Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Apo ni sawa na jiwe na mkate af mtu akuulize unakula nini?
 
Tunatekwa na propaganda za CCM,SLAA alikuwa padri tatizo ni nini?mbona Mwinyii alikuwa shee na alituongoza?Abdul Jumbe?,Idrissa Abdul Wakili?huo udini ni kwa wakristo tu?Tuache isia za udini ni propaganda ya CCM ili ihendelee kututawala.Kwangu mimi naona ZITTO ni hazina nzuri kwa CDM ila sio kwa sasa bado inaitajika kupata uzoefu zaidi,Nchi hapa ilipofika inahitaji kiongozi mwenye uwezo mkubwa ili kuirudisha ktk mstari,ZITTO ni chaguo la vijana lkn hata bungeni bado ajaonyasha uwezo wa kuzikabili changamoto.CCM na magazeti yao ya uhuru na mzalendo watampamba sana ila lengo lao ni kuivuruga CDM,Tuwe makiini muda wa kufikiria urais bado tujenge chama kwanza hasa vijini ambako kuna watanzania wengi.
 
Aina ya mada kama hizi zinajadiliwa Facebook,sio JF..CHADEMA inatofautiana na vyama vingine kwa kuamua mambo yake kwa busara na kwa hekima,hasa yale yenye maslahi kwa taifa zima,jamii au chama chenyewe..Kuanza kumfananisha Dr.Slaa na Zitto ni kuanza kuleta vidonda vya kura zisizo rasmi na kukiathiri chama..Maamuzi juu ya nani agombee yatafanyika muda muafaka utakapofika,na si vinginevyo..Na kamwe hatutatumia utaratibu dhaifu kama kura za maoni zisizoratibiwa vema..
 
Mnalinganisha Sisimizi na Tembo? Kama Zitto ana sifa za kuwa Rais ni afadhali CCM itawale miaka 50 ijayo
 
kura yangu ni kwa zitto kabwe.kumpa kura slaa labda awe kalani wa mahakama maana siwezi chagua mtu anayefanya kazi kwa kusikiliza majungu na kwa sasa anaendesha chama kwa nguvu ya mchumba wake josephine mshumbuzi.kumchagua slaa ni sawa na kuipa laana nchi yangu maana huyu mzee kila kitu kachelewa mpaka mapenzi kayajulia uzeeni
 
Namna ya kumjua rais mzuri kwa maana ya utendaji ni hii hapa ukiwalinganisha hawa 2:-

  1. Hivi kwanini Zitto husifiwa sana na watu ambao huwa na mapenzi makubwa na magamba? angalia uchaguzi wa 2009, watu waliotaka sana awe mwenyekiti wa CDM wengi wao walikuwa ni wale wenye maslahi na magamba, here includes TBC, rostam aziz teams.
  2. Mara kadhaa linapotoka tishio la kuwateketeza wana mageuzi (aidha kwa kuwaua au kuwekewa security systems) jina la dokta Slaa huwa lipo? why?
  3. Uasisi wa mapinduzi ya mfumo unaotawala, Zitto Kabwe ni mara chache sana kumsikia analizungumzia hilo, hata Team work management, ni mara chache sana kumwona au kumsikia akilisemea au kujishughulisha nalo, nafikiri hili nalo laweza kuwa doa kubwa endapo atakuja kuwa rais, ukiamini kila kitu utafanya mwenyewe na sio through your team, jiandae ku fail vibaya.
  4. Mimi bado napata shida sana na waislamu, hivi ni kwanini mnapenda sana kuona nchi inaongozwa tu na mwislam mwenzenu hata kama hana uwezo? Hivi shida na tabu tulizozipata kwasababu ya Kiwete bado hazitoshi, naomba umnielewe vizuri, sijasema waislam hakuna wenye uwezo, nina maana Kikwete kama mtu, uwezo wake au udhaifu wake hauna uhusiano wowote na dini yake. Hivi kwa mfano, Kikwete ni mwislamu na yupo Ikulu, nambieni faida mlioipata kama Waislamu ni nini? Sukari, elimu, afya, issue ya NSSF/PPF yote haya madhara yake yapo kwa wananchi wote bila kujali tofauti zetu za dini.
  5. Zitto na Dokta Slaa, katika kipindi chao cha ubunge, kuna vitu wamefanya kwao ambavyo hadi leo ni re-markable, hapa wanafanana.
  6. Tunalo tatizo kubwa la maadili ya kiuongozi katika nchi hii, hasa ufisadi, maisha ya Zitto na kipato chake, tuseme ukweli, kuna ukakasi mwingi sana, hayatafsiriki kabisa.

Mi sitaki kutoa conclusion kati yao nani anafaa, but kwa point hizo chache, labda tunaweza kuanzia kufkiri.
 
Slaa akipitishwa uchaguzi mkuu chadema itashiriki tu na wala sio kushinda maana wanachadema hatumkubali wala nn afu kigezo cha umri hapo ndo mnakosea kabisa maana ukiangalia hata historia ya maraisi wanaochukua madaraka wakiwa vijana uongozi wao unakuwa ni mzuri sana mfano Kagame na Gaddaf waliochukua nchi wakiwa na umri wa chini ya miaka 30.
Badilikeni 2achane na ukaskazini wanachadema lasi ivo 2tarudi nyuma!
 
kura yangu ni kwa zitto kabwe.kumpa kura slaa labda awe kalani wa mahakama maana siwezi chagua mtu anayefanya kazi kwa kusikiliza majungu na kwa sasa anaendesha chama kwa nguvu ya mchumba wake josephine mshumbuzi.kumchagua slaa ni sawa na kuipa laana nchi yangu maana huyu mzee kila kitu kachelewa mpaka mapenzi kayajulia uzeeni

Magamba wote mliopiga kura hapa inajulikana mmempigia nani.Na laiti ingekuwa kura hii inapigwa na wanachadema tu Dr Slaa angepata 100%.Hizo chache alizoacha ni za wanachama wa Magamba kwa vile hii ni public Polls.Pia hiki ni kipimo tosha cha kumpata mgombea urais ajaye.....Lazima apitishwe yule ambaye tunajua ni adui wa magamba...
 
By Edubwee: sababu mbona nyingi, lakini jiulize we mwenyewe wao wamekwambia wanataka Urais au kugombea urais? nambie kijana!
 
Slaa akipitishwa uchaguzi mkuu chadema itashiriki tu na wala sio kushinda maana wanachadema hatumkubali wala nn afu kigezo cha umri hapo ndo mnakosea kabisa maana ukiangalia hata historia ya maraisi wanaochukua madaraka wakiwa vijana uongozi wao unakuwa ni mzuri sana mfano Kagame na Gaddaf waliochukua nchi wakiwa na umri wa chini ya miaka 30.
Badilikeni 2achane na ukaskazini wanachadema lasi ivo 2tarudi nyuma!

mfano wako ni mfu kabisa na sisi hatuangalii hiyo mifano unajua kagame na huyo gaddaf waliingia madarakani kwa njia gani? halafu ukisema wewe ni Chadema unakua mnafiki. all in all Zitto bado hafai hata kidogo kua raisi kwanza ni mbinafsi na anajiona yeye ni bora kuliko wenzake na mjuaji kwa kila kitu hata ndani ya CHADEMA yeye anafanya mambo kwa utashi wake hata kama Dr Slaa hatakiwi na watu kama wewe lakini Zitto ndio kabisa hafai mbele ya umma na asipoangalia kwa hali iliyopo atapotea tu kwenye siasa..... na kuna uwezekano hata jimbo la Kigoma Kaskazini akalipoteza likaenda hata CUF
 
kwanza huyo anayemfikiria tayari anatuhuma ya kula mlungula chadema hatuangalii umaarufu wa mtu,tunaangalia mtu safi.
 
1.dr. ana elimu ya kutosha na busara zilizosheheni kila kitu ni mtu anayejitoa haswa
2.dr. anauthubutu wa kufanya maamuzi magumu historia inaonyesha aliwahi kumshitaki polisi mpambe wa askofu wake kwa ufisadi wa kutumia kanisa kufanya biashara akiwa katibu wa maaskofu.
3.dr hana sura mbili
4.dr ni haina ya rais tunayemuhitaji kipindi hiki cha mpito nchi ikiwa imetuwama kwenye lindi la kifisadi na rushwa atakae tuvusha hapo si mwingine bali ni dr. na wengine wataiga kutoka hapo
 
Slaa kwa sasa TZ hana wa kulingana naye, baada ya slaa kuna mbowe, Makamu mwenyekiti CDM, lissu, mnyika ndo Zitto
 
Ni kweli ni kumdhalilisha Dr Slaa kumpambanisha na Mh Zitto Kabwe, na ninachokiona hapo juu ni mpambano wa CDM na Watu wasioitakia mema CDM na hawa ndo wanampa kiburi Mh Zitto hata akaonekana Anatumiwa na CCM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom