Kurudi nyumbani na kujipanga upya

Kurudi nyumbani na kujipanga upya

Habari wana JF.

Mie ni kijana nimeona na nina watoto wawili. Kimaisha sipo vibaya sana nashukuru Mungu. Changamoto kubwa inayonipa hardtime ni Kodi ninazolipa kwa ujumla kuanzia kwenye biashara mpaka nyumba ya kupanga ninayoishi,najiona nimekua na mzigo mkubwa wa kulipa kodi mpaka nashindwa fanya moves nyingine.

Nimewaza kitu ambacho sijui nitafikiriwa vipi na wanaonizunguka ila kwa upande wangu naona itakua ni ahueni!!

Nimewaza kuhama nilipopanga na nirudi nyumbani kwetu,kupunguza kodi moja na kuongeza nguvu kwenye biashara ili ni make at least na mie nijenge mji wangu,maana umri wazidi kimbia.

Naombeni ushauri wenu kama ninalowaza ni sahihi au si sahihi!!
Kosa kubwa sana unataka kulifanya, urudi kwenu na mkeo? hapo kwenu hapana mtu yaani nyumba iko peke yake?

Maana kama kuna wanafamilia wanaishi kwenu rafiki yangu itakuwa bora kodi unazolipa kuliko yatakayozalishwa hapo home kwenu
 
Huenda aina ya kaz/biashara unayofanya haikulipi vizuri huku ukiwa na mzigo wa kulea familia,,,, kuliko kurudi home , bora uhame unapoishi utafute sehemu ya bei poa,,,, kama unaishi nyumba nzima hama, chukua room na sebule tu,,,,ikiwezekana kama bado watoto wadogo chukua single room tu mjibane hivo hivo kwanza !!!

Khs biashara waza nje ya Box panua wigo, ongeza mauzo faida nayo itapanda !! Ni hayo
 
Pole sana kama kijana mwenzangu...

Jamni watoto watoto watoto..
Watoto ni umaskini kama ujaweka foundation nzuri wakuu..

Juzi hapo nimekutana na maza anauliza kama nina mtoto au laah. Najua alikua anauliza kwa utani utani ila mi nikampa jibu ambalo sizani kama ataleta tena habari zake..

Nilimjibu ""unataka mjuu je huyo.mjukuu upo tayari kumlea au.. maana sina maisha hayo ya kuanza kukimbizana na watoto sasa hvi subri niweke mazingira mzuri ya mwanangu ""

Na siku zote hakuna watoto wa bahati mbaya wala mimba za bahati.mbaya kila kitu kinatokea kwa sababu yako weww mwenyewe...

Kwanini nimeongelea watoto.
Kijana mwenztu hapo juu mpaka hali kuwa hvo ni ishu ya familia..
Ukiwaza hivi pia waza hayo mazingira ukishayaweka sawa then ukawa na familia.
Kuna kupanda na kushuka,hali ikibadilika utaikimbia familia??
Kama wakati unaruhusu na yupo mtu sahihi anzisha familia na hautojuta.
 
Mkuu mkuu mkuu sikia niloyoongea kule juu nipo makini nipo conscious nipo understand...

Mkuu mkuu mkuu jua kabisa hiyo kupanda na kushuka haiji kwa kustukiza

Simalizi maneno mengi ila fatilia wengi wanaozingua source ni nini mkuu..

Mkuu kweli ujenge familia alafu uwe unategemea watoto wasomeshwe na ndgu kweli...

Unaanzisha familia ukiwa unawaza kama siku ikitokea upside down kuna ndgu..

Mkuu life hii basi ila mimi sitaki ingia kwa dimbwi la familia bila kua stable. Najua si kwa uwezo wangu ila yote namwachia Mungu mkuu
 
Pole sana kama kijana mwenzangu...

Jamni watoto watoto watoto..
Watoto ni umaskini kama ujaweka foundation nzuri wakuu..

Juzi hapo nimekutana na maza anauliza kama nina mtoto au laah. Najua alikua anauliza kwa utani utani ila mi nikampa jibu ambalo sizani kama ataleta tena habari zake..

Nilimjibu ""unataka mjuu je huyo.mjukuu upo tayari kumlea au.. maana sina maisha hayo ya kuanza kukimbizana na watoto sasa hvi subri niweke mazingira mzuri ya mwanangu ""

Na siku zote hakuna watoto wa bahati mbaya wala mimba za bahati.mbaya kila kitu kinatokea kwa sababu yako weww mwenyewe...

Kwanini nimeongelea watoto.
Kijana mwenztu hapo juu mpaka hali kuwa hvo ni ishu ya familia..
Hili swali hua linanikera sana wnapouliza, unauliza kiumbe ilihali unaona hali ya mtu ilivyo kwamba hajajipanga vizuri bado..
 
Gentleman,
hongera kwa tathimini makini yenye maono na malengo ya mbali sana kwa siku zijazo, ambayo ni very positive kwa mustakabali na ustawi mwema wa familia yako.

Nyumbani ni nyumbani my friends, ladies and gentlemen,

fedheha za nyumbani hazina karaa ukilinganisha na za kwenye nyumba ya kupanga. Fedheha za nyumbani ni nzuri sana ukizigeuza positively na kua fursa ya kukufanya ufanye bidii zaidi katika kutafuta ili hatimae ujenge na kuhamia kwako kwenye amani na utulivu zaidi, lakini pia ukiwa na uhakika hakuna wa kukufukuza kwenu hata muwe mmebanana vipi.

Naunga mkono uamuzi wako wa maana sana, wa kujiformat upya na hatimae kujipanga vizuri na kujizatiti kuyafikia malengo yako walau ukiwa mahali salama

Mkuu mkuu mkuu sikia niloyoongea kule juu nipo makini nipo conscious nipo understand...

Mkuu mkuu mkuu jua kabisa hiyo kupanda na kushuka haiji kwa kustukiza

Simalizi maneno mengi ila fatilia wengi wanaozingua source ni nini mkuu..

Mkuu kweli ujenge familia alafu uwe unategemea watoto wasomeshwe na ndgu kweli...

Unaanzisha familia ukiwa unawaza kama siku ikitokea upside down kuna ndgu..

Mkuu life hii basi ila mimi sitaki ingia kwa dimbwi la familia bila kua stable. Najua si kwa uwezo wangu ila yote namwachia Mungu mkuu
Ikawe kheri ndugu, Mungu ndie mpaji na mpangaji wa yote 🤝
 
Wanawake wana roho mbaya sana, hata wao kwa wao hawapendani.
na hiki ndicho kinachofata. ni ngumu sana mke na mamkwe wakae pamoja na waende sawa. mm na waifu tumepanga mbali na hom sasa kuna wkt waifu akaanza kung'ang'ana akakae na maza. nikawa nampotezea tu maana nawajua wote vizuri wawili. sasa alipokomaa nikamruhusu aende akakae mwezi mmoja. alikaa wiki kadhaa tu akarudi na complaints zilikuwa kibao. icho kipindi chote yupo kule na maza ilikuwa napokea simu za malalamiko kutoka kwa wote wawili. sasa ivi ni zaidi ya miaka 7 sijamsikia tena waifu aongelee mambo ya kwenda kwa mkwewe.
 
Ukijichanganya tu kurudi kwenu, jiandae kuachwa na mkeo.

CHukua hiyo!
 
Umesema umeoa na uko na watoto wawili, sidhani kama hilo wazo la kurudi kwenu litakua zuri sana hasa kama hakuna bond ya kutosha baina ya ndugu zako na huyo mkeo.

Unaweza ukajikuta unaongeza tatizo badala ya kusolve tatizo, na tatizo linaweza kuanzia hapo kwa mkeo na ndugu zako.

Fikiria namna ya kupunguza matumizi yale ambayo yanawezekana kwamfano nyumba, tafuta ambazo ni za bei rahisi zenye kuendana na budget yako.

Usikubali hiyo ndio iwe plan B yako pambana, watoto wa wili mke na hauko vibaya sana why urudi kwenye nyumba ya Mzee wako?
Nakazia ushauri wako mkuu
 
Sio rahis wengi kukuelewa humu. Chukua hatua unayoona kwako ima manufaa. Finances is a game about gains amd losses, ukiona maamuz yako yana egamia kwenye gains zaid na una uhakika na hilo hubahatishi, then fu*ck all other choices and GO for that option. Why funding the fancy life style while all it brings is your financial ruins???

Make sure una plan kamilk, utakaa home kwa muda gani? Na kwa muda huo unataka u achieve nini? Na hakikisha unayafanya hayo kweli, maana hatar ya kutofanya ni kuwa unaweza relax kwakua gharama za maisha zitapungua, hapo utakua huja solve jambo.

Kuna ile concept ya kusema "dont cut expenses ,increase income" but hii ni circumstancial. It does not apply just all the time or just under any circumstance.

Nikutakie kila la kheri.
Mambo sio rahis kama unavyoweza shauriwa. Jua unataka nini.

All the best
Ushauri murwa kbsa
 
Back
Top Bottom