Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Sidhani kama njia waliyotumia ni nzuri kunusuru naona kama wanaongeza makovu zaidi.
Then why manazi wa CDM wanatokwa povu, Hawaoni kama ni advantage kwao?
Kama CDM walitumia wazee kubinya demokrasia kwa Zito CCm wao wameona gia hii ndio inawafaa waachwe, kwangu mimi kulia na kucheka yote ni makelele tu
 
ama matokeo ya kura za maoni tena wapiga kura ni wa chama kimoja na hawazidi elfu kumi zinahesabiwa kwa siku tatu then ni bora kuacha haya mambo ya chaguzi

I am sure Sioi na Bill si wakiritimba hivi sema wako associated na watu weny akili fupi kama mimi ndio wanaoharibu siasa za CCM
 
Hakuna mahala kanuni za CCM inasema mgombea ubunge lazima apate asilimia 50 isipokuwa nafasi ya rais tu..
Kanuni za wagombea wa CCM ngazi ya Uwakilishi/Ubunge inasema hivi:-
(iv)​
Ngazi ya Baraza la Wawakilishi/Bunge:
(1)​
Wagombea watapigiwa kura za maoni na Mkutano Mkuu wa CCM wa kilaJimbo la Uchaguzi linalohusika,(2) Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya itawajadili wagombea.(3) Kwa upande wa Tanzania Bara, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCMya Mkoa itawajadili wagombea na kuwatolea mapendekezo yake kwa KamatiKuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa. Kwa upande wa Tanzania Zanzibar, Kamatiya Siasa ya Mkoa itawajadili wagombea na kuwatolea mapendekezo yake kwaKamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ambayo nayo itatoamapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.(4) Kamati Kuu itawajadili wagombea wote na kutoa mapendekezo yake kwaHalmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kwa ajili ya uteuzi wa mwisho.Katika kufanya kazi hiyo kwa upande wa Wabunge/Wawakilishi wanaomalizamuda wao, Kamati Kuu itazingatia pia tathmini itakayokuwa imefanyika ya
utendaji kazi wao katika kipindi kinachomalizika..

Mkuu Mkandara,

Mbona section 20 inasema wazi juu ya hilo? Ni kama hapa chini. Ni mwaka 2010 tu waliweka utaratibu kwenye waraka wa uchaguzi. Vinginevyo utaratibu unaotumika ni kama ilivyo kwenye katiba. Angalia katiba ya 2010, usije ukawa unaangalia matoleo ya nyuma.

20. (1) Mwanachama anayeomba nafasi ya
uongozi wa aina yoyote katika CCM
hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe
amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.

(2) Katika uchaguzi wa kujaza nafasi nyingi

kwa pamoja, ushindi utahesabiwa kwa kufuata
wingi wa kura alizopata mwombaji wa nafasi
hiyo zaidi ya wenzake, bila kujali kama kura
hizo zinafikia nusu ya kura halali zilizopigwa.

Mara zote mgombea anayechaguliwa na Mkutano Mkuu wa Wilaya jina lake hupelekwa kwenye ngazi ya mkoa kujadiliwa na baadae hupelekwa CC kwa ajili ya kujadiliwa...CC ndiyo hupitisha na kutangaza majina ya wagombea wa CCM katika chaguzi zote.....

right there!!
....and ccm's cc can do whatever they wish. Kama walivyofanya kwa Kigwangala
 
huyo Milya bado ni kijana mwambieni aache kuwa vuvuzela la wazee uchwara, hata wakijashika madaraka atabaki kuwa vuvuzela
 
Sawa tuzungumzie Demokrasia.. Hivi demokrasia inaaza pale mtu anapopewa nafasi ya kugombea au demokrasia ni pale watu wanapopewa nafasi ya kumchagua kiongozi wamtakaye... Sioni tafsiri halisi haswa ni ipi. Kama Chadema wameamua badala ya kila mtu achukue form halafu baraza linawachambua kulingana na vigezo vyao kwa nini isiwe rahisi kuwapa nafasi hiyo baraza hilo lije na majina ambayo wao tayari wanayaona yana sifa hizo kuliko mimi hapa Mkandara nichukue form kwa fikra kwamba nataka niwe rais (ambition) kumbe uwezo huo sina ila nije umbuliwa ktk vikao vya chama!. Ni vizuri sana kupendekezwa kuliko kujipendekeza hasa ktk nafasi hii ya Urais (a Leader).

Cjhadema hamkatazi mtu kugombea Urais isipokuwa msingi wa kumpata kiongozi wenu ni wa wanachi wenyewe wakijua tunamtaka kiongozi wa aina gani maana hii sio Jeshi au kutafuta mwenye CV baabu kubwa. Hivyo ipo sababu ya kuwapa mabaraza haya mawili kumchagua kiongozi wao ambaye atawawakilisha wote, japokuwa kama kuna Upinzani unapewa ruksa kuweka Upinzani.

Kama Chadema wangefuata mfumo wa Marekani au Ulaya basi tusingempata mtu kama Dr. Slaa maana hakutaka kugombea wala hakujua hazina alokuwa nayoi isipokuwa sisi wanachama. Na hii ndio sifa kubwa ya chama hiki kuwapa nafasi wananchi wenyewe kupitia wajumbe wao wamchague kiongozi anayewafaa. Badala ya kuletewa majina nyie wananchi ndio mnatoa jina au majina.
Kiukweli Mkuu wangu huu utaratibu unaotumiwa na CHADEMA si mbaya......Tatizo ni kwamba unaweza kuja kuleta matatizo mbeleni endapo kuna wanachama watapenda kujitokeza kugombea ilhali chama kina mtu ambaye kinamuona anafaa kuwa Rais.....Mfano mzuri ni ule mchakato wa kumpata Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA,chama pamoja na wazee ndani ya chama walimuona F.A. Mbowe anafaa kuwa Mwenyekiti wa chama wa Taifa(na kwa hakika hawakukosea) na Zitto Kabwe alijitokeza kugombea nafasi hiyo lakini wazee walimshuri ajitoe.....Hali hii ilizusha mkanganyiko ndani ya chama kiasi cha kutishia kuwepo kwa mgogoro ambao hata hivyo ulizimwa....Hivyo kuna hatari mbeleni wakajitokeza watu wa aina ya Zitto na kutaka kugombea Urais lakini kwa taratibu za chama wanashindwa maana chama kinakuwa na jina la mtu ambaye kimemuona atafaa kuwa Rais.....
 
Mara zote mgombea anayechaguliwa na Mkutano Mkuu wa Wilaya jina lake hupelekwa kwenye ngazi ya mkoa kujadiliwa na baadae hupelekwa CC kwa ajili ya kujadiliwa...CC ndiyo hupitisha na kutangaza majina ya wagombea wa CCM katika chaguzi zote.....

Mimi sijakataa kwenye hilo na wala sina haki ya kupinga hata kidogo. Hivi uamuzi wa kurudisha majina mawili ya mshindi wa kwanza na pili si yametolewa na CC? tena baada ya kura za maoni za mwanzo ambayo matokeo yake yaliisha jadiliwa na vikao vyote ulivyovieleza mpaka kuifikia hiyo CC?, Ina maana kuwa wameyajadili haya majina na kuona kuwa wote wanawakilisha matakwa yao (hao Political tycoons wa CC). Ina maana uchaguzi wa 2010 walifanya mchakato kama huu?. Kwa nini sasa kamati kuu ya Taifa isiuachie mkutano mkuu wa wilaya kuwa na maamuzi ya mwisho?. All Politics are local kwa nini watu wa Dar wanataka kuwaamulia watu wa Arumeru?. Au hii ni POWER GRAB of showing the ALMIGHTY CC is CCM?
 
Mkuu Mkandara,

Mbona section 20 inasema wazi juu ya hilo? Ni kama hapa chini. Ni mwaka 2010 tu waliweka utaratibu kwenye waraka wa uchaguzi. Vinginevyo utaratibu unaotumika ni kama ilivyo kwenye katiba.

20. (1) Mwanachama anayeomba nafasi ya
uongozi wa aina yoyote katika CCM
hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe
amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.

(2) Katika uchaguzi wa kujaza nafasi nyingi

kwa pamoja, ushindi utahesabiwa kwa kufuata
wingi wa kura alizopata mwombaji wa nafasi
hiyo zaidi ya wenzake, bila kujali kama kura
hizo zinafikia nusu ya kura halali zilizopigwa.

Kwa hiyo kanuni hii imeongezwa mwaka 2010 au? maana nayoiona mimi ni ile ya mwaka 2005.. ebu nipe link.
 
Mara zote mgombea anayechaguliwa na Mkutano Mkuu wa Wilaya jina lake hupelekwa kwenye ngazi ya mkoa kujadiliwa na baadae hupelekwa CC kwa ajili ya kujadiliwa...CC ndiyo hupitisha na kutangaza majina ya wagombea wa CCM katika chaguzi zote.....
Hiyo mara zote ndiyo anayoipinga Hofstede, kuwa kama kamati kuu imesharidhika na majina mawili na imeyarudisha chini hakuna haja tena kwa CC kuja kukaa na kuanza kujadili jina au majina yale yale, ndipo Hofstede akadhani ni vizuri sasa mkutano mkuu wa wilaya ukakasimiwa madaraka ya mwisho.
 
Then why manazi wa CDM wanatokwa povu, Hawaoni kama ni advantage kwao?
Kama CDM walitumia wazee kubinya demokrasia kwa Zito CCm wao wameona gia hii ndio inawafaa waachwe, kwangu mimi kulia na kucheka yote ni makelele tu

mkuu, hii ni siasa, hakuna democrasia kwenye siasa.PERIOD!!!

To prove my point, kwanini the 3rd runner up, somebody Kaaya, kwa nini hakupewa nafasi ya kuwepo kwenye kurudia kura? Katiba haisemi waondolewe.
Thats democracy in politics!
 
Ni vizuri tukawa wakweli kuwa Viongozi waliokuwa na dhamana ya kusimamia uchaguzi walipitiwa ama waliaamua kuiachia kamati kuu kutoa maamuzi juu ya nani mshindi ama vinginevyo baada ya kubaini ushindani umekuwa mkali kutokana na matokeo.

Hakuna shaka kuwa maamuzi yote yaliyofanyika yamezingatia katiba ya CCM kifungu cha 20 (1) na (2) japo kuna kuchelewa katika maamuzi ambayo yalistahili kufanyika mapema ndani ya Mkutano ule hasa baada ya mshindi kutofikisha zaidi ya nusu ya Kura halali zilizopigwa. Maamuzi ya CC yapo sahihi kulingana na katiba ya Chama.

Katiba ya CCM
20. (1) Mwanachama anayeomba nafasi ya
uongozi wa aina yoyote katika CCM
hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe
amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.(Ilistahili kutumiwa mapema Arumeru)

(2) Katika uchaguzi wa kujaza nafasi nyingi
kwa pamoja, ushindi utahesabiwa kwa kufuata
wingi wa kura alizopata mwombaji wa nafasi
hiyo zaidi ya wenzake, bila kujali kama kura
hizo zinafikia nusu ya kura halali zilizopigwa. (Ilitumiwa katika uchaguzi Mkuu 2010)

Kwa kuzingatia vifungu hivi aidha pasipo kupata malalamiko ama kupokea malalamiko CCM ilikuwa haina njia zaidi ya kuzingatia katiba.
 
Kiukweli Mkuu wangu huu utaratibu unaotumiwa na CHADEMA si mbaya......Tatizo ni kwamba unaweza kuja kuleta matatizo mbeleni endapo kuna wanachama watapenda kujitokeza kugombea ilhali chama kina mtu ambaye kinamuona anafaa kuwa Rais.....Mfano mzuri ni ule mchakato wa kumpata Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA,chama pamoja na wazee ndani ya chama walimuona F.A. Mbowe anafaa kuwa Mwenyekiti wa chama wa Taifa(na kwa hakika hawakukosea) na Zitto Kabwe alijitokeza kugombea nafasi hiyo lakini wazee walimshuri ajitoe.....Hali hii ilizusha mkanganyiko ndani ya chama kiasi cha kutishia kuwepo kwa mgogoro ambao hata hivyo ulizimwa....Hivyo kuna hatari mbeleni wakajitokeza watu wa aina ya Zitto na kutaka kugombea Urais lakini kwa taratibu za chama wanashindwa maana chama kinakuwa na jina la mtu ambaye kimemuona atafaa kuwa Rais.....
Wala hauna ubaya isipokuwa kuna tofauti kubwa ktk kugombea nafasi ya Uongozi ngazi za chama na zile za Kitaifa. Tatizo la Zitto na Mbowe binafsi yangu naamini kabisa kwamba ulisukwa na watu kuweka Uadui baina na Zitto na Mbowe na kwa bahati mbaya wote hawa wakaingia mkenge. Mbowe akifikiria Zitto ametumwa na Zitto akijua kwamba Mbowe anataka kukifanya chama ni cha ukoo akitumiwa pia na CCM.

Mimi najua sana yanayotokea mjini na ingawa wengi hawawezi kuelewa lakini mchezo mchafu ulichezwa na watu ndani ya Chadema kuweka ufa baina ya Mbowe na Zitto maana Zitto alikuwa anakuja kwa kasi ambayo watu wengine iliwakwaza hasa ktk kugombea vyeo ndani ya chama. Haya ni mambo ya kawaida kabisa ktk demokrasia tena afadhali yetu sisi maana huko Marekani huletwa hadi unayoyafanya na mkeo kuwa hojaya mgombea.. Tutafika tu taratibu.
 
Mimi sijakataa kwenye hilo na wala sina haki ya kupinga hata kidogo. Hivi uamuzi wa kurudisha majina mawili ya mshindi wa kwanza na pili si yametolewa na CC? tena baada ya kura za maoni za mwanzo ambayo matokeo yake yaliisha jadiliwa na vikao vyote ulivyovieleza mpaka kuifikia hiyo CC?, Ina maana kuwa wameyajadili haya majina na kuona kuwa wote wanawakilisha matakwa yao (hao Political tycoons wa CC). Ina maana uchaguzi wa 2010 walifanya mchakato kama huu?. Kwa nini sasa kamati kuu ya Taifa isiuachie mkutano mkuu wa wilaya kuwa na maamuzi ya mwisho?. All Politics are local kwa nini watu wa Dar wanataka kuwaamulia watu wa Arumeru?. Au hii ni POWER GRAB of showing the ALMIGHTY CC is CCM?

your last sentence is correct. Thats how it is.
Kumbuka, haya majina mawili yaliyopitishwa na cc, yatakuja kujadiliwa tena, na kama aliyepata more than 50per ni mtu wasiyemtaka, zengwe la mambo ya nidhamu na utendaji yataibuliwa, na cc inaweza kimpitisha aliyepata 30per.
Thats is democracy in politics, hasa ya ccm.
 
Sawa tuzungumzie Demokrasia.. Hivi demokrasia inaaza pale mtu anapopewa nafasi ya kugombea au demokrasia ni pale watu wanapopewa nafasi ya kumchagua kiongozi wamtakaye... Sioni tafsiri halisi haswa ni ipi. Kama Chadema wameamua badala ya kila mtu achukue form halafu baraza linawachambua kulingana na vigezo vyao kwa nini isiwe rahisi kuwapa nafasi hiyo baraza hilo lije na majina ambayo wao tayari wanayaona yana sifa hizo kuliko mimi hapa Mkandara nichukue form kwa fikra kwamba nataka niwe rais (ambition) kumbe uwezo huo sina ila nije umbuliwa ktk vikao vya chama!. Ni vizuri sana kupendekezwa kuliko kujipendekeza hasa ktk nafasi hii ya Urais (a Leader).

Chadema haimkatazi mtu kugombea Urais isipokuwa msingi wa kumpata kiongozi wenu ni wa wanachi wenyewe wakijua tunamtaka kiongozi wa aina gani anayetufaa maana hili sio Jeshi, Polisi au shirika kutafuta mwenye CV baabu kubwa. Hivyo ipo sababu ya kuwapa mabaraza haya mawili kumchagua kiongozi wao ambaye atawawakilisha wote, japokuwa kama kuna Upinzani unapewa ruksa kuweka Upinzani.

Kama Chadema wangefuata mfumo wa Marekani au Ulaya basi tusingempata mtu kama Dr. Slaa maana hakutaka kugombea wala hakujua hazina alokuwa nayoi isipokuwa sisi wanachama. Na hii ndio sifa kubwa ya chama hiki kuwapa nafasi wananchi wenyewe kupitia wajumbe wao wamchague kiongozi anayewafaa.
Mkuu hii sio demokrasia kamwe
 
Kwa hiyo kanuni hii imeongezwa mwaka 2010 au? maana nayoiona mimi ni ile ya mwaka 2005.. ebu nipe link.

Mkuu Mkandara, Katiba hubadilika kulingana na mabadiliko ya kimtazamo,kiuchumi,kijamii na pengine teknolojia.Hivyo inawezekana 2005 ilikuwa chachu ya mabadiliko ya sheria hii kulingana na udhaifu ulioonekana. Nadhani kwa kuwa sheria hii ipo ama ilitangulia kuwepo hakuna shaka juu ya kutumika kwake.
 
Mimi sijakataa kwenye hilo na wala sina haki ya kupinga hata kidogo. Hivi uamuzi wa kurudisha majina mawili ya mshindi wa kwanza na pili si yametolewa na CC? tena baada ya kura za maoni za mwanzo ambayo matokeo yake yaliisha jadiliwa na vikao vyote ulivyovieleza mpaka kuifikia hiyo CC?, Ina maana kuwa wameyajadili haya majina na kuona kuwa wote wanawakilisha matakwa yao (hao Political tycoons wa CC). Ina maana uchaguzi wa 2010 walifanya mchakato kama huu?. Kwa nini sasa kamati kuu ya Taifa isiuachie mkutano mkuu wa wilaya kuwa na maamuzi ya mwisho?. All Politics are local kwa nini watu wa Dar wanataka kuwaamulia watu wa Arumeru?. Au hii ni POWER GRAB of showing the ALMIGHTY CC is CCM?
Uchaguzi wa mwaka 2010 haukufuata mchakato huu......Utaratibu ulibadilishwa lakini baada ya uchaguzi utaratibu ulirudishwa na kwa kuanzia ulitumika katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga......Kwa utaratibu wa CCMKamati kuu ndiyo yenye maamuzi ya mwisho ya nani akiwakilishe chama katika uchaguzi husika....Na huu ni utaratibu ambao kimsingi una mapungufu mengi,kuna haja ya wanaCCM wa eneo husika wakaachiwa mamlaka ya kuchagua ni nani awawakilishe katika uchaguzi husika(sitegemei kuona vyama vingine vinatumia utaratibu kama huu wa CCM).....Kimsingi yote haya yanafanyika kutokana na makundi/mpasuko mkubwa uliopo ndani ya CCM ambapo mgawanyiko wa kimakundi ndani ya chama unapelekea makundi husika kupambana na kila kundi kutaka kumuweka mgombea linayemtaka yeye....

Utaratibu umetumika kwa mujibu wa Ibara ya 20(Kifungu cha 1 cha 2 na cha 3 cha Katiba ya CCM)

20. (1) Mwanachama anayeomba nafasi ya
uongozi wa aina yoyote katika CCM
hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe
amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.

(2) Katika uchaguzi wa kujaza nafasi nyingi
kwa pamoja, ushindi utahesabiwa kwa kufuata
wingi wa kura alizopata mwombaji wa nafasi
hiyo zaidi ya wenzake, bila kujali kama kura
hizo zinafikia nusu ya kura halali zilizopigwa.

(3) Kanuni za Uchaguzi wa CCM zitaweka
vifungu mahsusi, vitakavyowezesha uwakilishi
wa Wanawake katika vikao vya CCM hatimaye
kuwa si chini ya asilimia 50 ya wajumbe wote
wanaochaguliwa kujaza nafasi za makundi,
kwa kila ngazi ya uongozi wa Chama.
 
Ujinga tu wanapima nguvu ya maji, wameru wasingeongea ccm wangeipotezea kwangu mimi ni mchezo sawa na nyongeza ya marupurupu ya wabunge baada ya kelele mkuu akachomoa
 
Back
Top Bottom