Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Mkuu mkandara,
Kibaya zaidi wagombea wenzake wamelalamika mwenzao kafanyiwa harambee na viongozi wa chama hakiwemo Lema, wamekusanya Sh10 milioni pamoja na magari manane kwa ajili ya kampeni za ubunge.

Mshikaji wangu unavyompenda LEMA! Yani siku haipiti hujataja jina lake kwenye thread yako! LEMA muoe huyu Dada!

 
katiba ya CCM toleo la 2010 ni hili hapa.

http://www.cms.ccmtz.org/doc/KATIBA.pdf
Mbona hii imekaa kama uchaguzi wa viongozi ndani ya Chama na sio Uwakilishi/Bunge ambayo inapatikana ktk kanuni za chama. Ikiwa ndivyo, inakuwaje CCM watunzi wa hizi sheria inapofikia kugombea Ubunge kitaifa swala la asilimia 50 linakufa? wakati mnajua umuhimu wa asilimia 50 ambazo mnazitumia ndani ya chama?
 
Uchaguzi wa mwaka 2010 haukufuata mchakato huu......Utaratibu ulibadilishwa lakini baada ya uchaguzi utaratibu ulirudishwa na kwa kuanzia ulitumika katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga......Kwa utaratibu wa CCMKamati kuu ndiyo yenye maamuzi ya mwisho ya nani akiwakilishe chama katika uchaguzi husika....Na huu ni utaratibu ambao kimsingi una mapungufu mengi,kuna haja ya wanaCCM wa eneo husika wakaachiwa mamlaka ya kuchagua ni nani awawakilishe katika uchaguzi husika(sitegemei kuona vyama vingine vinatumia utaratibu kama huu wa CCM).....Kimsingi yote haya yanafanyika kutokana na makundi/mpasuko mkubwa uliopo ndani ya CCM ambapo mgawanyiko wa kimakundi ndani ya chama unapelekea makundi husika kupambana na kila kundi kutaka kumuweka mgombea linayemtaka yeye....

Utaratibu umetumika kwa mujibu wa Ibara ya 20(Kifungu cha 1 cha 2 na cha 3 cha Katiba ya CCM)

20. (1) Mwanachama anayeomba nafasi ya
uongozi wa aina yoyote katika CCM
hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe
amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.


(2) Katika uchaguzi wa kujaza nafasi nyingi
kwa pamoja, ushindi utahesabiwa kwa kufuata
wingi wa kura alizopata mwombaji wa nafasi
hiyo zaidi ya wenzake, bila kujali kama kura
hizo zinafikia nusu ya kura halali zilizopigwa.


(3) Kanuni za Uchaguzi wa CCM zitaweka
vifungu mahsusi, vitakavyowezesha uwakilishi
wa Wanawake katika vikao vya CCM hatimaye
kuwa si chini ya asilimia 50 ya wajumbe wote
wanaochaguliwa kujaza nafasi za makundi,
kwa kila ngazi ya uongozi wa Chama.

Sasa kama Kamati kuu ndiyo ina maamuzi ya mwisho ya nani awe mgombea kwa nini wanarudisha majina mawili wilayani ili kwenda kupotezea watu muda kama wao ndiyo waamuzi ya mwsho?
 
Mbona hii imekaa kama uchaguzi wa viongozi ndani ya Chama na sio Uwakilishi/Bunge ambayo inapatikana ktk kanuni za chama. Ikiwa ndivyo, inakuwaje nyie CCm ndio watunzi wa hizi sheria inapofikia Ubunge kitaifa swala la asilimia 50 linakufa? wkaati mnajua umuhimu wa asilimia 50 ambazo mnazitumia ndani ya chama?
Bob......

Hiyo ni kwa Viongozi wote(wakiwemo viongozi wa ndani ya chama pamoja na wale wanaoshirki katika kura za maoni za kuomba kuteuliwa kuwakilisha chama katika uchaguzi wa ngazi ya serikali za mitaa,udiwani, Uwakilishi, ubunge, Uspika, Umeya na Urais wa Muungano na ule wa SMZ)....Jaribu kupitia kitabu hiki cha kanuni na taratibu za Uteuzzi ndani ya CCM...

http://www.cms.ccmtz.org/doc/kuteuzi.pdf
 
CCM hawana mfalme Suleiman! Wamefanya hivyo kumkomoa Lowassa tu!

Mkuu Mnyisansu heshma kwako;

Hili siwezi kulipinga moja kwa moja ila kwa hali ilivyo heshma ya Edward itabaki chanya tu kama atampigia Kampeni Sarakikya and not Sioi na sababu tunazo na haya ndiyo yanayoenda kutokea muda si mrefu........
 
Amina.....

Cha msingi ni kuomba tu hayo yasitokee kwenye uchaguzi mkuu wa viongozi wa CHADEMA na ule mchakato wa kumpata mgombea Urais wa mwaka 2015......

Balantanda;

Likely kama mtu wa CC angeshinda CCM ingefunika kombe na angetangazwa hivyo hivyo;nina uhakika Sioi Sumari siyo mtu wao na huenda kuwa MKWE wa LOWASSA kumemponza kijana huyu!William Sarakikya ana nafasi kubwa sasa maana wale wote walioenguliwa watawaeleza wapambe wao wampe kura!

Pole Sioi!
 
May it please you waungwana

Labda CCM wametumia busara kwa maamuzi hayo ya kurudia uchaguzi wa Arumeru Mashariki. Na busara hii ni kwa namna ambavyo kumekuwa na mawazo tofauti pamoja na sintofahamu baina ya pande mbili ndani ya Chama hicho kimoja jambo ambalo si tu litawapa CCM wakati mgumu bali watakuwa na % 40 ya kushinda.

Ni wakati muafaka kwa wanachama wa CCM kutafakari upya juu ya maamuzi yao waliyoyafanya kwa kutazama kati ya Sarakikya na Sioi nani atastahili kupewa zile kura 205 za Elirehema, 176 za Elishilia, 22 za Musani na 11 za Rishiankira lazma mtazame na mfanye uamuzi usio na harufu ya rushwa wala upendeleo wa namna iwayo ile mkikumbuka mlipoangukia na mtakapo inukia.

Mkijiuliza mambo ya msingi mathalan nafahamu Sarakikya alikuwa mgombea mwaka 2010 katika kura za maoni ndani ya Chama na alifanya vizuri lakini pia ama alikuwa au ni kamanda wa vijana ktk Jimbo hilo je Sioi katokea wapi na uwezo wake ni upi???

I aint campaigning but Sarakikya you deserve it! All the best watu wa Meru

Mkuu uko sahihi katika maoni yako lakini huoni kama mwishoni umeonekana kugusia wasifu wa mmoja na kumuacha mwingine hivyo kuwaacha wapiga kura katika muono wa upande mmoja. Nadhani tuwape nafasi wanaCCM wa Arumeru kumchagua wanae amini kuwa atawawakilisha vyema katika ushindani wa vyama.
 
Bob......

Hiyo ni kwa Viongozi wote(wakiwemo viongozi wa ndani ya chama pamoja na wale wanaoshirki katika kura za maoni za kuomba kuteuliwa kuwakilisha chama katika uchaguzi wa ngazi ya serikali za mitaa,udiwani, Uwakilishi, ubunge, Uspika, Umeya na Urais wa Muungano na ule wa SMZ)....Jaribu kupitia kitabu hiki cha kanuni na taratibu za Uteuzzi ndani ya CCM...

http://www.cms.ccmtz.org/doc/kuteuzi.pdf
Naam hii haina tofauti na ile niliyoiweka mimi ila natafuta mahala panaposema mgombea Uwakilishi/Bunge anatakiwa kupata silimia 50 ya kura - wewe umepaona?
 
Balantanda;

Likely kama mtu wa CC angeshinda CCM ingefunika kombe na angetangazwa hivyo hivyo;nina uhakika Sioi Sumari siyo mtu wao na huenda kuwa MKWE wa LOWASSA kumemponza kijana huyu!William Sarakikya ana nafasi kubwa sasa maana wale wote walioenguliwa watawaeleza wapambe wao wampe kura!

Pole Sioi!
Hivi kuna anayejua historia ya kisiasa ya Sioi?......

Ni upi ushiriki wake katika siasa(zaidi ya kuwa mwanachama) za ndani za CCM?....Kuna anyejua atujuze?
 
Mkuu wangu sintokubishia maana kila mtu anatazama kivyake lakini nachoweza kusema na qoutes nilizonazo zinasema hivi:- Democracy is a means for the people to choose their leaders and to hold their leaders accountable for their policies and their conduct in office. The people decide who will represent them in parliament, and who will head the government at the national and local levels. They do so by choosing between competing parties in regular, free and fair elections..


sasa ikiwa wewe unazungumzia HAKI ZA BINADAMU ambapo kuna usawa baina yetu na sote tunapewa nafasi sawa ktk vyombo vya dola hilo jingine. Sii lazima kuweka jina ndio demokrasia wakati at the ned kamati inaweza kuliengua jina hilo hata kabla hujazungumza lolote. \

Hata huko Marekani kwenyewe watu hujitoa kwa sababu hana fedha za kuendelea na uchaguzi sasa kama kweli hii ni demokrasia inakuwaje mtu ashindwe kwa sababu hana mtaji..Litazame unavyotaka muhimu ni kwamba wananchi ndio wanamchagua kiongozi wao na sio kila mtu kupewa nafasi ya kugombea. Kwa uposhaji wa aina hii ndio maana tuna vyama 20 sasa hivi.
Mkuu hii dhana ya demokrasia kweli ni pana na kwasababu hapa tunajadili ya CCM na asilimia hamsini basi tuyaache
Isipokuwa msingi wa demokrasia unaanzia kwenye haki ya kuchagua na kuchaguliwa
 
Haaa haa haaa haa CCM,

Sasa yupi kati yao wa kuhongwa na cheo cha U-Kuu wa Wilya au Ubalozioni hapo juu. CHADEMA mwendo mchaka mchaka, ulimi njee kwa hao MAAFISADI.

Kura tukazilinde ipasavyo na daftari la wapiga kura Arumeru tuk-iundie Taskforce ya kulipitia nukta kwa nukta maana hiyo ni jukumu la chama kikiwa ni Mdau namba moja kwenye uchaguzi wowote hivyo hatupaswi kumuachia Tendwa peke yake mana haaminiki tena kwa kuwa ni Refarii/Mchezaji katika siasa siku hizi.
 
Mkuu hii dhana ya demokrasia kweli ni pana na kwasababu hapa tunajadili ya CCM na asilimia hamsini basi tuyaache
Isipokuwa msingi wa demokrasia unaanzia kwenye haki ya kuchagua na kuchaguliwa
Bila shaka haki ya KUCHAGUA haiwezi kuwa haki ya kugombea bali unachagua chama au mtu unayemtaka, na Haki ya KUCHAGULIWA inatokana na wachaguzi ambao ni wananchi sio mgombea, na ndio maana kuna kanuni zake kila chama na nchi zinatofautiana. Isipokuwa Utawala wa demokrasia ndio unatakiwa kuwa na maadili fulani ambayo ni pamoja na kuwapa wananchi wake halki sawa na kadhalika (Haki za binadamu)
 
Naam hii haina tofauti na ile niliyoiweka mimi ila natafuta mahala panaposema mgombea Uwakilishi/Bunge anatakiwa kupata silimia 50 ya kura - wewe umepaona?
Kuna kipengele hiki hapa ambacho kipo ukurasa wa 41.....

xiii) Uteuzi wa mwisho wa wagombea
Katika vikao vya mwisho vinavyofanya uchaguzi wa
kumpata mgombea mmoja ambaye Chama Cha
Mapinduzi kitawasilisha jina lake katika vyombo vya
Dola, ni yule atakayekuwa amepata zaidi ya nusu ya
kura zote halali zilizopigwa.
 
Kwa ufafanuzi sahihi ni kwamba kilichofanyika leo na CC ya NEC ya CCM ni kupanua demokrasia ya maamuzi kwa kurejesha majina mawili ya mshindi wa kwanza katika kura za maoni na mshindi wa pili ili sasa Mkutano Mkuu wa jimbo upigie kura majina hayo mawili na baadae kutoa fursa kwa vikao vya juu yaani Kamati za siasa za wilaya na mkoa na baadae CC kujadili na kumpitisha mmoja wapo. Sioni mkanganyiko tena. kwani katika hesabu za kawaida kati ya hao wawili, lazima mmoja apate zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote au wagongane au wafungane kwa kupata asilimia hamsini kila mmoja. huo ndiyo uzuri wa demokrasia. lazima ifuate ili kumpata mtu anayekubalika zaidi kuwakilisha chama chetu.
Wale ambao hawana hoja, na badala yake wanataka kupinga kila kitu, sasa niwakati wa kuaibika.

Mkuu Mwigulu Nchemba,
Tunashukuru kwa ufafanuzi. Nakuomba sana sana sana ukija huku Arumeru kumbuka kubeba Condom! Mambo ya kuparamia wake zetu kavu kavu hatupendi!

 
Hapa hakuna cha aclimia ham sini na nikwamba walichakachu kwa wajumbe wakampitisha kinyamela sasa wameona huyu jamaa {sioi} kuwa cyo ki2 na hanafact kwa watu ndio sasa wanataka kumpitisha sarakkya kwa danganya toto eti kumshindanisha sioi na sarakkya. Ni mag.amba matupu tu na mwanya huu chadema lazma wapite.
 
Bila shaka haki ya KUCHAGUA haiwezi kuwa haki ya kugombea bali unachagua chama au mtu unayemtaka, na Haki ya KUCHAGULIWA inatokana na wachaguzi ambao ni wananchi sio mgombea, na ndio maana kuna kanuni zake kila chama na nchi zinatofautiana. Isipokuwa Utawala wa demokrasia ndio unatakiwa kuwa na maadili fulani ambayo ni pamoja na kuwapa wananchi wake halki sawa na kadhalika (Haki za binadamu)

Mkuu unatunia semi ngumu kueleweka
Ipo hivi unahaki ya kuchagua uiwapo utafikisha miaka fulani na una akili timamu na umekidhi vigezo mfano unashahada ya kura
Na una haki ya kuchaguliwa iwapo utatimiza miaka fulani una akili timamu na umekidhi vigezo, mfano kupitia chama nk
Sasa iwapo kundi la watu fulani tu likiwa ndilo lenye power ya kuamua nani wa kuchaguliwa hii si sawa
Sana sana mtapishaba kidogo namna ya kuteua wagombea lakini msingi ni kila mwenye sifa anahaki ya kuomba
Sasa huu ndio msingi wa demokrasia kinyume cha hapo ni kupora demokrasia
 
Back
Top Bottom