Lyceum
JF-Expert Member
- Oct 1, 2009
- 1,046
- 568
MADAI YALIOMUUA KOLIMBA CCM JUU YA 'UKWELI ALMASI' WA CHAMA KUKOSA DIRA WALA HAYANA TOFAUTI KUBWA NA YALE YA MWANASAYANSI GALILEO GALILEI KWA VIONGOZI WA DINI DUNIANI
Hata Mwanasayansi Galileo Galilei alipata kukatwa kichwa kwa maagizo ya viongozi wa dini baada ya kuelezea kwamba sura ya dunia ni dwara na kwamba inakwenda inachukua umbo mchongoko mfano wa yai.
Ni majuzi tu baada ya miaka zaidi ya 400 kupita ambapo Marehemu Galileo ametokea kuombwa radhi na viongozi wa dini baada ya kubainika wazi kwamba madai yake ki-uhakika ndio hasa ukweli wa mambo ulivyo.
Kwa nini mtu aje aone ajabu hii CCM Kombokombo ya 'Kamanda' Kikwete kuja kujikamua ujasiri wa kumuomba radhi Horrace Kolimba badala ya kumhonga mwanaye na viji-cheo cha U-DC, wakati Kolimba mwenyewe wala hajamaliza hata robo karne tangu auweke wazi huo 'udhaifu almasi' wa Chama Cha Mapinduzi miaka kadhaa iliopita????
Mkuu napata mashaka kama unaelewa historia ya Galileo vizuri. Galileo hakuuwawa ila alikufa baada ya kupata homa kali na ugonjwa wa moyo. Walichofanya kanisa ni kumtoboa macho kwa kuwa walidhani kuwa jua linaizunguka dunia badala ya dunia kulizunguja jua kama alivyoamini Galileo. Weka kumbukumbu vizuri mkuu. Hata hivo ni kweli ccm wamepoteza dira na hawaujui ukweli.