Kusaidia wenye uhitaji ni baraka

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Nilikutana na mama mmoja ana real estate, nyumba zake hazipungui 20. Nilikua na hamu ya kufahamu alianzaje. Aliniekeza kuwa alipata ajira yake ya kwanza akiwa na miaka 26. Kazi ilikua nzuri na hakua na maisha ya anasa. Alinunua kiwanja na kujenga nyumba ya nyuma kuanzia. Ilkua na vyumba viwili self contained.

Kuna siku alikaa nyumbani, mama yake alimfahamisha kuwa wanatoka kwenye msiba. Wakawa wanahadithia jinsi watu wasivyo na Utu. Mwenye nyumba amewaeleza ndugu wa marehemu kuwa anahitaji nyumba yake mara baada ya msiba. Aliwavumilia kwa muda mrefu waliishi bila kukipa kodi. Muda huu wakikua wanamuuguza marehemu.

Yule mama aliifuatilia hii habari, aliweza kuonana na mjane. Alimwambia ahamie kwenye nyumba yake akae mpaka atakapo jipanga. Bahati nzuri mjane ni mwakiriwa, alimufu gharama za maji na umeme. Watoto wake waliendelea na shule na yule mama alihangaika.

Baada ya miaka saba yule mjane alimkabidhi nyumba yake. Wakati huu huyu mwenye nyumba aliamua kuikarabati kidogo ili apate mpangaji mwingine. Alipata offer, kuna muwekezaji amefungua ofisi jirani yake na anataka eneo la kijenga godown. Offer aliyopewa ilikua nzuri sana.

Aliweza kununua viwanja vinne na kujenga taratibu. Nyumba ya kwanza ilipokwisha alipata shirika, alipata kodi ya mwaka mmoja kwa mkupuo. Aliendelea kujenga ya pili. Baada ya hapo nyingine zilifuatia. Lakini baraka kubwa ilikuja baada ya mjane kumkabidhi nyumba yake.

1621322295483.png

 
Wengi hawalitambui Hili... Mungu ambariki Sana dada Gladness. Bila yeye, leo Mimi ningekuwa shambanoi au natangatanga kulisha ng'ombe za watu mijni. Hakunijua, sikumjua na Hata hatukuwa kabila moja. Lakini aliamua kunisomesha japo kipato chake kilikuwa kidogo.
 
Kuna baraka kubwa ktk Kuimiza na kulisha yatima na maskin. Unapowa gusa hawa yatimabumegysa Aliyekuumba. Ndio maana nae haachi kumlipa yule mama kwa kuwasitiri hao ndugu kwa moyo
 
Back
Top Bottom