Kusaga: Clouds FM haina chama! Akanusha Clouds kununuliwa na Rostam Aziz

Kusaga: Clouds FM haina chama! Akanusha Clouds kununuliwa na Rostam Aziz

Amekanusha taarifa za Clouds FM kununuliwa na Rostam Aziz.

Kwani anachaguliwa mahali pa kuuza kitu chake. Haina maaana nikimuuzia mtu kitu ndio mimi niko hicho chama. Pia kukanusha au kutokukanusha wengine inatuhusu nn?
 
Kusaga ni CCM pure, na hata radio station yake inasambaza propaganda kuhusu vyama vya upinzani, kuhusu katiba na mambo yote hasi yanayoihusu serikali, hakuna siku moja nimesikia wanatoa habari zinazohusu mambo mabaya ya serikali, badala yake watatafuta namna yoyote ya kuisafisha serikali ya CCM, hata viongozi wa CCM, ili wapate ulaji...

Kusaga na clouds mtakuwa na lakujibu siku ya siku mambo yakishaharibika, endelea kufurahia tenda na bakshishi unazopata wakati huu
 
Kulikua na uzushi siku mbili tatu zilizopita kuwa clouds Fm imeuzwa kwa Rostam Aziz na mtoa mada aliandika akiwa na uhakika sana kwamba ameambiwa na mtu wa karibu na clouds, Leo the big boss CEO wa clouds Bwana Joseph Kusaga amekanusha na kusema kuwa ni uzushi wa watu either wanaokaa bila kazi au watumiaji wa madawa ya kulevya au wapinzani wake wa kibiashara ndio wanaosambaza uzushi

MY TAKE: Yule jamaa aliyesema amepata taarifa za ukweli sasa sijui ametoa wapi, anaweza akawa yuko Right but in the wrong position
 
Aache unafiki, Clouds ni CCM.

Afadhali umeliona ilo! Wote tunafahamu kiherehere cha kibonde na alivyowakejeli madaktari nao wakamkumbusha namna walivyomsaidia halafu leo hii kusaga anataka kutudanganya hajui motive ya kituo chake?
 
Clouds kwa ujumla wake linafaham fika kuwa Chadema ilivyo na wafuasi wengi especially vijana ambao ndio wasikilizaji wao wakubwa so wakijichanganya tu waitajetaje walau kwa cku mbili basi ccm hawana chao.

Huwa wanawapa airtime kidogo NCCR ambayo wanajua wahana nguvu au kujidai kuwapigia cmu CUF kuwahoji viongoz wao ILA hawawez kamwe kufanya hvyo kwa CHADEMA kwa kua wanafahamu fika kwa kufanya hvyo ni sawa na kuwasha moto nyikani kwan utashika kwa kasi na CCM itakua mwisho wao.
 
Clouds fm wamekana kuwa shutuma zinazotolewa kwenye social media hasa jamiiforums kwamba wao CCM sio za kweli.

Akihojiwa CEO wa clouds katika kipindi power breakfast, amesema wao kama radio hawana chama kwa sababu hata sheria TCRA haziruhusu.

Pia kwenye uchaguzi wa mwaka huu wagombea wote watapewa nafasi sawa.

Ameendelea kusema kuwa wafanyakazi wachache kuwa CCM haimaanishi clouds yote ni CCM.

Pia clouds imekanusha habari zilizozagaa kuwa radio imenunuliwa na Rostam Aziz, ameongeza kuwa hizo ni propaganda za kuichafua radio hiyo.

Amesema kama wakiuza radio watatangaza kwasababu radio ni yao,na hawamuogopi mtu.

Wakati wanamuhoji nimesikia wanamuita Joh (labda ndiye Joseph Kusaga) sina uhakika na majina mengine,wanomfahamu watatujuza.

Wanafiki wakubwa ninyi!
 
Miaka 10 mfululuzo tangu JK aingie madarakani,wamemuacha kibonde afanye siasa redioni,hawakutoa tamko kama hili.Leo hii 2015 wanatoa tamko wana hofia nini au wameona dalili gani?.

Hata mimi siwaelewi hawa Clouds! Miaka yote wamemuacha BABA FANUELI afanye siasa za maji taka kupitia cloud hawakukemea. Leo wanaona JK karibu anatoka madarakani wanatafuta sehemu ya kujiengemeza.

Janja ya Nyani .. tumeshaijuia Cloud FM.
 
Habari Wanabodi,

Akizungumza moja kwa moja kutoka Abu Dhabi,CEO wa Clouds Media Ndugu Joseph Kusaga ametamka wazi mtandao wa JF unamuandika vibaya kwamba redio yake ni ya CCM,amesema kwamba radio yake haina chama,anafuata sheria za TCRA,kama kuna mfanyakazi wake anashabikia chama flani basi akirudia tena atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Amesema kama clouds FM ingekuwa ina ushabiki na vyama basi ingekuw ya chadema maana Mbowe ni rafiki yak mkubwa sana wamefahamiana zaidi ya miaka 30.

Nawasilisha.

Hata Le Mutuz hujinadi kuwa Mbowe ni rafiki yake wa muda Mrefu

Kwanza ni jambo la ajabu mtu mwenye exposure kama huyo Kusaga kuishambulia JF wakati anajua JF ni mtandao ambao watu wanaandika na kuleta data.Yeye angekanusha tu badala ya kwenda mbali na kuituhumu JF

Anakua kama sio mwanahabari bwana
 
clouds imechukiwa kwa uccm wake, kwa sasa clouds inapendwa na wasichana wa shule za msingi na form two.

efm habari ya mjini
 
Back
Top Bottom