Kusaga: Clouds FM haina chama! Akanusha Clouds kununuliwa na Rostam Aziz

Kusaga: Clouds FM haina chama! Akanusha Clouds kununuliwa na Rostam Aziz

Tutawajua tu kwa matendo yao. Maneno eke yake hayatoshi
 
Kama umemuelewa dhumuni la mtoa mada ni kwamba Clouds Media waliandaa Sherehe ya bday ya Mh Rais sasa nayeye ameshauri kama hawana chama wana balance basi wamuandalie sherehe ya kuzaliwa Lema au hata mbowe(nimeongeza mimi)


Mkuu bila kusahau majuzi hapa wakati @Nchemba akidanganya umri wake kwa dunia nzima aliitumia clouds FM na wakampa zawadi ya Cake kabisa studio kwenye kipindi cha Power Breakfast
 
waongo wakubwa hao,hata kwenye uchambuzi wa magazeti,habari za upinzani huwa wanapitisha putisha tu headings.
lakini habari za ccm PJ na hando wanachambua na kuingia deep huku barba akichombeza kimtindo.
 
toleo la MAWIO la jana,limeripoti kikamilifu clouds kutumika na CCM kisiasa na kipropaganda!!

clouds fm wameshiriki kuandaa na kuomba zaidi ya 2.5 bln kutoka Ikulu kwa ajili ya propaganda ya kuhimiza kura ya ndio ya kura ya katiba ya CCM,mchanganuo huo umeandikwa na RUGE MUTAHABA ukihusisha pia wanamziki wa clouds kwa wingi walio chini ya THT!!!

Kusaga wala RUGE hawawezi kukili waziwazi ila watambuzi wa mambo wanajua na wao pia unafiki wao wanaujua,wao kwao ni pesa tu kwanza!!!!

Kama wanafanya haya kama njia ya kujitaftia pesa sasa shida inakuwa wapi?

Wasipochakalika kutafta pesa kwa njia zote wewe ndo utaenda kuwalipia mishahara wafanyakazi?

Watu wengine bwana sijui mna matatizo gani.. kampuni kutumia fursa kama hiyo kutengeneza pesa ina tatizo gani?

Tatizo lenu ili mlidhike kama hawana upande wowote mnataka wafanye siasa zenye mlengo mmoja wa upinzani kama ITV, Tanzania Daima na Mawio wafanyavyo ndio muwaone wako fair?
 
huwa najiuliza sana kw nn jambo la clouds linapewa nafas kubwa xana JF. clouds ni kampuni na iko kibiashara. Je wao na biashara zao jf ina2husu nn? Na kama hupend clouds wanavyoendesha mambo yao chagua radio nyingine na si kulalamika.
 
Kama kuna wafanyakazi ambao ni ccm na wanaitumia radio kutangaza habari za kipropaganda za ccm bila kuchukuliwa hatua na uongozi kama ilivyo Kibonde,tafsiri yake ni kuwa uongozi umebariki yafanyikayo. Swali alilomwuliza Hando halikuwa swali sababu jibu lake lilikuwa dhahiri kuwa hawezi kukubali sababu ni kinyume cha sheria kama alivyosema .
 
Kama wanafanya haya kama njia ya kujitaftia pesa sasa shida inakuwa wapi?

Wasipochakalika kutafta pesa kwa njia zote wewe ndo utaenda kuwalipia mishahara wafanyakazi?

Watu wengine bwana sijui mna matatizo gani.. kampuni kutumia fursa kama hiyo kutengeneza pesa ina tatizo gani?

Tatizo lenu ili mlidhike kama hawana upande wowote mnataka wafanye siasa zenye mlengo mmoja wa upinzani kama ITV, Tanzania Daima na Mawio wafanyavyo ndio muwaone wako fair?

mkuu hapa ndio mwisho au bado unaendelea.
 
ni wazi kwamba hiyo radio station inatumika na ccm,huitaji elimu kuona hilo
 
Ukiwa mahakamani lazima ukane kila kitu.
 
Kimsingi Joe hajaishambulia JF ......amesema huo ni uzushi kutoka mitandaoni hasa Jamii Forums .....nadhani amesema ukweli maana habari nyingi huanzia huku .......amelea sana akina Kibonde kudhalilisha wapinzani wazi na hii imejengea maadui wengi ile radio tofauti na ilivyokuwa ikipendwa mwanzo ........

Kuhusu Clouds kuuzwa anajua mwenyewe ........
 
huwa najiuliza sana kw nn jambo la clouds linapewa nafas kubwa xana JF. clouds ni kampuni na iko kibiashara. Je wao na biashara zao jf ina2husu nn? Na kama hupend clouds wanavyoendesha mambo yao chagua radio nyingine na si kulalamika.
Shule gani umesoma ya kuchanganya herufi na namba.?
 
Haya bwana kusaga...ila hili la uccm kulipinga ni ngumu maana lipo dhahiri kabisa.
 
huwa najiuliza sana kw nn jambo la clouds linapewa nafas kubwa xana JF. clouds ni kampuni na iko kibiashara. Je wao na biashara zao jf ina2husu nn? Na kama hupend clouds wanavyoendesha mambo yao chagua radio nyingine na si kulalamika.

Mkuu hizi ndo hasara za mafanikio... ukitaka kujua kama umefanikiwa hasa kwa afrika basi angalia watu wanavyokusema vibaya... kama unasemwa vibaya sana jua umefanikiwa kuliko wao. Sio Clouds tu inayosemwa vibaya angalia hata wasanii wetu kama akina Diamond wanasemwa vibaya kisa mafanikio au enzi zile Kanumba alipokaribishwa BBA alikandiwa sana na kingereza chake. Me naona tatizo ni Nyota.

Tanzania imejaa wachawi na wengi wao hawajijui kama ni wachawi.

Kampuni binafsi na sio ya umma lakini watu wako busy kwenye mtandao kutoa mapovu na kutoa maelekezo ni namna gani iendeshwe.. mbona wakati wanaanza hammkuwapa ushauri? Iweje wamefanikiwa ndo mnakimbizana kutoa ushauri na lawama kwenye mitandao? Yote ni wivu tu wa maendeleo.

Kama ni wivu basi kuwa postive lakini watu wengine wapo negative hawataki kujifunza kitu. Wamekalia majungu kwenye mitandao huku wakilalamikia ukosefu wa ajira.. sasa niwaulize hao akina Kusaga na Ruge waliwahi kuajiriwa wapi hapo kabla ili tupime malalamiko yako?

Napenda nitoe shukrani za dhati kwa TCRA kwa kushirikiana na Makampuni ya Simu kuweza kupunguza Vifurushi vya internet hadi Mb8 kwa Mb60. Walau itapunguza wimbi la vijana wanaoshinda kwenye mitandao bila kazi za kueleweka za kupiga majungu na domo.

Ukiona media haikupendezi hamia nyingine kwani hujalazimishwa kusikiliza badala ya kuleta malalamiko ya kipuuzi kwenye mitandao. Sio kila upuuzi uuwazao lazima uandikwe hapa kwenye mitandao.
 
Kimsingi Joe hajaishambulia JF ......amesema huo ni uzushi kutoka mitandaoni hasa Jamii Forums .....nadhani amesema ukweli maana habari nyingi huanzia huku .......amelea sana akina Kibonde kudhalilisha wapinzani wazi na hii imejengea maadui wengi ile radio tofauti na ilivyokuwa ikipendwa mwanzo ........

Kuhusu Clouds kuuzwa anajua mwenyewe ........
Ni kweli maana inaaminika Rostam ndio tajiri zaidi Tanzania ila miradi yake haieleweki vizuri.
 
Ukweli upo wazi. Clouds ni mouthpiece ya ccm na inatumika kuendeleza maslahi ya ccm. Hata review ya magazeti asubuhi kama kuna issue inakandia ccm hawasomi, ushahidi upo. Kama Kusaga anabisha basi akubali kuhojiwa na waandishi ambao wako huru na siyo hao ambao wako kwenye pay roll yake.
 
Back
Top Bottom