Kusaidia jamii inayokuzunguka

Kusaidia jamii inayokuzunguka

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,349
Wengi wetu hatuelewi matatizo katika jamii inayotuzunguka. Si lazima uwe tajiri ili uweze kuisaidia jamii. Kidogo ulichonacho kinaweza kubadilisha maisha ya mtu.

Nilikuwa ninaangalia African Channel siku moja, nilimuona baba mmoja Mnigeria ni tajiri anayeishi Marekani. Huyu tajiri biashara yake ilianzia kwenye mafuta Nigeria lakini sasa hivi ana vitega uchumi vingi vikubwa Marekani.

Anasomesha wanafunzi 20 kila mwaka kutoka Nigeria wasio na scholarship. Anawalipia tuition fees na accommodation mpaka wamalize shule.

Unaweza kununua kilo 10 za sukari kuwasaidia wasiojiweza. Kama hutaki ujulikane unaweza kumpa Imam, Paroko au mchungaji.

Kuna kisa nilikutana nacho Arusha. Chalii mmoja wa Mererani alimjengea mjane nyumba self contained umeme na maji na akamwambia mama usinipe asante ila niingize kwenye sala zako za kila siku kwa Mungu. Ni baada ya kusikia mama anafukuzwa kwenye nyumba kwa kukosa kodi.

Unapotoa usitegemee asante, fanya hayo kwa kumshukuru Mungu kwa kile alichokupa. Christmas inakuja, kuna familia haziwazi hata sikukuu itakuwaje matatizo ni mengi. Kuziwezesha familia hizi kula mlo wa sikukuu si jambo dogo. Fikiria.
 
Usiseme umepoteza kitu, bali sema nimekirudisha kwa wenyewe, kwa kuwa kila ulichonacho siyo mali yako ya kudumu, bali umepewa utumie kwa muda, ipo siku kitarudi kilipotoka. Hivyo tumia vizuri kila ulichonacho sasa.
 
Unapotoa usitegemee asante, fanya hayo kwa kumshukuru Mungu kwa kile alichokupa. Christmas inakuja, kuna familia haziwazi hata sikukuu itakuwaje matatizo ni mengi. Kuziwezesha familia hizi kula mlo wa sikukuu si jambo dogo. Fikiria. Sky Eclat,
 
Sky Eclat,

Hua nashangaa sana!

Hii ni social narcissism!

Kutoa msaada kwa jamii infact ni kuzidi kulea matatizo zaidi

Na hao waliotoa msaada infact isingetakiwa tujue chochote

Wanajifanya kufundisha wenzao what to do sababu ya publicity tu hakuna roho genuine hapo!

Kutoa msaada ni overrated mno!

Huwezi saidia mtu kama huna surplus!

Kutoa hasa ni wakati hata surplus huna, hii no one can do!

Watoa misaada ni ma-narscissitic maniacs!

They talk too much!
 
Mwaka jana kipindi kama hiki cha kukaribia xmas kuna mdada alinitumi elfu kumi. Kabla ya mwaka mpya akapata mchumba. Kuna trafik police alinitumia elfu hamsini. Kabla ya mwaka mpya akapandishwa cheo. Kuna mwana CCM alinitumia laki, juzi kashinda bila kushindana. Kuna konda alinirudishia chenji badala ya mia sita kanipa elfu tisa mia sita sasa hivi ni dereva na leseni juu.
Sikuambii unitumie pesa ila ukiangalia huo mtiririko huhitaji kuambiwa ona.
 
Ww jamaa bana!!
kundi likiwa linaelekea kulia...
ww unajitenga unaenda kushoto!!?
kundi likielekea kushoto.....
unajitenga unaenda upande wa kulia..
anyway ndio brand yako lkn.,
Na kwanini ufuate mkumbo wa kundi limeelekea wapi, jifunze kusimamia mawazo yako hata kama yanakinzana na majority, kuwa tofauti na wengine si dhambi.
 
Na kwanini ufuate mkumbo wa kundi limeelekea wapi, jifunze kusimamia mawazo yako hata kama yanakinzana na majority, kuwa tofauti na wengine si dhambi.
Hakuna ubaya wwte....
nime-highlight character yake....
infact anaweza kuwa sahihi kuliko kundi
 
Mwaka jana kipindi kama hiki cha kukaribia xmas kuna mdada alinitumi elfu kumi. Kabla ya mwaka mpya akapata mchumba. Kuna trafik police slinitumia elfu hamsini. Kabla ya mwaka mpya akapandishwa cheo. Kuna mwana CCM alinitumia laki, juzi kashinda bila kushindana. Kuna konda alinirudishia chenji badala ya mia sita kanipa elfu tisa mia sita sasa hivi ni dereva na leseni juu.
Sikuambii unitumie pesa ila ukiangalia huo mtiririko huhitaji kuambiwa ona
Namba yako tafadhari mkuu.
 
Nimecheka had nimehis vichomi🤣🤣🤣
 
Ww jamaa bana!!
kundi likiwa linaelekea kulia...
ww unajitenga unaenda kushoto!!?
kundi likielekea kushoto.....
unajitenga unaenda upande wa kulia..
anyway ndio brand yako lkn.,

Tunaitwa Contrarians!

Shida ni kwamba,watu hawapendi views from the other bad side!

Wanapenda vitu vizuri vizuri tu!

Lazima watu waelewe kuna different way of viewing things,sio angle moja tu ambayo ni obvious!
 
Mungu anataka tumpende, ukipenda Mungu, anamsogeza Mwanadamu karibu ili umpende huyo. Kumpenda Mungu bila mwanadamu ni kama haiwezekani. Mungu, mwanadamu upendo unakamilika.
 
Unapotoa usitegemee asante, fanya hayo kwa kumshukuru Mungu kwa kile alichokupa. Christmas inakuja, kuna familia haziwazi hata sikukuu itakuwaje matatizo ni mengi. Kuziwezesha familia hizi kula mlo wa sikukuu si jambo dogo. Fikiria.
Mbona kichaa anaposaidia watu anataka asifiwe na Kila mtu, anapenda Sana sifa lakini mnakaa kimya tu
 
Mwaka jana kipindi kama hiki cha kukaribia xmas kuna mdada alinitumi elfu kumi. Kabla ya mwaka mpya akapata mchumba. Kuna trafik police alinitumia elfu hamsini. Kabla ya mwaka mpya akapandishwa cheo. Kuna mwana CCM alinitumia laki, juzi kashinda bila kushindana. Kuna konda alinirudishia chenji badala ya mia sita kanipa elfu tisa mia sita sasa hivi ni dereva na leseni juu.
Sikuambii unitumie pesa ila ukiangalia huo mtiririko huhitaji kuambiwa ona.
Tuwekee na namba yako ya simu mkuu...
 
Back
Top Bottom