jmapunda
JF-Expert Member
- Jul 9, 2015
- 731
- 2,924
Kwa kawaida huwa sipendi kuingia kwenye mtego wa u timu.Siku zote mtu hafundishwi muziki mzuri ni upi kwa sababu kila mtu ana hisia zake juu ya wimbo fulani.Siyo sawa kushindanisha nyimbo zenye ladha na msisimko tofauti.Hapo mtakuwa mnawashindanisha watu!Nimezisikiliza nyimbo zote.Kila moja ina ladha yake.Achana na mambo ya kuangalia kama kuna ujumbe au la...zote zina mdundo mzuri.Mimi ni muumini wa watu wanaoshirikiana kuimba kwa pamoja mtindo ambao unaitwa 'call and responding' kwani unaongeza ladha kwenye wimbo kwa kusikia sauti tofauti tofauti.Tuwe wakweli Diamond ni msanii mwenye kipaji cha kweli....anaweza kuimba na kumiliki jukwaa kwa kucheza.Lakini pia ana uwezo wa kupiga gita kitu ambacho wabongo fleva wengi hawawezi.Wanaosema ana roho mbaya siyo kweli.Kwanza ameunda kundi la WCB,ina maana yuko tayari kufanya kazi na watu wengine na huo ndio mwanzo wa kuwa na live band kitu ambacho ni muhimu kwa muziki wa dunia ya leo.Tusiwahukumu kwa makandokando yao,tuwahukumu kwa muziki wao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app