Kusaini kwenye vitabu getini

Kusaini kwenye vitabu getini

JF huwa tunashirikishana maujuzi, mie nimiliona hilo kwa mabaya, naomba na wewe Tajirimsomi unisaidie mazuri yake. Natanguliza shukrani zangu za dhati, wako mtiifu, CHIKIRA MTABARI
Ngoja ntakujibu.

Eneo ulilolitaja ndo kibaruani kwangu ngoja niwaulize wakuu wangu uo utaratibu una faida gani
 
Ngoja ntakujibu.

Eneo ulilolitaja ndo kibaruani kwangu ngoja niwaulize wakuu wangu uo utaratibu una faida gani
Angalia usije ukaonekana umeuliza swali la kichokozi na kichochezi halafu ukamwaga unga, hahahahahaha. nakutakia siku njema mwaya
 
kujua idadi ya walio hudumiwa kwa mwaka au mwezi
kujua marehem au majeruhi ikiwa jengo linaanguka au laa
kukwepa kesi hasa za kusingiziwa km eneo la tukio halikuhusu
kupunguza vishoka na watu wasio na kazi kwenye ofisi za umma nk
 
Huo ni utaratibu mzuri mtu ambaye hataki kusaini kwenye daftari hilo ndio ana matatizo. Kusaini kwenye daftari kuna faida nyingi sana. Tena nawasahuri wanaoandika taarifa Zao kwenye daftari waweke taarifa za ukweli
 
Nimekuelewa vizuri Erickford4, kumbe utaratibu huu ni kwa faida ya wateja wa nje wanaotembelea ofisi zile, sasa vipi kwa upande wa usalama wa watumishi na mali za ofisi ile. Si umeshasikia ile story kwamba kuna majambazi yalienda ofisi Fulani yana silaha yakaingia ndani yakamteka mtunza fedha awapatie fedha zote zilizokuwa kwenye kasiki!

Kuhusu hayo majambazi hilo ni suala lingine halihusiani kabisa na hilo daftari kuna baadhi ya ofisi au vituo vya polisi wanakuandikia SIMAMA UKAGULIWE.

Na ukisimama hapo wanakukagua aidha kwa mashine (kama ipo) au kwa kukupapasa lakini suala la kuandika kumbukumbu zako kwenye daftari lipo palepale..

Kwa hiyo suala la daftari la kumbukumbu na tukio la ujambazi haviendani mkuu.
 
Kuhusu hayo majambazi hilo ni suala lingine halihusiani kabisa na hilo daftari kuna baadhi ya ofisi au vituo vya polisi wanakuandikia SIMAMA UKAGULIWE.

Na ukisimama hapo wanakukagua aidha kwa mashine (kama ipo) au kwa kukupapasa lakini suala la kuandika kumbukumbu zako kwenye daftari lipo palepale..

Kwa hiyo suala la daftari la kumbukumbu na tukio la ujambazi haviendani mkuu.
Ahsante mkuu, sasa umenielewesha mubashara kuwa "kauntabuku" zile ni kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi na si vinginevyo. Nakushukuru sana Erickford4. Barikiwa
 
Mkuu ujue kitechnolojia bado tupo nyuma sana hatuna vifaa na watumiaji wa vifaa hawapo, huu utaratibu unamsaidia mlinzi pindi likitokea tatizo, vumilia tu mkuu bado sisi ni ulimwengu wa tatu.
Tatizo gani kwa mfano? Na Je kama katoa details za uongo?
 
Mfano kikitokea cha kutokea labda jengo likalipuka, inakuwa rahisi kujua nani na nani walikuwa ndani na hivyo ndugu wa waathirika kupata habari.
Kama wameandika majina sahihi na kwa muandiko unaosomeka.
 
Hapo halmashauri mbona sio shida na hkn usumbufu kujaza hicho kitabu.
Ukienda Rita ya dar ndio utashangaa hio foleni ya kujaza majina yako kwenye kitabu.
 
Mkuu, utaratibu wa kusaini ni utaratibu mwema na wenye manufaa makubwa. Katika mahakama zetu, yupo mtu aliwahi kukwepa kitanzi kwa daftari kama hilo tu kuwasilishwa mahakamani. Alionekana alikuwa mbali na tukio wakati likitokea

Kumbe inaweza kutumika kama alibi??

Naonaga kwenye kideo tu mambelez wanatumia hadi risiti za kwenye stores.

Nikejifunza kitu hapa
 
Utaratibu wa wizara ya nishati na madini makao makuu ni mzuri, ungeigwa kwenye ofisi zote.

Kwao unaandika majina na kuwaachia identity card yako, then wanakupa electronic card ambayo ndio itakupa access kuingia ndani as milango yao ipo electronically secured. Pale huwezi kuchomoa kirahisi hata kama una nia ovu.

Ukienda embassies nyingi unaacha identity card, wanaku-scan kama kiroba na unaandika majina yako kamili, huwezi kuchomoa kirahisi.
 
Kwani huyo kibaka na mhuni anashindwa kusaini kwenye hiyo kaunta buku na kwenda kufanya yake?! ndio maana nikasema hivi huo utaratibu hauna tija. Hizi halmashauri nilizozitaja wajitahidi wanunue kale "kadude ka kupapasa mtu" akiingia pale getini
Tatizo watanzania wengi hasa wakina baba hawakipendi kale kadude ka "kupapasa" wanasema kana mionz ambayo INA athari, ya kupunguza nguvu ya kusaka "watoto"
 
Back
Top Bottom