Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

May it please you waungwana

Labda CCM wametumia busara kwa maamuzi hayo ya kurudia uchaguzi wa Arumeru Mashariki. Na busara hii ni kwa namna ambavyo kumekuwa na mawazo tofauti pamoja na sintofahamu baina ya pande mbili ndani ya Chama hicho kimoja jambo ambalo si tu litawapa CCM wakati mgumu bali watakuwa na % 40 ya kushinda.

Ni wakati muafaka kwa wanachama wa CCM kutafakari upya juu ya maamuzi yao waliyoyafanya kwa kutazama kati ya Sarakikya na Sioi nani atastahili kupewa zile kura 205 za Elirehema, 176 za Elishilia, 22 za Musani na 11 za Rishiankira lazma mtazame na mfanye uamuzi usio na harufu ya rushwa wala upendeleo wa namna iwayo ile mkikumbuka mlipoangukia na mtakapo inukia.

Mkijiuliza mambo ya msingi mathalan nafahamu Sarakikya alikuwa mgombea mwaka 2010 katika kura za maoni ndani ya Chama na alifanya vizuri lakini pia ama alikuwa au ni kamanda wa vijana ktk Jimbo hilo je Sioi katokea wapi na uwezo wake ni upi???

I aint campaigning but Sarakikya you deserve it! All the best watu wa Meru
 
huu utaratibu wa mshindi lazima apate above 50% umeanza kuwa applied arumeru sio mazee, mbona kwenye kura za maoni 2010 haikutumika wakti kibao walishinda hata bila kufikisha hiyo pasenti? kweli ccm longo nyingi
 
ccm hawajui hesabu wanadhani wagombea wakiwa wawili basi mmoja atapata zaidi ya 50% wakati kiukweli siyo. mathalani kama wapiga kura wapo 1000 halafu katika kura zilizopigwa ikatokea kura 350 (35%) zimeharibika then hakuna mgombea atakayefikisha 50% (endapo angalau kila mgombea anapata zaidi ya 25% ya kura zote).

swali: ccm watatumia kipengele kipi ktk katiba kumpata mshindi?
 
Umeanza kutumika wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga.....Ulikuwepo kbla na ulibadilishwa mwaka 2010 na baadae kurudishwa tena...
 
Sendeka piga tena hiyo layoni Milya kofi ingine ifunge mudomo, ina mudomo sana hii mbalelo(mtoto wa mbusi)
 
mkuu, hii ni siasa, hakuna democrasia kwenye siasa.PERIOD!!!

To prove my point, kwanini the 3rd runner up, somebody Kaaya, kwa nini hakupewa nafasi ya kuwepo kwenye kurudia kura? Katiba haisemi waondolewe.
Thats democracy in politics!
Mkuu sidahani kama hii nayo ni ngumu kuelewa kivile
Kama una wagombea wa tano na kila mmoja akapata asilimia 20 unategemea nini au kurudia mara ngapi uhaguzi ili mtu apate asilimia 51?
Sitaki kuamini kama hujui hili
 
Ni vizuri tukawa wakweli kuwa Viongozi waliokuwa na dhamana ya kusimamia uchaguzi walipitiwa ama waliaamua kuiachia kamati kuu kutoa maamuzi juu ya nani mshindi ama vinginevyo baada ya kubaini ushindani umekuwa mkali kutokana na matokeo.

Hakuna shaka kuwa maamuzi yote yaliyofanyika yamezingatia katiba ya CCM kifungu cha 20 (1) na (2) japo kuna kuchelewa katika maamuzi ambayo yalistahili kufanyika mapema ndani ya Mkutano ule hasa baada ya mshindi kutofikisha zaidi ya nusu ya Kura halali zilizopigwa. Maamuzi ya CC yapo sahihi kulingana na katiba ya Chama.

Katiba ya CCM
20. (1) Mwanachama anayeomba nafasi ya
uongozi wa aina yoyote katika CCM
hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe
amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.(Ilistahili kutumiwa mapema Arumeru)

(2) Katika uchaguzi wa kujaza nafasi nyingi
kwa pamoja, ushindi utahesabiwa kwa kufuata
wingi wa kura alizopata mwombaji wa nafasi
hiyo zaidi ya wenzake, bila kujali kama kura
hizo zinafikia nusu ya kura halali zilizopigwa. (Ilitumiwa katika uchaguzi Mkuu 2010)

Kwa kuzingatia vifungu hivi aidha pasipo kupata malalamiko ama kupokea malalamiko CCM ilikuwa haina njia zaidi ya kuzingatia katiba.

Mkuu Mussa nadhani CCM baada ya kuona kuna manung'uniko toka kwa baadhi ya wagombea hasa matumizi ya rushwa (ambayo hayakuthibitika kwa maana ya ushahidi) ikakumbuka kifungu kilichosahaulika na kuamua kurudia uchaguzi ili kuvunja makundi yaliyoanza kuibuka. Na imani baada ya uchaguzi huu wa pili mshindi atakayepatikana ataweza kupeperusha vyema bendera na kuungwa mkono na wenzie iwapo hakutakuwa na rafu/rushwa ama fitina.
 
Hapa ndipo unapogundua pesa mwanaharamu, imemfanya Sioi aonekane raia wa Tanzania.
 
Mbona hawakurudia Jimbo la Mbarali ambapo Modestus Kilufi aliongoza kwa 1,521 akifuatiwa na Burton Kihaka kura 1,332 huku mbunge anayemaliza muda wake, Esterina Kilasi akiambulia kura 614.Kilufi hakupata 50% ya kura zote!

Hata jimbo la Moshi mjini hakuna aliyapata nusu ya kura zote zilizopigwa;
Ramole amepata kura 1,554, akifuatiwa na Mwenyekiti wa WAZAZI mkoa wa Kilimanjaro, Thomas Ngawaiya (1,539) na Justine Salakana (1,152).

Rungwe Magharibi kwa Prof Mwakyusa na Richard Kasesera kuna mmoja wao aliyepata zaidi ya 50%?CCM jamani one party with multiple standards?

Pia wamekemea kitendo cha kusema Lowasa Katoa hela kwa ajili ya Sioi wakati hela hizo zimetolewa na Fred Lowasa pamoja na rafiki zake.

kwani watu wanakosea kusema hela imetoka kwa Lowasa? Si ni kweli imetoka kwa Fred Lowasa???
 
ccm hawajui hesabu wanadhani wagombea wakiwa wawili basi mmoja atapata zaidi ya 50% wakati kiukweli siyo. mathalani kama wapiga kura wapo 1000 halafu katika kura zilizopigwa ikatokea kura 350 (35%) zimeharibika then hakuna mgombea atakayefikisha 50% (endapo angalau kila mgombea anapata zaidi ya 25% ya kura zote).

swali: ccm watatumia kipengele kipi ktk katiba kumpata mshindi?
Zitatumika asilimia za kura nzima may be
 
huyo jamaa aliyeshinda sijui alitoka wapi....mtu hayupo kwny chama mara eti anashinda...haiwezekani kabisaaa.....!
 
Mkuu hii sio demokrasia kamwe
Mkuu wangu sintokubishia maana kila mtu anatazama kivyake lakini nachoweza kusema na qoutes nilizonazo zinasema hivi:- Democracy is a means for the people to choose their leaders and to hold their leaders accountable for their policies and their conduct in office. The people decide who will represent them in parliament, and who will head the government at the national and local levels. They do so by choosing between competing parties in regular, free and fair elections..

sasa ikiwa wewe unazungumzia HAKI ZA BINADAMU ambapo kuna usawa baina yetu na sote tunapewa nafasi sawa ktk vyombo vya dola hilo jingine. Sii lazima kuweka jina ndio demokrasia wakati at the ned kamati inaweza kuliengua jina hilo hata kabla hujazungumza lolote. \

Hata huko Marekani kwenyewe watu hujitoa kwa sababu hana fedha za kuendelea na uchaguzi sasa kama kweli hii ni demokrasia inakuwaje mtu ashindwe kwa sababu hana mtaji..Litazame unavyotaka muhimu ni kwamba wananchi ndio wanamchagua kiongozi wao na sio kila mtu kupewa nafasi ya kugombea. Kwa uposhaji wa aina hii ndio maana tuna vyama 20 sasa hivi.
 
Mbona hawakurudia Jimbo la Mbarali ambapo Modestus Kilufi aliongoza kwa 1,521 akifuatiwa na Burton Kihaka kura 1,332 huku mbunge anayemaliza muda wake, Esterina Kilasi akiambulia kura 614.Kilufi hakupata 50% ya kura zote!

Hata jimbo la Moshi mjini hakuna aliyapata nusu ya kura zote zilizopigwa;
Ramole amepata kura 1,554, akifuatiwa na Mwenyekiti wa WAZAZI mkoa wa Kilimanjaro, Thomas Ngawaiya (1,539) na Justine Salakana (1,152).

Rungwe Magharibi kwa Prof Mwakyusa na Richard Kasesera kuna mmoja wao aliyepata zaidi ya 50%?CCM jamani one party with multiple standards?

Mkuu majibu ya swali lako yako katika baadhi ya michango ya wanaJF humu.Soma katiba ya CCM kifungu cha 20 (1) na (2).
 
Back
Top Bottom