndani as milango yao ipo electronically secured. Pale huwezi kuchomoa kirahisi hata kama una nia ovu.

Ukienda embassies nyingi unaacha identity card, wanaku-scan kama kiroba na unaandika majina yako kamili, huwezi kuchomoa kirahisi.
Aiseee kumbe, ahsante Eli79 kwa kuchangia mawazo yako
 
Kumbe inaweza kutumika kama alibi??

Naonaga kwenye kideo tu mambelez wanatumia hadi risiti za kwenye stores.

Nikejifunza kitu hapa
Hata mimi nimejifunza aisee
 
kujua idadi ya walio hudumiwa kwa mwaka au mwezi
kujua marehem au majeruhi ikiwa jengo linaanguka au laa
kukwepa kesi hasa za kusingiziwa km eneo la tukio halikuhusu
kupunguza vishoka na watu wasio na kazi kwenye ofisi za umma nk
Ahsante sana kwa maelezo yako "matamu"
 
Huo ni utaratibu mzuri mtu ambaye hataki kusaini kwenye daftari hilo ndio ana matatizo. Kusaini kwenye daftari kuna faida nyingi sana. Tena nawasahuri wanaoandika taarifa Zao kwenye daftari waweke taarifa za ukweli
Shukrani
 
Mkuu, utaratibu wa kusaini ni utaratibu mwema na wenye manufaa makubwa. Katika mahakama zetu, yupo mtu aliwahi kukwepa kitanzi kwa daftari kama hilo tu kuwasilishwa mahakamani. Alionekana alikuwa mbali na tukio wakati likitokea
Heeee! kumbe. Aiseee, ahsante sana
 
wewe ni muhaifu wa kariba fulani ktk hizo ofisi za umma..!!!..
uvumilivu umekushinda mkuu.....jipange na plan B...
 
Habarini wana JF.

Mie huwa sielewi utaratibu unaotumiwa na ofisi mbalimbali za umma, kwa mfano hapa Mwanza nimeona utaratibu huo unatumika mageti ya kuingilia ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

Unapoingia getini (mgeni), walinzi wanataka uandike kwenye "kauntabuku" ukionyesha majina yako kamili, sehemu unapotoka, namba yako ya simu, ofisi unayokwenda, muda wa kuingia na kutoka.

Huwa najiuliza hivi utaratibu huu ni kutaka kupata idadi ya wageni waliotembelea ofisi hizo au ni kwa ajili ya usalama. Na kama ni kwa ajili ya usalama hivi mgeni ambaye ana nia ovu ataweka details zake za ukweli?!!

Huwa nina kereka kweli hasa unapomuona "kamanda" kakomaa kweli kweli kutaka watu watie sahihi zao vitabuni.

Ofisi za umma mnaotumia huu utaratibu huu, badilikeni. Tumieni mitambo ya kisasa kuwakagua wageni kubaini kama wana silaha za kudhuru au la!!

Mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuu acheni kutusumbua kwenye mageti yenu watu tuna haraka zetu. Alaaaaaaaaaa!!!!!!!!!🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁
kaka kaka nakuomba sana tena sana ukikuta kitabu saini ndugu au kama hakipo omba upewe walioweka siyo wajinga mkuu. Je ukiambiwa unaingi kwa ajili ya uhalifu utajibuje acheni hizi kitu
 
Kwao unaandika majina na kuwaachia identity card yako, then wanakupa electronic card ambayo ndio itakupa access kuingia ndani as milango yao ipo electronically secured. Pale huwezi kuchomoa kirahisi hata kama una nia ovu.
Mkuu yaani hata kuingia manispaa au kwenye halmashauri zetu tuige hiyo technology daah!! Hizi ni sehemu ambazo walala hoi ndio sehemu zao halafu uwavalishe tag access card,simply utakuwa umewatisha na hawatarudi tena.watakuwa wanalalamikia kwenye vijiwe vya kahawa tu.
 
Kusaini kitabu ni kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi. Wanaweza kuzitumia hizo kumbukumbu kuboresha huduma zao wanazotoa. Isaidia pia katika shughuli za ulinzi na usalama. Ni muhimu kuandika majina yako sahihi.
 
kaka kaka nakuomba sana tena sana ukikuta kitabu saini ndugu au kama hakipo omba upewe walioweka siyo wajinga mkuu. Je ukiambiwa unaingi kwa ajili ya uhalifu utajibuje acheni hizi kitu
Ahsante mob kwa ushauri wako ila mimi DADA
 
Kusaini kitabu ni kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi. Wanaweza kuzitumia hizo kumbukumbu kuboresha huduma zao wanazotoa. Isaidia pia katika shughuli za ulinzi na usalama. Ni muhimu kuandika majina yako sahihi.
Shukurani, mfumwa, kikore mathewa
 
Mkuu yaani hata kuingia manispaa au kwenye halmashauri zetu tuige hiyo technology daah!! Hizi ni sehemu ambazo walala hoi ndio sehemu zao halafu uwavalishe tag access card,simply utakuwa umewatisha na hawatarudi tena.watakuwa wanalalamikia kwenye vijiwe vya kahawa tu.
hahahahaaha, tehe tehe tehe
 
kaka kaka nakuomba sana tena sana ukikuta kitabu saini ndugu au kama hakipo omba upewe walioweka siyo wajinga mkuu. Je ukiambiwa unaingi kwa ajili ya uhalifu utajibuje acheni hizi kitu
Hakina maana yoyote! Labda kile cha ndani guest register lakini hivi vya walinzi waviondoe tu,waweke cctv getini tosha.kama mtu anania mbaya ataingia halmashauri kufanya nini?
 
mimi naona lengo lao na utaratibu ni mzuri sana sema vifaa, vitendea kazi vyao ndo viko duni sana pale palitakiwa pawepo mashine za kisasa kabisa.
 
Back
Top Bottom