Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Mkuu.....Kwa hakika sina jibu la swali hilo maana hata katika kanuni na taratibu za uteuzi ndani ya CCM halipo....
Mbona jibu rahisi tu hata katiba imezungumzia, atachaguliwa kwa kura halali, tukitumia mfano wake wa kura 1000 halafu 350 zikaharibika kwa msingi huo kura halali ni 650 percentage itatafutwa kwa kura halali 650 simple. Labda mjadala ni kura halali ni zipi, pamoja na zilizoharibika.
 
Mkuu unatunia semi ngumu kueleweka
Ipo hivi unahaki ya kuchagua uiwapo utafikisha miaka fulani na una akili timamu na umekidhi vigezo mfano unashahada ya kura
Na una haki ya kuchaguliwa iwapo utatimiza miaka fulani una akili timamu na umekidhi vigezo, mfano kupitia chama nk
Sasa iwapo kundi la watu fulani tu likiwa ndilo lenye power ya kuamua nani wa kuchaguliwa hii si sawa
Sana sana mtapishaba kidogo namna ya kuteua wagombea lakini msingi ni kila mwenye sifa anahaki ya kuomba
Sasa huu ndio msingi wa demokrasia kinyume cha hapo ni kupora demokrasia
Kama nilivyosema wewe unayo Tafsiri yako maana hata kule ambako hakuna demokrasia wanaweza kuweka vitu hivyo wazi, hata Burma mtu yeyote anaruhusiwa kujiandikisha kugombea au kupiga kura lakini hawana Demokrasia maana kwa sababu wananchi hawapewi mamlaka ya kuwachagua viongozi bali wanaletewa list ya viongozi na wachague toka hao..

Unachoongea wewe hapa ni SHERIA - act na sio tafsiri ya Demokrasia. Discriminatory in voting practices got nothing in process na mgombea unless haki yake kama raisa ndio inavunjwa, Demokrasia inawatazama wananchi wapiga kura zaidi ya mgombea kuchagua kiongozi wamtakaye, sijui kama umenielewa.
Na nimekupa mifano huko nyuma kwamba hata hao mabingwa wa Demokrasia wameshindwa kuitekeleza kwa kutumia mfamo wako. - Nani aliyegundua miaka 18 au 20 ndio miaka inayotakiwa mtu kugombea ndio iwe Demokrasia?. Hata asiye na akili timamu nani kasema huyu hana haki ya kugombea na akigombea basi kutakuwa hakuna demokrasia.
Mkuu wangu ni wananchi kumchagua viongozi wao ndio tafsiri ya Demokrasia dhidi ya Udikteta (pinzani) ndiko tulikotokea..hayo mengine yote ni sheria za kikatiba zinazomfunga mwananchi na viongozi as to control and outlaw all human discrimination.. lakini hakuna tafisiri zaidi ya niliyokupa.
 
Mbona jibu rahisi tu hata katiba imezungumzia, atachaguliwa kwa kura halali, tukitumia mfano wake wa kura 1000 halafu 350 zikaharibika kwa msingi huo kura halali ni 650 percentage itatafutwa kwa kura halali 650 simple. Labda mjadala ni kura halali ni zipi, pamoja na zilizoharibika au za wajumbe wote waliopiga kura.
Asante sana mkuu.....Hope Matola na mdau mwingine wamekuelewa.....
 
Kuna huyu mkuu aliuliza hivi
ccm hawajui hesabu wanadhani wagombea wakiwa wawili basi mmoja atapata zaidi ya 50% wakati kiukweli siyo. mathalani kama wapiga kura wapo 1000 halafu katika kura zilizopigwa ikatokea kura 350 (35%) zimeharibika then hakuna mgombea atakayefikisha 50% (endapo angalau kila mgombea anapata zaidi ya 25% ya kura zote).

swali: ccm watatumia kipengele kipi ktk katiba kumpata mshindi?
Nikamjibu hivi nikimaanisha yawezekana watapigia hesabu kura ambazo hazija haribika kupata hiyo asilimia 50
Zitatumika asilimia za kura nzima may be
Ukauliza hivi
Kwani hizo asilimia haziwezi kupatikana kwenye kura za awali!!?? think Big my friend.
Nikakujibu
Za awali zipi wakati hazijafika asilimia 51???? think Big my friend

Mara yamekuwa ya kimagamba, au ulimaanisha za awali zipi?
Wewe umeshafunikwa na hesabu za kimagamba za 2+2-4=
 
ccm hawajui hesabu wanadhani wagombea wakiwa wawili basi mmoja atapata zaidi ya 50% wakati kiukweli siyo. mathalani kama wapiga kura wapo 1000 halafu katika kura zilizopigwa ikatokea kura 350 (35%) zimeharibika then hakuna mgombea atakayefikisha 50% (endapo angalau kila mgombea anapata zaidi ya 25% ya kura zote).

swali: ccm watatumia kipengele kipi ktk katiba kumpata mshindi?

Mkuu hebu tusaidie ufafanuzi kwenye post # 195.

Nadhani hili hapa chini ni jibu tosha kwa maswali hayo mawili hapo juu...

Mbona jibu rahisi tu hata katiba imezungumzia, atachaguliwa kwa kura halali, tukitumia mfano wake wa kura 1000 halafu 350 zikaharibika kwa msingi huo kura halali ni 650 percentage itatafutwa kwa kura halali 650 simple. Labda mjadala ni kura halali ni zipi, pamoja na zilizoharibika.
 
Balantanda;

Likely kama mtu wa CC angeshinda CCM ingefunika kombe na angetangazwa hivyo hivyo;nina uhakika Sioi Sumari siyo mtu wao na huenda kuwa MKWE wa LOWASSA kumemponza kijana huyu!William Sarakikya ana nafasi kubwa sasa maana wale wote walioenguliwa watawaeleza wapambe wao wampe kura!

Pole Sioi!
Tukubali Sioi amechinjiwa baharini that isn't democracy at all.
 
Hivi kuna anayejua historia ya kisiasa ya Sioi?......

Ni upi ushiriki wake katika siasa(zaidi ya kuwa mwanachama) za ndani za CCM?....Kuna anyejua atujuze?
Balantanda now you are talking.... huo ndio msingi wa Sioi kukataliwa,
mimi nadhani hapo ndipo ilipo nguvu ya CC... 'can you tell us who are you' usifikiri umeulizwa jina,
if that is the case so kwa nini basi kuna kura za maoni na uchaguzi ulikuwa wanini.
 
Balantanda;

Likely kama mtu wa CC angeshinda CCM ingefunika kombe na angetangazwa hivyo hivyo;nina uhakika Sioi Sumari siyo mtu wao na huenda kuwa MKWE wa LOWASSA kumemponza kijana huyu!William Sarakikya ana nafasi kubwa sasa maana wale wote walioenguliwa watawaeleza wapambe wao wampe kura!

Pole Sioi!

Malafyale,

Ukiachia kura za maoni za 2010 ni nani umewahi kuona anashinda CCM kwa kura chini ya asilimia 50?

Wakati wa uchaguzi mkuu, CCM huwa wanatoa kanuni za uchaguzi. Hizo ndio zinafafanua kwa undani juu ya namna ya kuendesha uchaguzi.

Kwa mwaka 2010 baada ya kuruhusu wanachama wote kupiga kura, waliamua pia kwamba utakuwa usumbufu na gharama kubwa kutaka mshindi awe na zaidi ya asilimia 50. Ikaamuliwa matokeo yoyote yale yatakayopatikana kama yameendeshwa kihalali basi yapelekwe juu na kamati kuu itaamua.

Lakini kwa hizi chaguzi ndogo, utaratibu unarudi ule ule wa kama kwenye katiba. Hawa waliosimamia kura walifanya makosa kutokuruhusu washindi wawili kupigiwa tena kura.
 
Pia wamekemea kitendo cha kusema Lowasa Katoa hela kwa ajili ya Sioi wakati hela hizo zimetolewa na Fred Lowasa pamoja na rafiki zake.

kwani watu wanakosea kusema hela imetoka kwa Lowasa? Si ni kweli imetoka kwa Fred Lowasa???
1.JPG
 
Hili jambo nilishangaa sana nilipoona matokeo. Katiba ya CCM inataka mshindi apatikane kwa zaidi ya nusu ya kura.

Sijui ilikuwaje kiongozi wa juu kama Mwigulu hakuliona hili?

Kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 walifuta hiki kifungu cha umuhimu wa nusu kwasababu kura zilikuwa zinapigwa na wanachama wote. Ilikuwa ngumu na gharama kuendesha uchaguzi mara mbili.

Kwenye chaguzi zote za mwanzoni ambazo zilikuwa zinafanywa na mkutano mkuu wa wilaya, nusu ni lazima.

Nafikiri wamefanya la maana kuamua kufuata katiba.
Katiba ya SASA haisemi hiyo asilimia 50, labda baadaye. Hii ya leo nadhani ni busara tu za Kamati Kuu, na nadhani wako sahihi. Saa nyingine lazima uangalie busara badala ya katiba (hasa ya vyama vya siasa).
 
Mkuu uko sahihi katika maoni yako lakini huoni kama mwishoni umeonekana kugusia wasifu wa mmoja na kumuacha mwingine hivyo kuwaacha wapiga kura katika muono wa upande mmoja. Nadhani tuwape nafasi wanaCCM wa Arumeru kumchagua wanae amini kuwa atawawakilisha vyema katika ushindani wa vyama.

Mkuu kama hilo laweza kuwa tatizo nipo tayari kukutakeni radhi! Ila hili nimelisema si kwa nia mbaya ila mazingira; unajua wewe unapokuwa Jaji halafu baba yako akaletwa mbele yako kwa kosa la kuua unachopaswa ni kujitoa kwenye kesi hiyo manake kama usipojitoa na ukamuhukumu baba yako kunyongwa kutokana na Sheria watu bado watanung'unika wakidhani umempendelea mzazi wako.

Hivyo mimi nimelazimika kufanya hivyo kwa sababu ya mazingira yaliyopo manake hata kama Katiba inamruhusu Sioi kugombea ila kwa kweli bado walakini ni mkubwa mno kwanza hata arobaini ya mzazi wake bado kwisha lakini pili ni juu ya uthubutu na uwezo mnaweza shangaa akasema baba ndo aliniambia nigombee hii jamii tutaiambia nini??

Naomba nisimamie pale pale Sarakikya piga moyo konde..........
 
Mwigulu LM Nchemba said:
Kwa ufafanuzi sahihi ni kwamba kilichofanyika leo na CC ya NEC ya CCM ni kupanua demokrasia ya maamuzi kwa kurejesha majina mawili ya mshindi wa kwanza katika kura za maoni na mshindi wa pili ili sasa Mkutano Mkuu wa jimbo upigie kura majina hayo mawili na baadae kutoa fursa kwa vikao vya juu yaani Kamati za siasa za wilaya na mkoa na baadae CC kujadili na kumpitisha mmoja wapo. Sioni mkanganyiko tena. kwani katika hesabu za kawaida kati ya hao wawili, lazima mmoja apate zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote au wagongane au wafungane kwa kupata asilimia hamsini kila mmoja. huo ndiyo uzuri wa demokrasia. lazima ifuate ili kumpata mtu anayekubalika zaidi kuwakilisha chama chetu.
Wale ambao hawana hoja, na badala yake wanataka kupinga kila kitu, sasa niwakati wa kuaibika.
Hapana Mwigulu LM Nchemba, naona umeamua kuchakachua hata taratibu zenu wenyewe!

Kwa utaratibu wa CCM siku ya kupiga kura za maoni inakuwa ni moja tu, na ikitokea kuwa mshindi hakupata asilimia 50%, wagombea wengine huchujwa na kubakizwa wagombea wawili walioongoza halafu kura hurudiwa siku hiyo hiyo katika kikao hicho hicho.

Sababu pekee ambayo inayoweza kufanya matokeo yafutwe na uchaguzi urudiwe siku nyingine ni kama kuna tuhuma za haki kutotendeka katika uchaguzi wa awali kama matendo ya rushwa, udanganyifu, wizi n.k., tuhuma ambazo lazima zithibitishwe.

Haya ya Arumeru ni funika kombe mwanaharamu apite!
 
Balantanda now you are talking.... huo ndio msingi wa Sioi kukataliwa,
mimi nadhani hapo ndipo ilipo nguvu ya CC... 'can you tell us who are you' usifikiri umeulizwa jina,
if that is the case so kwa nini basi kuna kura za maoni na uchaguzi ulikuwa wanini.

Yea, tell us about yourself. Ulizaliwa lini na wapi ikizingatiwa inadaiwa kwenye ile form aliacha wazi sehemu ya kuhaza uraia wake? Interviews nyingine noma.

Kusema kweli sijui ni kwa nini huyo jamaa aliamua kugombea ubunge. For this particular time, he should have been grieving for the loss of his father, for God sake. Hivi hata matanga yameisha?
 
Msalie mtume....Pengine ndivyo baba yake alitaka ifanyike!
 
Kwa utaratibu wa CCM siku ya kupiga kura za maoni inakuwa ni moja tu, na ikitokea kuwa mshindi hakupata asilimia 50%, wagombea wengine huchujwa na kubakizwa wagombea wawili walioongoza halafu kura hurudiwa siku hiyo hiyo katika kikao hicho hicho.

Sababu pekee ambayo inayoweza kufanya matokeo yafutwe na uchaguzi urudiwe siku nyingine ni kama kuna tuhuma za haki kutotendeka katika uchaguzi wa awali kama matendo ya rushwa, udanganyifu, wizi n.k., tuhuma ambazo lazima zithibitishwe.

Haya ya Arumeru ni funika kombe mwanaharamu apite!
Kweli mkuu ndivyo inavyotakiwa, kama kuna mgombea hakufikisha 50% uchaguzi unarudiwa kwenye kikao kile kile hatoki mtu ikibidi kukesha mnakesha, cha kushangaza leo majina yamefika CC sasa yalipelekwa kufanywa nini kukudolewa macho au, ninachojua kule lingeenda jina moja tu ambalo CC ingelikubali au kulikataa. Labda tusiingilie sana ni mageuzi mapya wengine tulikuwa kwenye CCM ya miaka ya 80.
 
Acha usharo baro hapa..
Matokeo ya form 4 yameshatoka hivi hakuna mweye taarifa hizi shule zinafunguliwa lini? maana hivi vitoto vya facebook vinadhani sisi tuko hapa kutafuta wachumba. nakerwa sana na uandishi wa kipuuzi namna ile.
 
Back
Top Bottom