Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Huyo 'Sioi Mi Msumari' kweli hatoweza 'kuoa' kura katika round ya pili baada ya kuchomachoma na 'msumari'=mshiko, round ya kwanza.
 
Nitarudia kusema haya... CCM wakitaka kushindwa watashindwa lakini wakilitaka jimbo la Arumeru watalichukua na hakuna wa kumzuia....Hizi porojo zetu sisi wote hapa ni matumaini HOPE ambayo inategemea na CCM wanataka nini, lakini bado kabisa wananchi hawana nguvu ya maamuzi...Mtanisamehe ila ndio ukweli unaouma sana.
Kwahiyo Jimbo la Arusha mjini ambako ndio roho ya Arusha hawakulitaka!!?? kama nimekuelewa vizuri.
 
Huitajiki kuwa na Degree ili ufahamu kwamba hili jimbo tayari limekwenda CHADEMA. CCM itaingia kwenye uchaguzi ikiwa vipande vipande, nawashauri viongozi wa CHADEMA kama wanaisoma thread hii wasitangaze mgombea wao mpaka Magamba watangaze mgombea wao, kuna kazungurukee hapa inataka kufanyika.

Matola,
Umesema huitajiki kuwa na degree kufahamu jimbo linakwenda Chadema, halafu hapo hapo unapata wasiwasi unatoa na ushauri kwa Chadema wasimtangaze kwanza mgombea wao, mwisho wa uchaguzi najua utakuja humu Jamvini na kusema tumeibiwa kura tulikuwa tumeshinda.
 
Mi nawasahuri CCM kutokana na hali tete waliyonayo ni vyema wasishiriki huu uchaguzi maana utawamaliza tu!

Waache washiriki maana kama hawatashiriki ushindi kwa CDM hautanogo.Washiriki wagalagazwe wakamwonyeshe mkewao Kafu.NILITABIRI LAZIMA CHAMA FULANI KITACHAFULIWA KWA RUSHWA.SUBIRINI MWONE KABLA YA MACHI MOSI
 
Matola,
Umesema huitajiki kuwa na degree kufahamu jimbo linakwenda Chadema, halafu hapo hapo unapata wasiwasi unatoa na ushauri kwa Chadema wasimtangaze kwanza mgombea wao, mwisho wa uchaguzi najua utakuja humu Jamvini na kusema tumeibiwa kura tulikuwa tumeshinda.
Ukweli una tabia moja kuu, nayo ni kusimama kuwa kweli milele. CCM hapo wanajipa matumaini ya kutumia dola ili kushinda huo uchaguzi na sio kura za wananchi na ndio maana wameshindwa kuheshimu maoni ya kura za wanachama wao, hivi ni lini uliwahi kusikia CCM kura za maoni unahitajika upate over 50%?
 
KATIBA YA CCM
20. (1) Mwanachama anayeomba nafasi ya
uongozi wa aina yoyote katika CCM
hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe
amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.
[/QUOTE
wewe nape tumia ID yako

Mkuu,

Mimi ni Mwakalinga aka Mtanzania na Wakongwe hapa wanajua. Natumia majina yangu kamili wala sihitaji kuficha ID.
 
Siku chache baada ya Wiliam Sarakikya kutaka kuhamia Chadema huku aliekuwa mshindi wa tano (Msani) akihamia chadema chama cha Mapinduzi wamekubaliana na matakwa ya Wiliam Sarakikya kuwa uchauguzi huo urudiwe, kamati kuu ya ccm (CC) kupitia msemaji wake Nape Nauye amesema uchaguzi huo utarudiwa tarehe 1-3-2012, huku akiwataja watakao chuana kuwa ni Wiliam Sarakikya na Sioi Sumari alie tumia zaidi ya mil 100 kwenye uchaguzi uliopita.

Kaka si ulisema huyu jamaa alikuwa anajiandaa kuingia Chadema na ukatuwekea na picha juzi kati akiwa na kamanda Lema?? sasa itakuwaje hapa na anatakiwa apigiwe kura tena na chama chake??
 
Balantanda..that was then this is now, talk on the present issues.

Which is better, kuchangiwa na wapiga kura wako (CDM) au kuwahonga wapiga kura (CCM)?
Hapana......Hapa tunazungumzia utaratibu......Kila chama si kina taratibu mkuu?,achana na suala la past ama present issues...Swala ni je,utaratibu uliotumika kuwapata wagombea Urais na wale wa viti maalum ulikuwa ni sahii?,upo kwenye katiba ya CHADEMA?......

Halafu......Achana na suala Rushwa ndani ya CCM....Nilichotaka mimi unieleze ni kwa nini Nassari anaendesha harambee ya kuchangisa fedha za kumsaidia katika uchaguzi ilhali bado hajapitishwa na chama kama mgombea Ubunge wa CHADEMA?.......Isije suala hili likaja kuleta matatizo mbeleni(endapo Nassari atachaguliwa) na kuleta mgogoro miongoni mwa walioomba kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA....Hili ni angalizo tu
 
Kwahiyo Jimbo la Arusha mjini ambako ndio roho ya Arusha hawakulitaka!!?? kama nimekuelewa vizuri.
Walilitaka sana isipokuwa hapakuwa na jinsi ila naweza sema hivi pengine hata Arumeru walishindwa mwaka 2010 ukizingatia wananchi waliojiandikisha kupiga kura na matokeo ya kura...Na yapo majimbo kibao wameachia na mengine kuzuia ili mradi wawe na nguvu ya rais na bungeni.

Sehemu kibao CCM hawakufanya vizuri lakini majibu yaliyotoka yalikuwa ni ufisadi kwa kwenda mbele na nachojaribu kusema huwezi pambana na Ufisadi kwa kuendelea kutumia mbinu zile zile kupitia sanduku la Kura. Chadema inatakiwa sasa hivi kutumia mbinu tofauti kabisa za kudai haki kwa wananchi wake maana hawashindwi kwa mapenzi ya wananchi.
 
CCM inazidi kujidhihirisha kwa umma kuwa ni chama kinachosimamia demokrasia ktk chaguzi za ndani za chama. Kwakweli hayo ni maamuzi mazuri, changamoto iliyopo ni kuhakikisha uchaguzi wa marudio tar 1/3 vitendo vya rushwa vinadhibitiwa
 
Wana jf baada ya kuthibitisha kua SIOI ni raia wa Tanzania sasa zengwe jingine,uchaguzi kura za maoni kurudiwa tar1.3 na matokeo yatatangazwa tar 03.03,sababu ya kurudia ni hakufikisha 50%,sasa kupambanishwa na SARAKIKYA.
Chanzo:NAPE-WAPO RADIO jioni hii.
 
poa ni kweli kwani umesahau wakati wa mkapa na Kikwete 1995
 
Balantanda..that was then this is now, talk on the present issues.

Which is better, kuchangiwa na wapiga kura wako (CDM) au kuwahonga wapiga kura (CCM)?
Mkuu nakuhakikishia kwenye masuala ya kutafuta wagombe wa nafasi mbali mbali CDM nayo ni moja ya vyama havina kabisa hiyo demokrasia
Sitataja tena mifano(ipo mingi) maana kwako wewe ni sahihi kwasababu ilikuwa "zamani" na wewe unaangalia "sasa" tu
Waacheni jamani wenyewe wamesema wanahitaji upate zaidi ya asilimia 50
 
Hapana......Hapa tunazungumzia utaratibu......Kila chama si kina taratibu mkuu?,achana na suala la past ama present issues...Swala ni je,utaratibu uliotumika kuwapata wagombea Urais na wale wa viti maalum ulikuwa ni sahii?,upo kwenye katiba ya CHADEMA?......

Halafu......Achana na suala Rushwa ndani ya CCM....Nilichotaka mimi unieleze ni kwa nini Nassari anaendesha harambee ya kuchangisa fedha za kumsaidia katika uchaguzi ilhali bado hajapitishwa na chama kama mgombea Ubunge wa CHADEMA?.......Isije suala hili likaja kuleta matatizo mbeleni(endapo Nassari atachaguliwa) na kuleta mgogoro miongoni mwa walioomba kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA....Hili ni angalizo tu
Sawa kabisa una point mkuu, kwani katiba ya Chadema inasema vipi?...Na uchaguzi halali ni upi au unatakiwa uwe vipi?..
 
Hapa tunajadili siasa za pande zote hata wewe umeuliza uteuzi wa Chadema wa urais na viti maalumu so hakuna mwenye ngoswe hapa.
Teh teh.........Lol!.....

Umeliona swali alilouliza Tumaini lakini?.....
 
Muda wote katiba ya CCM inasema hivyo. Kwenye kura za maoni za mwaka 2010 CCM walibadili utaratibu na wakaamua wanachama wote wapige kura. Kwasababu ya ugumu wa ku organise uchaguzi wa wanachama wote mara mbili, wakaweka waraka wa uchaguzi ambao ulikuwa unasema mshindi atapatikana kwa a simple majority.

Kwenye by-elections kama hii ya Arumeru au ile ya Igunga wanatumia utaratibu ule ule wa zamani wa Mkutano mkuu wa CCM wa wilaya kwenye kura za maoni. Kwahiyo kwa maoni yangu mimi nilitegemea hata hicho kifungu cha asilimia 50 kitumike. Nilishangaa kwenye hili la Arumeru wakatumia simple majority.

Nafikiri msimamizi alichemsha na akatumia waraka wa uchaguzi wa 2010 kuendesha kura ya maoni kwa kutumia mkutano mkuu wa CCM wa wilaya. Kitu ambacho kilikuwa makosa.

wanaojua zaidi wamesahihisha na kwa mawazo yangu mimi wako sahihi.

Mtanzania, ni kweli kutokana na Katiba ya CCM hiyo kanuni ya asilimia 50 ipo.

Ambacho unakosea na hukisemi kwa wazi ni kuwa hiyo kanuni iliwekwa kando kabla ya 2010. Hiyo kanuni iliwekwa kando na Mkapa akiwa Mwenyekiti kabla ya Uchaguzi Mkuu wa CCM wa 2005 uliompitisha Kikwete kuwa mgombea. Kikwete alipowashinda akina Mwandosya na Salim hakupata zaidi ya asilimia 50, na sikumbuki kama uchaguzi ulirudiwa.

Hiyo kanuni haijawahi kutumika tena toka 1995 wakati Mwalimu alipoitumia kama njia ya kumuengua Msuya, ili Kikwete apambane na Mkapa. Si kweli kuwa ilibadilishwa kwa ajili ya 2010 tu.

Kanuni za Chaguzi za CCM zinakinzana na Katiba ya CCM kuhusu ugombeaji, na hii ni mojawapo tu.

Hiyo kanuni haikutumika Igunga wala Uzini.

Msimamizi haundi kanuni wala haamui kanuni ipi atumie na ipi aiteme. Kama ilivyo sawa, msimamizi husimamia kanuni zote zinazoongoza uchaguzi kwa wagombea wote waliopitishwa na chama, kutokana na kanuni zilizopitishwa na Kamati Kuu, KABLA ya Uchaguzi.

Haiwezekani wagombea wote wasiwe sahihi (hakuna mgombea aliyepinga kuhusu Sioi kupitishwa kwa chini ya asilimia 50), msimamizi Arumeru asiwe sahihi, halafu Kamati Ya Siasa ya Wilaya pia isiwe sahihi, halafu Kamati Ya Siasa ya Mkoa isiwe sahihi, na kama muujiza Kamati Kuu pekee ndiyo ione kosa hilo katika kanuni.

Talk about shifting the goalposts AFTER taking the penaly kick.

Ushauri wangu kwa Sioi Sumari ........ ikifika hiyo March 1 JIENGUE na uepukane na karaha na mizengwe ya akina Wassira na Chitanda. (Katika hili JK hana bifu ila anapelekwa tu kama bodaboda.....what's new!!! Kwake nadhani yoyote ni sawa).
 
Wakuu,

Hapa huyu mheshimiwa Mwigulu amechemsha sana. Ni aibu kwa chama kikongwe kama CCM wanashindwa kuielewa na kuifuata katiba yao.

Kama ni kweli kwamba Nape alitetea kwenye TV kwamba sio lazima kufikisha asilimia hamsini, naye hapo anachemsha. Imekuwaje chama kikongwe hivyo kikafika mahali ambapo viongozi wake wakuu wanashindwa hata kuielewa katiba yao?

Najua ile kura ya maoni ya mwaka 2010 imewachanganya lakini ni kosa kubwa watu wote hao kuchanganyikiwa na kushindwa kuuona ukweli mpaka CC ndio inakuja kuwaambia kwamba mmekosea?

Sasa kama secretariat ya CCM hawaijui katiba yao, vipi wale wenzetu kule wilayani? Vyama vimeingiza Wababaishaji ambao wanafikiri wanaweza kufanya mambo bila kusoma na matokeo yake ndio hayo.

Mambo mengine yanasikitisha sana!
 
Back
Top Bottom