Mtanzania, ni kweli kutokana na Katiba ya CCM hiyo kanuni ya asilimia 50 ipo.
Ambacho unakosea na hukisemi kwa wazi ni kuwa hiyo kanuni iliwekwa kando kabla ya 2010. Hiyo kanuni iliwekwa kando na Mkapa akiwa Mwenyekiti kabla ya Uchaguzi Mkuu wa CCM wa 2005 uliompitisha Kikwete kuwa mgombea. Kikwete alipowashinda akina Mwandosya na Salim hakupata zaidi ya asilimia 50, na sikumbuki kama uchaguzi ulirudiwa.
Hiyo kanuni haijawahi kutumika tena toka 1995 wakati Mwalimu alipoitumia kama njia ya kumuengua Msuya, ili Kikwete apambane na Mkapa. Si kweli kuwa ilibadilishwa kwa ajili ya 2010 tu.
Kanuni za Chaguzi za CCM zinakinzana na Katiba ya CCM kuhusu ugombeaji, na hii ni mojawapo tu.
Hiyo kanuni haikutumika Igunga wala Uzini.
Msimamizi haundi kanuni wala haamui kanuni ipi atumie na ipi aiteme. Kama ilivyo sawa, msimamizi husimamia kanuni zote zinazoongoza uchaguzi kwa wagombea wote waliopitishwa na chama, kutokana na kanuni zilizopitishwa na Kamati Kuu, KABLA ya Uchaguzi.
Haiwezekani wagombea wote wasiwe sahihi (hakuna mgombea aliyepinga kuhusu Sioi kupitishwa kwa chini ya asilimia 50), msimamizi Arumeru asiwe sahihi, halafu Kamati Ya Siasa ya Wilaya pia isiwe sahihi, halafu Kamati Ya Siasa ya Mkoa isiwe sahihi, na kama muujiza Kamati Kuu pekee ndiyo ione kosa hilo katika kanuni.
Talk about shifting the goalposts AFTER taking the penaly kick.
Ushauri wangu kwa Sioi Sumari ........ ikifika hiyo March 1 JIENGUE na uepukane na karaha na mizengwe ya akina Wassira na Chitanda. (Katika hili JK hana bifu ila anapelekwa tu kama bodaboda.....what's new!!! Kwake nadhani yoyote ni sawa).