kura ya maoni; Zitto vs Mbowe

kura ya maoni; Zitto vs Mbowe

piga kura yako hapa, kati ya zitto kabwe na mbowe freeman, yupi ana mvuto wa kisiasa zaidi?

acha jazba changia na piga kura yako kimya kimya na kwa ustaarabu, rudi nyumbani kapumzike, subiri matokeo. hairuhusiwi kufanya vurugu.

WARAKA WA CHACHA WANGWE.
UTANGULIZI.
Jumamosi, June 28 mwaka huu
wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya
CHADEMA walidai kuwa wamesitisha
Umakau Mwenyekiti wangu katika
kikao kilichofanyika mjini Dodoma
siku hiyo. Kesho yake Mwenyekiti wa
CHADEMA Taifa, Mhe. FREEMAN
MBOWE akaitisha mkutano wa
waandishi wa habari na kutaja
sababu za kunisimamisha uongozi.
Inatosha tu kusema kuwa sababu
zote alizotoa ni za uzushi kama ile
inayodai kuwa mimi navujisha siri za
chama kwa viongozi wa CCM bila
hata kutaja siri hizo, au kusema
nimezitoa lini, wapi, na kwa kiongozi
yupi?Kikao hicho kinachosemekana
kunisimamisha uongozi, kilikuwa na
wajumbe 31 ambao takribani nusu
hawakuwa na uhalali wa kupiga kura
kinyume cha katiba na kanuni za
CHADEMA kwa vile walikuwa
wameandaliwa kwa kazi hiyo.
Wajumbe 7 walikataa kushiriki
njama hizo.
Kufuatia jaribio hilo la kunivua
uongozi kutokubalika kwa
wanachama walio wengi wa
CHADEMA , Mwenyekiti MBOWE na
wafuasi wake wameendelea kuhaha
kwa kuongeza sababu nyingine
mbalimbali ili kuhalalisha njama zao.
Sasa hivi wameingia hatua ya
kuwashawishi wanachama wa
Tarime eti wanifukuze
uanachama.Kwa kuzingatia katiba,
kanuni na taratibu za CHADEMA,
nilichokifanya mimi baada ya
kubaini njama zao ni kukata rufaa
kwa Baraza Kuu la Chama, kupinga
upotoshaji unaofanywa chini ya
uongozi wa Mhe. MBOWE
anayeonekana kutaka kuendesha
chama kinyume na matarajio ya
wanachama walio wengi.Hivyo basi
zipo habari za uhakika kuwa kikao
hicho cha Baraza Kuu hakitaitishwa
ama kabisa, au kitacheleweshwa
kwa makusudi, kwa visingizio
mbalimbali ikiwemo kutokuwa na
fedha za kukidhi gharama za kikao
hicho.
Naomba nikiri kuwa ninakerwa sana
na mtiririko mzima wa sakata hili
linalozua mgogoro unaokiyumbisha
chama. Ukweli ni kwamba mimi
niligombea Umakamu Mwenyekiti
nikiwa na agenda ya kufufua uhai wa
chama kwa kukaripia vitendo
visivyostahili katika kuendesha
chama. Agenda yangu haijabadilika.
Yote niliyoyasema wakati nagombea
nafasi hii yanafahamika kwa wana
CHADEMA wote.
Walikuwepo walioyalalamikia na
walikuwepo walioyapongeza
matamshi yangu hayo.Mwisho wa
yote wana CHADEMA waliridhika
kuwa ajenda yangu ilikuwa sahihi na
hivyo wakanichagua kuwa Makamu
Mwenyekiti. Hivyo basi hata kama ni
kweli kuwa ulikuwepo mvutano
wakati wa kampeni ile, lakini hilo ni
jambo la kawaida katika uchaguzi.
Nijuavyo mimi hayo yalitakiwa yawe
si ndwele nasi tugange yajayo kwani
wanachama walikwisha fanya
uamuzi halali kupitia kura zao.
Baada ya kuingia kwenye wadhifa wa
Makamu Mwenyekiti Taifa,
nilifanikiwa kuzungumza na Mhe.
MBOWE kuhusu mambo, hususan
yale, niliyoyapigania wakati wa
kinyang?anyiro kile na kumuomba
tukae chini na kutafuta jinsi ya
kufanikisha azma hiyo.Ni imani
yangu kuwa waraka huu utawasaidia
wanaCHADEMA wenzangu na
watanzania wote kwa ujumla,
kuelewa vizuri ukweli wa mambo
niliyoyapigania kabla ya kuwa
Makamu Mwenyekiti, na
ninayoendelea kuyasimamia hivi
sasa nikiwa Makamu Mwenyekiti, na
inshallah nitakayoyatekeleza baadae
kama Taifa Mwenyekiti wa
CHADEMA.
Kimsingi mambo tunayotofautiana
na Mhe. MBOWE ni haya yafuatayo:-
MATUMIZI YA RUZUKU
CHADEMA hupata ruzuku ya Tshs.
66,000,000 kwa mwezi (Milioni sitini
na sita). Mimi nasema si haba hasa
tukizingatia chama kilikotoka.
Naamini kuwa kiasi hiki cha fedha
kikisimamiwa vizuri kinaweza
kukirahisishia chama kujieneza
katika ngazi zote toka Tawi, Wilaya,
Mkoa na Taifa.
Si kweli kwamba matatizo yote
yatamalizwa na fedha hizi lakini basi
hata ofisi za chama zinaweza kuwa
hai nchi nzima kitu ambacho kwa
sasa hakipo. Mahesabu yanaonesha
kuwa mtaji wa laki moja
(Tshs.100,000/=) kwa wilaya moja
nchini inatosha, hivyo kwa Wilaya
126 kwa mwezi jumla yake ni Tshs.
milioni 12 (Tshs. 12,600,000/= )
zinahitajika ( Wilaya 126 x 100,000
kila wilaya = 12,000,000/=)Hata
tukisema tupeleke kiasi hicho kwa
kila jimbo la uchaguzi jumla yake ni
Tshs. Milioni 23 (Tshs. 23,000,000/=)
kwa maana ya majimbo 213 x
100,000 = 23,000,000/=.
Mhe. MBOWE anasema hizo ni pesa
nyingi sana kwa uimarishaji wa
chama. Mimi nasema hapana,
kiwango hiki kwa kila Wilaya au
Jimbo la uchaguzi ni muafaka kwani
haba na haba hujaza kibaba.Chini ya
uongozi wa Mhe. MBOWE na wafuasi
wake hawastaajabu kuwa kati ya
Tshs. 374,144,000.40 zilizopatikana
kama ruzuku katika ya Januari 1 na
Juni, 30, 2008, Tshs. 350,000,000/=
zilitumika Makao Makuu ya
CHADEMA na Tshs. 25,000,000/= tu
ndizo zilikwenda Wilayani
kuimarisha chama.Mimi naona mgao
huu unayatukuza Makao Makuu ya
CHADEMA isivyostahili wakati huo
huo ukidhalilisha chama nchi nzima.
MADENI YA UCHAGUZI
Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha
wanachama kuwa alikuwa anakidai
chama US $ 181,949.00 sawa na
Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa
chama kimekwisha mlipa Tshs.
175,000,000/=Baada ya kupata
wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na
kwa kuzingatia takwimu zionekanazo
hapo juu katika kulinganisha
matumizi ya fedha Wilayani na
Makao Makuu niliamua kumshauri
MBOWE asitishe kujilipa deni
kutokana na fedha za ruzuku kwani
siamini kuwa kulipa madeni
yaliyopita kunaendana na utaratibu
wa usimamizi wa fedha za ruzuku
kwa vyama vya siasa toka serikalini.
Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo
nilipomshauri kuwa kama ni hivyo
basi atuthibishie pesa hizo anazodai
alikikopesha chama ziliingia kwenye
akaunti gani ya CHADEMA, kupitia
hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia
kutaja ni kikao gani cha chama
kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo
kwani kama hakuna ushahidi wa
maidhinisho, ni dhahiri kuwa
matumizi hayo hayakudhibitiwa na
chama na kwa mantiki hiyo
kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya
Mhe. MBOWE.Vilevile, nilimueleza
kuwa matumizi ya fedha hizo
alizodai alikikopesha chama
yalikuwa yakinuka harufu ya
UFISADI.
Stakabadhi zote kuhusiana na
matumizi hayo zilionesha kuwa
gharama za aidha ununuzi na / au
ukodishaji wa vifaa hivyo,
hazikutofautiana na viwango
wanavyolipishwa watalii kwa
huduma kama hizo, kwa maana ya
gharama ya juu sana.Na kwa kuwa
hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE
amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya
deni alilodai kuikopehsa CHADEMA,
vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza
sauti na kadhalika vimebakia kuwa
mali yake binafsi, basi bila kumficha
nilimueleza kuwa huko ni
kukinyonya chama kwa kukigeuza
kitega uchumi cha watu
binafsi.Kuhusu suala la kulipa
madeni kupitia ruzuku ya serikali,
nilimuomba Mhe. MBOWE afuatilie
kwa Msajili wa Vyama vya siasa ili
tupate ufafanuzi kama kweli fedha
za ruzuku ya serikali kwa vyama vya
siasa, inaweza kutumika kulipia
madeni ya viongozi wa vyama hivyo
yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA
isiathirike kisheria.
Niseme kweli hapa kwamba, kwa
vile wanaCHADEMA wengi
walinichagua kuwa Makamu
Mwenyekiti, na hata mimi
mwenyewe tulikuwa wagombea wa
nafasi za ubunge, udiwani n.k katika
uchaguzi wa mwaka 2005
ningefarijika sana iwapo na sisi
tungerejeshewa angalau chochote
cha kufidia gharama zetu, kwa
maana kwamba kama chama
kimeamua kurudisha gharama hizo
kiwalipe wote badala ya kulipa
madeni kwa wateule wachache.
UTEUZI WA WABUNGE WA VITI
MAALUM
Naamini ukweli wa suala hili hauna
mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na
wafuasi wake walighushi orodha ya
majina ya viti Maalum badala ya
kupeleka yaliyopendekezwa na
Kamati Kuu sio siri.
Naamini hata Mhe. MBOWE
anakubaliana nami kuwa suala hili si
moja ya siri anazodai nimevujisha!
Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku
uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi
baadhi ya waasisi wa chama
wakataka kujitoa na hivyo
kumlazimisha Mwenyekiti Taifa
( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu
(DR WILBROAD SLAA) kukiomba
radhi kikao cha Kamati Kuu ya
CHADEMA kwa kukiuka katiba,
kanuni na maadili ya chama katika
suala hili la kugushi viti maalum.
Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo
hicho cha upendeleo bado kina
iumiza taswira ya CHADEMA. Chama
kinaonekana kuendekeza ujanja
ujanja kiasi kwamba watu na binti
zao, wakwe zao, shemeji zao, waume
wenzao, wachumba wa shemeji zao,
wake wenza na kwa kiwango
kikubwa watu wa kabila moja ndiyo
wamekuwa sura ya CHADEMA
bungeni.Katika hili nilichoweza
kumueleza Mhe. MBOWE ni kuwa
chaguzi mbalimbali tangu za Mitaa,
Ubunge na Urais zinakaribia ni vizuri
tufanye bidii kusambaza nguvu zetu
nchi nzima tuwe na mtaji wa kura
maeneo mengi ili kashfa kama hii
isijirudie. Hii ni kwa msingi kuwa
chama kikijitanua kutakuwa hakuna
sababu ya kuwaona watu wa eneo
fulani tu kuwa ndiyo mhimili wa
CHADEMA na hivyo zikitokea fursa
itakuwa rahisi chama kuwakilishwa
na mtandao wake mpana badala ya
koo au kabila fulani.Sasa kwa kuwa
kuimarisha chama kitaifa maana
yake ni matumizi ya fedha, nalo hili
likawa nongwa ingawa kwa mtazamo
wa Makao Makuu kulipa madeni kwa
wateule wachache si nongwa.
Cha ajabu ni kwamba Mhe. MBOWE
hakukana kuwa hili la viti maalum
na hata upangaji wa ajira kwa
ukabila una leta athari mbaya kwa
mustakabali wa CHADEMA
Katika maongezi yangu nae nilikuwa
wazi nilipotahadharisha kuwa:
1. Watanzania wakiendelea kuona
kwamba CHADEMA inaendeshwa kwa
misingi ya kikabila hawatajiunga na
chama chetu na tutakosa wafuasi.
2. Watanzania wakiona kuwa sisi
tumeweka mbele ukabila kuliko
utaifa hawatatupa madaraka na
kutawala kwa kuhofia yale
yanayotokea nchi jirani kama
Rwanda, Burundi, Kenya na
kadhalika ambako nafasi za raia
wote zimehodhiwa na kabila moja na
hatma yake watu wamechinjana
kama kuku kwa kupinga hilo.
Pia nilimwambia kwamba, kwa jinsi
sura ya uteuzi wa Wakurugenzi na
watendaji wengine wa Makao Makuu
inavyoonekana, sasa tayari chama
chetu kimebatizwa jina la CHAMA
CHA WACHAGA, na hii si kuwatendea
haki raia wengine na makabila yao
ambao wataonekana kama punguani
kujihusisha na chama na
ukabila.Yote haya ninayosema
kuhusu ukabila, upendeleo na
kadhalika sio dhana tu. Kufuatia
malalamiko mengi yaliyokuwa
yakisikika nchi nzima kuhusu
masuala haya, Kamati Kuu ya
CHADEMA ilikwisha unda Tume
kutafuta ukweli wa mambo hayo.
Tume hiyo ya watu watano
iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo
Mziray ambaye ni mjumbe wa
Kamati Kuu ya CHADEMA nayo
imekwisha toa taarifa yake kwamba
Makao Makuu ya CHADEMA
yanatawaliwa na ubaguzi wa
kikabila, kidini na kielimu.
UTENDAJI WA KIBABE
CHADEMA ni chama kilicho njia
panda kwa sasa kutokana na
utendaji wa kibabe wa Mhe. MBOWE.
Ninafahamu jinsi vyama vingine vya
upinzani hapa nchini kama vile
NCCR ? Mageuzi vilivyoporomoka
haraka haraka mithili ya nyumba ya
mabua. Chama NCCR ? Mageuzi
kilifikia mahali pazuri tu hadi watu
wakaanza kufikiria kuwa kingekuwa
chama mbadala kwa CCM.
kwa bahati mbaya uchu wa
madaraka, ulafi wa ruzuku, na tabia
za kimangimeza kwa pamoja
vikakiathiri hadi kupoteza umaarufu
wake.Na hata vyama vingine vya
upinzani vina dalili hizo hizo japo
kwa viwango vinavyotofautiana. Ila
badala ya kujichunguza na kujua
kasoro zetu, kila siku vyama vyetu,
vimekuwa vikidai kuwa ni chama
tawala ndicho kinachoviroga, kama
ambavyo Mhe. MBOWE ameanza
kuweweseka kupitia vyombo vya
habari.Napenda kuthibitisha kuwa
katika mgogoro unaopaliliwa sasa na
Mhe. MBOWE ndani ya CHADEMA
kutokana na ufisadi, ufuska, ulevi
wa madaraka na umangimeza chanzo
chake ni tabia yake ya kuendesha
chama kibabe. Mathalan kumzuia
Martin Mung?ong?o Mkurugenzi
aliyechaguliwa kwa kura kutofanya
kazi zake ndani ya chama, madai ya
kupigana na watendaji wa chama
ndani ya baa na vitendo vingine vya
aina hiyo ni ushahidi tosha wa hulka
hii.
Hadi sasa Mhe. MBOWE amefanikiwa
kukizuia chama hiki kisifanye kazi ya
siasa mkoa wa Dar es salaam kwa
miaka minne.Ninavyoongea hivi sasa
CHADEMA imekuwa ikikimbia vikao
vya Democratic Union of Afrika
(DUA), Muungano wa Vyama Vya
Upinzani, uliofanikisha CHADEMA
kujuana na Conservative Party ya
Uingereza na Republican ya
Marekani. Vyama dada hivi vyote
vinaulalamikia uongozi wa CHADEMA
kwa kufuja fedha ya misaada na
kuwasilisha kwao risiti za kugushi,
kama ilivyofanyiwa Conservative
Party baada ya kutoa msaada wa
Tshs. 78,000,000 kwa ajili ya ununuzi
wa baiskeli na pikipiki ambazo
hazikununuliwa.Katika mkutano wa
Kamati Kuu ya CHADEMA huko
Dodoma hivi majuzi tu, Mhe. MBOWE
kwa kauli yake aliwatisha wajumbe
kuwa alikuwa amethibiti uwezekano
wowote wa wajumbe kujisikia huru
kwa kutoa mawazo ambayo
yangepingana na ajenda yake
aliyoitoa ghafla kikaoni
kunisimamisha Umakamu
Mwenyekiti.
Mhe. MBOWE Alikifahamisha kikao
kuwa alitoa taarifa kwa IGP, SAID
MWEMA kuwa kuna wahuni ambao
walitaka kuuchafua mkutano wake,
naye IGP akahakikisha kuwa
mkutano ule unalindwa kwa kiwango
cha kushtua kama ambavyo hata
vyombo vya habari
vimethibitisha.Hayo ni baadhi tu ya
mambo yanayobainisha Mhe.
MBOWE ni kiongozi wa aina gani.
HITIMISHO
Kama nilivyokwisha sema hapo
awali, sijaacha na sintoacha ajenda
yangu ya kufufua uhai wa CHADEMA
kwani ndiyo ahadi iliyofanikisha
kuchaguliwa kwangu kuwa Makamu
Mwenyekiti Taifa. Nilipopata
wadhifa huo nilianza kuitekeleza
ajenda hiyo kupitia mahojiano na
Mwenyekiti MBOWE kuhusu
matumizi ya ruzuku, madeni ya
uchaguzi, uteuzi wa wabunge wa viti
maalum, nafasi za ajira Makao
Makuu, na kuhusu mwenendo wa
chama Mkoa wa Dar es salaam.
Nilijikuta katika mvutano mkubwa
kila nilipogusa eneo lolote katika
haya. Nakiri kuwa kwa kiwango
kikubwa sikuwa na uwezo wa
kubadili mambo hayo yaliyokuwa
yakiratibiwa kwa ukaribu na Mhe.
MBOWE na wafuasi wake kwani
sikupewa ushirikiano wa aina yoyote
na chama pale Makao Makuu.
Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli
kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu,
sikupewa vitendea kazi kama
magari, vipaza sauti na/au vyombo
vya habari, na sikuwahi kupata
taarifa yoyote ya kiutendaji toka
Makao Makuu.Kwa kuzingatia yote
hayo, naomba nichukue fursa hii
kuwashukuru kwa dhati wanachama
wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam
ambao kwa pamoja tulisimama
kidete kufufua uhai wa chama hapa
jijini. Niseme tu ushirikiano wao wa
hali na mali uliniwezesha
kushughulikia masuala muhimu ya
kitaifa na kimataifa.
Rai yangu kwa wana CHADEMA na
wale wote wanaokitakia mema
chama chetu na nchi yetu kwa
ujumla ni kwamba kazi ya kupigania
demokrasia ya kweli ndani na nje ya
chama, kukiepusha chama na
vitendo vya ukabila, migogoro,
ubadhirifu, umangimeza, ufisadi na
ubaguzi wa aina yoyote bado
inaendelea na nawaombeni mniunge
mkono kwa hali na mali katika vita
hii. Naamini tutashinda.Mungu
Ibariki CHADEMA Mungu Ibariki
TANZANIA Mungu Ibariki AFRIKA
 
piga kura yako hapa, kati ya zitto kabwe na mbowe freeman, yupi ana mvuto wa kisiasa zaidi?

acha jazba changia na piga kura yako kimya kimya na kwa ustaarabu, rudi nyumbani kapumzike, subiri matokeo. hairuhusiwi kufanya vurugu.

Hivi, unalenga nini kwenye hizi kura zako, kwanini umechagua hawa, kwa nini muda huu. Kwa nini usitafsiriwe kuwa u- pamoja na wanaojaribu kuwaambia wananchi kuwa CHADEMA kuna mgogoro mkubwa. Usiwe na jazba jibu kwa ufasaha, hairuhusiwi kutukana.
 
Mbona wana CCM wanamtetea sana ZZK? Hiki ni kiashiria tosha kuwa ZZK hakuwahi kuwa CDM. Mlimtuma kuvuruga CDM. Acheni kuchezea maisha ya wa TZ bana
 
CCM na Zitto wenu mtahangaika sana mwaka huu, kama mnampenda sana mpeni uenyekiti wa CCM!
 
Kwa huu ujinga wenu ndio maana mtu kutoka nafasi ya juu katika balaza la umoja wa mataifa leo hii unateuliwa Mbunge na kuchekelea kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
Kwani ni lazima mawazo yetu yafanane?yani we paka shume umeniharibia siku.
Soon utaitwa mrs Mbowe kenge wewe!
 
mkuu ndo umeishiwa ivyo?kwani lazima kufungua kila siku kwenye jf?mbona furusa ni nyingi nchi hii,au ujawaona watu wa clouds wakusaidie
 
Back
Top Bottom