Habarini wana JF.
Mie huwa sielewi utaratibu unaotumiwa na ofisi mbalimbali za umma, kwa mfano hapa Mwanza nimeona utaratibu huo unatumika mageti ya kuingilia ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
Unapoingia getini (mgeni), walinzi wanataka uandike kwenye "kauntabuku" ukionyesha majina yako kamili, sehemu unapotoka, namba yako ya simu, ofisi unayokwenda, muda wa kuingia na kutoka.
Huwa najiuliza hivi utaratibu huu ni kutaka kupata idadi ya wageni waliotembelea ofisi hizo au ni kwa ajili ya usalama. Na kama ni kwa ajili ya usalama hivi mgeni ambaye ana nia ovu ataweka details zake za ukweli?!!
Ofisi za umma mnaotumia huu utaratibu huu, badilikeni. Tumieni mitambo ya kisasa kuwakagua wageni kubaini kama wana silaha za kudhuru au la!!