Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Katiba ya SASA haisemi hiyo asilimia 50, labda baadaye. Hii ya leo nadhani ni busara tu za Kamati Kuu, na nadhani wako sahihi. Saa nyingine lazima uangalie busara badala ya katiba (hasa ya vyama vya siasa).

Mkuu,

Mbona umekuwa mgumu sana kuelewa? pamoja na maelezo yote ambayo yametolewa kwenye thread hii bado unasema katiba ya sasa haisemi hiyo asilimia 50?

Umeisoma katiba yenyewe? Au ndio ubishi wa vijuweni bila data? Soma tena thread hii na utajua ukweli wote.
 
Hii ni njia ya kuwapa wajumbe another rushwa, then Sioi we will be winner again cause ana pesa.
 
Kuna kipengele hiki hapa ambacho kipo ukurasa wa 41.....

xiii) Uteuzi wa mwisho wa wagombea
Katika vikao vya mwisho vinavyofanya uchaguzi wa
kumpata mgombea mmoja ambaye Chama Cha
Mapinduzi kitawasilisha jina lake katika vyombo vya
Dola, ni yule atakayekuwa amepata zaidi ya nusu ya
kura zote halali zilizopigwa.

Mkuu bala,kanuni hii inaeleza wazi kuwa jina ambalo vikao vya juu vya maamuzi ya chama ni lile ambalo limepata zaidi ya 50%.Iweje sasa kamati kuu ikubali kuketi na kujadili majina ambayo hayajafikisha nusu ya kura?Kipi kinaanza kati ya hivi vitu viwili?Anapatikana kwanza mwenye zaidi ya 50% au inaketi kwanza CC?Ni kweli uchaguzi mkuu uliopita CCM hawakutumia hii kanuni na hata sasa mpango wao ilikuwa ni kutoitumia!Na wala wasidanganye kuwa wamerejea kwenye kanuni na huku wakifanya tofauti na kanuni hiyohiyo rejewa inavyoelekeza!Ninaamini kabisa kuwa angeongoza wanayemtaka wala haya mambo ya kanuni tusingeyasikia.Hao akina Mwigulu wawe wazi tu kwamba mambo hayajaenda kama walivyotaka na sasa wanaamua kurudi ndani ya chumba cha uchaguzi wa kura za maoni kuendelea na hatua zinazofuata(ambazo hazikufuatwa makusudi) baada ya uhesabuji wa kura kumalizika na matokeo kutangazwa.Na kwa kuwa matokeo yanaonyesha hamna aliyefikisha nusu basi wawili wa juu watapigiwa kura na wajumbe.Baada ya hapo jina la aliyepata 50% litapelekwa kwenye vikao vya maamuzi.Kilichofanyika sasa ni kucancel process nzima iliyokosewa(kwa kanuni waliyoiamua) na kuirudisha ile siku ya kura za maoni ili taratibu ziende kwa kufuata hiyo kanuni!
 
Msalie mtume....Pengine ndivyo baba yake alitaka ifanyike!

Kwa alimwambia nikifa kachukue form chap chap? Huyu kalazimishwa tuu. Inawezekana hajua hata mbele na nyuma ya siasa.
 
Balantanda;

Likely kama mtu wa CC angeshinda CCM ingefunika kombe na angetangazwa hivyo hivyo;nina uhakika Sioi Sumari siyo mtu wao na huenda kuwa MKWE wa LOWASSA kumemponza kijana huyu!William Sarakikya ana nafasi kubwa sasa maana wale wote walioenguliwa watawaeleza wapambe wao wampe kura!

Pole Sioi!

Namfahamu Sioi vizuri at a personal Level.Huyu ni Company Secretary wa Stanbic Bank Tanzania,sidhani kama alikua na involvement kubwa na siasa ila anajaribu kutumia jina la Marehemu Mzee wake na Jina la Lowassa.Akitolewa Sioi mjue ndio hivyo hivyo atakavyotoswa Lowassa 2015.
 
Kwa bahati mbaya sana kikao cha kamati kuu ccm kimefanikiwa kuwa danganya wasiojua kwamba hoja ya kurudia kura za maoni arumeru ni asilimia.kwanza ndani ya katiba ya ccm hakuna mahali wanapotaja kwamba mgombea ubunge afikishe zaidi ya asilimia 50,kama ipo ibara waje hapa wataje ni ibara gani na ni katika jimbo gani utaratibu huo ulisha wahi kutumika?kwa kadri nilivyojua tangu mwanzo na hasa kupitia wanachama wenyewe wa ccm kwamba kulikuwa na tuhuma za rushwa na hata kufikia hatua ya kutaja hata rushwa kwamba ilitolewa hadi laki moja na nusu.tuhuma nyingine ni kuhusu uraia wa ndg sioi sumari kwamba ni raia wa kenya na tuhuma ya tatu ni kwamba ndg sioi sumari ni muumini wa lowasa na hivyo fedha za kuhonga zilitoka kwa lowasa na mwisho ni kwamba mwigulu nchemba na stephen wasira walitumwa kuhakikisha kwamba mgombea wa benard membe ndg sarakikya anashinda na ndio maelekezo ya kikweke .kwa sababu hizo hapo juu kwa chama ambacho kinajifanya kuwa kina uzoefu mkubwa kimeshindwa kujibu au hata kusemea tuhuma hizo zote badala yake wametangaza tarehe nyingine ya kurudia kura za maoni kwa hoja nyepesi.hii haiondoi ukweli wa hoja hizo na kwa maana hiyo ni kwamba ccm wamebanwa wakatafuta the so called exit point which is not sustanable!nawa sihi chadema msifanye makosa na panga mipango wa watu makini kwa ushindi usipange mtu kwa sababu ya sura,gari,kelele jali uwezo wa kupanga ,kuratibu,kuamua ,k usimamia na wakati huo huo kutoa maelekezo sahihi kwa watu wa chini yake.ushauri wakati ccm wanaendelea kudanganya watu nyie semeni ukweli hata kama unauma kwa sababu huwa unauma kwa kawaida.
CCM siyo chama cha siasa siku hizi ila ni genge lenye maslahi binafsi na uchumi wa TZ. Yeyote aliye makini lazima aingie kwenye mizengwe, au unyimwe uraia, au upate shida nyingine za kutengenezwa ikiwepo kukolimbwa, kum'kyembwa etc. Be ware CCM si chama!! cha siasa.
 
Hii sheria ya asilimia 50 plus mbona siku nyingi haifanyi kazi! au ndiyo kubebana? hapa ni kwamba mmoja alikuwa na kashfa ya kutumia rushwa na adhabu yake ilikuwa kuondolewa na mshindi wa pili kuchukua nafasi!! kilichofanyika sasa ni uchakachuaji!!

Hapa ndo utagundua EL ana nguvu kiasi gani, hadi Magamba wanaogopa kumng'oa mkwewe wazi wazi....Eti kisa Fifty Percent, hahahaa....
Hapa issue ni kwamba SIOI na EL wametumia Fifty Cent lkn hajafikisha Fifty Percent......

Magamba kwa kuogopana bwana, sijui nani kawaroga hawa ndugu zangu...? Haya bwana, sie yetu macho.....
 
Dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, hiyo laana itawatafuna CCM hadi wakome. Mara nyingi wanapoendekeza propaganda za kihuni kuwa kuna vyama vya kidini sijui kikabila sasa ngoja tuone huko Arumeru. Hayo mambo kuwa hakufikisha 50% hakuna lolote ni uhuni tu, wao wangesema labda ni rushwa au kuna kambi imeshindwa, kwani kama ni rushwa mbona CCM ndiyo zao, hakuna mwenye uwezo wa kumnyoshea kidole mwenzake, labda wanazidiana dau tu, hata hivyo acha watoane macho tu.
 
Kurudiwa sio tija suala la msingi linalopaswa kujadiliwa ni RUSHWA je ni wajumbe gani watakaopiga kura? Nadhani haitaleta maana yeyote ile iwapo wajumbe wanaosadikiwa kupewa rushwa watapewa nafasi nyingine ya kuteua mgombea, ingekuwa ni vyema sana kama NEC ingewaondoa wagombea wote wa awali kwani walihusika na rushwa iwe ndogo ama kubwa; jimbo tunalichukua tena hata kama tutasimamisha kichaa.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
CCM ni mabingwa wa kahamisha post za magoli wakati football match ikiwa katikatika inaendelea.
Huo utaratibu wa kupata >50% ya kura kwa mgombea ubunge haipo mahala popote kwenye katiba au
taratibu za uchaguzi za CCM. Hatukuwahi kuusikia huo utaratibu kwenye uchaguzi wa 2010.

Ole wao (CCM)Sioi aje ashindwe kwenye hilo dulu la pili mtazijua hasira za EL!

CCM wanafikiri wataendelea kucheza football game kwa kutumia Ice hockey rules milele.
These are two different games. Chama cha wasanii huzaa mamuzi ya Usanii = VIONGOZI WASANII
 
kwa kweli CCM ni landrover 109, kwamba starter ikigoma kupiga unatumia hendeli, huu utaratibu wa nusu ya kura umeanza lini? mbona watanzania tunafanywa wapuuzi kiasi hiki. Yaani chama hakina guideline za kuendesha uchaguzi, wakilala wakiamka wanakuja na utaratibu mpwa walioshauriana kitandani na wake zao au waume zao
Pumb...vu
 
.....CCM bwana
wanajua kwenda na wakati
mara siyoi wsio raia,mara hakufikish 50%,katiba ya CCM inabadilika kila siku
 
ccm ilianza kutumia lini huu mfumo?

nape kama uko humunikumbushe kama ni juzi mliporekebisha katiba yenu tujue.
na kama sio ni wapi tena uliporudia kwa sababu ya kutofikia %?
 
jaman tulio arumeru tulijionea wenyewe hakuna cha asilimia wala nini,kiranja mkuu wa ufisadi yule wa ile kashfa alimbeba mtu kisa kaoa mwanae kuna mengi tu lowasa aliwapa watu chapaa hilo halifichiki chekini atakavyopigwa chin
 
aada ya huu mchezo akifunguka ccm hapatatosha.

hii sinema ni kali?😛hoto:siipati hii kitu.
 
mnakumbuka walivyomtoa sitta uspika?eti safari hii awe mwanamke
 
Kutokana na taarifa nape watarudia kura za maoni tarehe mosi march.hapa naona kuna utata kwa sababu badala ya kujibu tuhuma kadhaa wamehbua hoja ya wagombea kutofikisha asilimia 50 kitu ambacho kimsingi haipo kwenye katiba ya ccm na haijawahi kutumiwa mahali popote vinginevyo wataje ibara pamoja na mfano wa jimbo ambalo utaratibu huo ulishawahi kutumika.pamoja na kwamba ccm kukwepa hoja madai ya kutolewa rushwa,suala la uraia wa sioi sumari,mwigulu na wasira kutumwa ili kuhakikisha sarakikya anashinda,na menginem mengi kwa sababu hata uchaguzi ukirudiwa sio majibu ya hoja hizo.nacho kiona hapa ni ccm kutafuta exit point badala ya kujibu tuhuma hizo nzito.nawashauri watani wao chadema wasifanye makosa hayo na badala yake waendelee kujibu hoja,kusema ukweli,kujipanga,na kushinda ila wakisha dola wasifanyie vikao ikulu na mbaya zaidi ni kutumia rasilimali za watanzania kudanganya watanzania kwa masirahi ya ccm.

hatuna utani na mag.a.mba
 
Na huyo Sarakikya wao atagaragazwa vibaya sana!!! Siasa za CCM siku hizi ni PESA kwanza na sio MVUTO kwanza!!! Kwa formula hii sidhani kwamba Sarakikya ana chake hapo. Labda kama wanataka posho za bure!!!
 
Kura za maoni zinarudiwa baina ya Sioi Sumri na W. Srakikya kwa kuwa hawakufukisha asilimia 50.

Demokrasia CCM ni safu sana.

Source: Nape kupitia Clouds FM

Wanataka kutuaminisha kuna demokrasia nadani ya hiki chama!? mfa maji kweli haishi kutapatapa. Si kunajimbo mshindi wa tatu alipitishwa kibabe 2010!?
 
CCM hawataki tu kukubali kuwa hivi ni vita vya makundi.Fitna....
 
Back
Top Bottom