Kurudi nyumbani na kujipanga upya

Kurudi nyumbani na kujipanga upya

Rudi nyumbani ila jipange kwa vita kati ya mkeo na mama yako. Kabla hujahamia bora uongee nao separate kabisa. Wewe unamjua mkeo vizuri na unamjua mama yako vizuri. Ikiwa mabifu anaanzisha mama yako basi mtulize mkeo mwambie asigombane na mama awe mvumilivu kwa kipindi fulani mtahama.
Na ikiwa mkeo ndio mkorofi basi mpange kabisa mama yako kuwa ampuuzie mkwe wake kwa muda kisha mtahama. Na ujitahidi uhasama usi escalate.
Kamwe usije kumdharau mama yako sababu ya mkeo kwa kuwa mkeo lazima atakuwa anakwambia maneno mengi kuhusu mama yako. Na pia kama mama yako akikwambia maneno kuhusu mkeo uwe unayachunguza sio kuamini tu.
Hao watu huwa ni mtihani kuishi nao nyumba moja, ila kwa sababu hakuna jinsi basi wote mvumiliane.

Nakutakia kila la heri na Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi mambo yako
 
Rudi nyumbani ila jipange kwa vita kati ya mkeo na mama yako
na hiki ndicho kinachofata. ni ngumu sana mke na mamkwe wakae pamoja na waende sawa. mm na waifu tumepanga mbali na hom sasa kuna wkt waifu akaanza kung'ang'ana akakae na maza. nikawa nampotezea tu maana nawajua wote vizuri wawili. sasa alipokomaa nikamruhusu aende akakae mwezi mmoja. alikaa wiki kadhaa tu akarudi na complaints zilikuwa kibao. icho kipindi chote yupo kule na maza ilikuwa napokea simu za malalamiko kutoka kwa wote wawili. sasa ivi ni zaidi ya miaka 7 sijamsikia tena waifu aongelee mambo ya kwenda kwa mkwewe.
 
Ukiona umeenda kupanga hlf bado una mawazo ya kurudi kwenu ujue wazi wewe sio mpambanaji na hayo maisha yameshakushinda kwa 100%.

Mm nawakubali sana wachaga. wachaga wakishatoka makwao apo ni 'no way back' hakuna mambo ya kusema utarudi nyumbani. kwanza ukisema unarudi utakuta chumba chako tayari kimepatiwa matumizi mengine nawew hauna nafasi tena apo.

na hii ni kwa watoto wote wa kike na wa kiume. ndomaana mtoto wa kichaga mkizinguana ni bora akuondoe wewe maana anajua majeshi hayanaga kurudi nyuma. Jamii zetu za kibongo zingeiga hii style ya kichaga tungekuwa mbali sana. sio mtu hujipiganii kiswsw unafanya maujinga yako uko ukijua nikivurunda narudisha majeshi home.
 
Habari wana JF.

Mie ni kijana nimeona na nina watoto wawili. Kimaisha sipo vibaya sana nashukuru Mungu. Changamoto kubwa inayonipa hardtime ni Kodi ninazolipa kwa ujumla kuanzia kwenye biashara mpaka nyumba ya kupanga ninayoishi,najiona nimekua na mzigo mkubwa wa kulipa kodi mpaka nashindwa fanya moves nyingine.

Nimewaza kitu ambacho sijui nitafikiriwa vipi na wanaonizunguka ila kwa upande wangu naona itakua ni ahueni!!

Nimewaza kuhama nilipopanga na nirudi nyumbani kwetu,kupunguza kodi moja na kuongeza nguvu kwenye biashara ili ni make at least na mie nijenge mji wangu,maana umri wazidi kimbia.

Naombeni ushauri wenu kama ninalowaza ni sahihi au si sahihi!!
Mke mtumie kama chanzo cha kupunguta ugumu mpe biashara
 
Pole sana lakini USIRUDI NYUMBANI.. katika maisha ukishafika atu ya kujitegemea kuna aibu flani mtu unakua nayo unaweza rudi nyumbani familia ikakutegemea asilimia 90 kutoa mahitaji jambo ambalo litakurudisha nyuma zaidi labda kama kwenu ni wakishuaa kwelii wanaelewa hali yako kuwa unajitafuta otherwise Katafute chumba cha bei rahisii zaidi upunguze kodi unayolipa labda kama nyumbani hakuna familia kabisa, Mahitaji muhimu yanamaliza pesa kuliko kodi.
 
Kimbia familia,upange kachumba ka elfu 20,

Utawatafutaga mambo yakiwa sawa
Familia hana haja ya kuikimbia kama ni mtoto mmoja au wawili alafu wadogoo..! bora airudishe familia nyumbani ila yeye asiende kuishi hapo japo matumizi yatamkaba maana itabdi ajihudumie na ahudumie familia pia.
 
Nyumbani ni yupo mama na mdogo wangu tu.mzee alishatangulia mbele za haki.
Kiukweli bond ya mke na familia yangu si nzuri sana
Ila mpaka nimewaza hivyo nimeumia sana maji naona yapo shingoni.
Ila asante kwa ushauri wako mkuu
Kama bondi ya mama na mke haipo vizurii si uache mke upeleke watoto wako kwa mama mzee huna nyumba huna gari maisha yamekupiga bado unakomaa kuling'ang'ania janamke ambalo halielewani na mamako. Piga chinii peleka watoto kwa mama utachopata unakula na mama soon tu unajenga. Yani kwa maelezoo hayoo ni wazi huyo mwanamke ni mbinafsii na ndio anakurudisha nyuma kimaendeleo. Piga chini kama huna chochote unawaza nini wakati hakuna ata kugawa mali hapo
 
Nyumbani ni yupo mama na mdogo wangu tu.mzee alishatangulia mbele za haki.
Kiukweli bond ya mke na familia yangu si nzuri sana
Ila mpaka nimewaza hivyo nimeumia sana maji naona yapo shingoni.
Ila asante kwa ushauri wako mkuu
Mama mdogo wako..mke wako..watoto na wewe hiyo ni familia tayari so jipime kama utaweza kutoa mahitaji ukwepe kodi au ndo utabadilisha matumizi ya hela tu toka kodi mpaka matumizi plus ugomvi wa mama na mke maana hiyo ni lazimaaa uwepoo tu.
 
Pole sana ila hongera kwa maamuzi hayo magumu.
Kwenye maisha sio mbaya kuamua kujishusha ili kujibalance na kujipanga upya hujafanya kitu kibaya .
Kwenye maisha kuna kupanda na kushuka
Na ni lazima ukubaliane na ukweli ni mbaya sana kufia na tai shingoni.
Piga moyo konde naamini utafanikiwa
 
Gentleman,
hongera kwa tathimini makini yenye maono na malengo ya mbali sana kwa siku zijazo, ambayo ni very positive kwa mustakabali na ustawi mwema wa familia yako.

Nyumbani ni nyumbani my friends, ladies and gentlemen,

fedheha za nyumbani hazina karaa ukilinganisha na za kwenye nyumba ya kupanga. Fedheha za nyumbani ni nzuri sana ukizigeuza positively na kua fursa ya kukufanya ufanye bidii zaidi katika kutafuta ili hatimae ujenge na kuhamia kwako kwenye amani na utulivu zaidi, lakini pia ukiwa na uhakika hakuna wa kukufukuza kwenu hata muwe mmebanana vipi.

Naunga mkono uamuzi wako wa maana sana, wa kujiformat upya na hatimae kujipanga vizuri na kujizatiti kuyafikia malengo yako walau ukiwa mahali salama 🐒

Mawazo kama haya mazuri uwe unayatoa pia kwenye hoja zako za kisiasa.
Kumbe unakuwaga na mawazo mazuri nilikuwa najuwa wewe ni mtu wa hovyo sana kwenye kila nyanja
 
Mawazo kama haya mazuri uwe unayatoa pia kwenye hoja zako za kisiasa.
Kumbe unakuwaga na mawazo mazuri nilikuwa najuwa wewe ni mtu wa hovyo sana kwenye kila nyanja
relax gentleman,
zingatia mawaidha na usonge mbele bila kubaika :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom