Kupotea taratibu kwa alama ya Kanisa Katoliki katika kupinga dhuluma

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Tangu kale, tangu enzi za manabii, Kanisa lilisimama katika ukweli, lilifundisha, lilikemea na kuwaonya watawala dhidi ya dhuluma. Mifano ipo mingi.

Muelekeo huo wa Kanisa uliwaongezea imani kubwa waumini, wasio waumini na hata watawala waliheshimu sana kauli za Kanisa kwa sababu waliamini kuwa wakati wote Kanisa lilisimama katika haki na ukweli ambao msingi wake mkubwa ni Kristo mwenyewe. Kristo, hata alipokuwa pekee yake dhidi ya maelfu ya wayahudi, aliendelea kusimama katika ukweli. Kuna maneno mawili ambayo yametokea mara nyingi katika biblia kuliko mengine yote. La kwanza ni upendo (mara 320) na la pili ni ukweli (mara 222).

Kanisa Katoliki katika mataifa mengi liliweza kuwasemea wanaodhulumiwa, na hata hapa kwetu, wakati TEC ilipokuwa ikiongozwa na baadhi ya viongozi (Rais wa TEC), kanisa lilikuwa na msimamo na kauli zilizo thabiti kwa watawala dhidi ya dhuluma.

Kanisa Katoliki lilianza kuwa kimya kabisa, na kwa namna fulani kuonekana kubariki matendo ya dhuluma kama vile kupotezwa watu, kutekwa, kuuawa, kubambikiwa watu kesi tangu TEC iliporidhia kumchagua kiongozi wake mwenye mahusiano ya karibu na watawala, eti kwaajili ya kupunguza tension kati ya Serikali na Kanisa. Kanisa limeondoka kutoka kwenye jukumu lake la msingi la kuwa sauti ya wasio na sauti wanapoonewa, mpaka kuwa mwandani wa Serikali hata pale serikali inapofanya dhuluma. Hali hii inaendelea kudhoofisha sana imani yetu kwa kanisa la Kristo na viongozi waliostahili kuyaishi maandiko.

Kuhusu haki za wananchi, Kanisa la Ulimwengu linasema yafuatayo:

The dignity of human life

Christians believe that all human life is sacred, unique and God-given. They also believe that all humans are made in the image of God.

Then God said, “Let us make mankind in our image, in our likeness, so that they may rule over the fish in the sea and the birds in the sky, over the livestock and all the wild animals, and over all the creatures that move along the ground.Genesis 1:26-27

Christians believe this to mean that many of the characteristics of God are reflected in humans. As a result, Christians believe that all human life should be treated with respect and dignity.

The belief that all humans are special can be seen in a document known as The Universal Declaration of Human Rights, which sets out all the different rights that every human should be entitled to.

As a result of the belief that all human life is special and God-given, Christians will try to do all they can to promote human rights. Human rights refer to the basic freedoms and rights of every human being in the world. Christians do this in many different ways including supporting charities such as Amnesty International who campaign for human rights.

Kanisa Katoliki la Tanzania, kwa kutokemea matendo yasiyo ya haki, limeendelea kuwa sehemu ya familia ya wakatoliki Duniani au limejitenga na jamii nyingine za wakatoliki?
 
Sasa kama anayetawaliwa kwa dhulma anaona sawa,kanisa lifanyeje sasa ndugu yangu? Wanaopaswa kusimama kwa dhati haswa ni wananchi
Ni kweli. Kuna wajibu wa kila mwananchi na muumini katika kupinga dhuluma. Tunapofanya hivyo tinatekeleza wajibu wetu kama raia na kwa upande mwingine kama waumini. Lakini Kanisa linatakiwa kuweka kauli yake thabiti. Kanisa siyo jeshi, siyo mahakama ya Duniani. Haliwezi kuadhibu na hata kuzuia wanachotaka watawala, lakini msimamo unaoegemea ukweli, unatakiwa kuwa wazi na thabiti.
 
Hii nchi ngumu sana kaka 🤣 🤣 🤣 . Mwaka jana RC lilisimama kidete dhidi ya serikali kwenye masuala ya CORONA,angalia jinsi wananchi walivyoliponda na kulishambulia kwa kuliita kanisa la shetani lisilokuiwa na imani-Hii inchi imejaa majimaji warriors wengi mnooo,kuwabadilisha ni kazi ngumu sana.
 
... Kanisa Katoliki lilianza kuwa kimya kabisa, na kwa namna fulani kuonekana kubariki matendo ya dhuluma kama vile kupotezwa watu, kutekwa, kuuawa, kubambikiwa watu kesi tangu TEC iliporidhia kumchagua kiongozi wake mwenye mahusiano ya karibu na watawala, eti kwaajili ya kupunguza tension kati ya Serikali na Kanisa. Kanisa limeondoka kutoka kwenye jukumu lake la msingi la kuwa sauti ya wasio na sauti wanapoonewa, mpaka kuwa mwandani wa Serikali hata pale serikali inapofanya dhuluma. Hali hii inaendelea kudhoofisha sana imani yetu kwa kanisa la Kristo na viongozi waliostahili kuyaishi maandiko.

Kanisa Katoliki la Tanzania, kwa kutokemea matendo yasiyo ya haki, limeendelea kuwa sehemu ya familia ya wakatoliki Duniani au limejitenga na jamii nyingine za wakatoliki?
Soma huu ujumbe wa Kwaresma 2018, tena katikati ya utawala wa hayati JPM, halafu urudi tena kusema kama hayo uliyoandika ni halisi ama la. Kama utaweza, soma document yote, kama unaona ni ndefu, basi walau soma Sura ya Tatu

Attachments

  • Ujumbe wa Kwaresima 2018.pdf
    10 MB · Views: 8
Hii nchi ngumu sana kaka .Mwaka jana RC lilisimama kidete dhidi ya serikali kwenye masuala ya CORONA,angalia jinsi wananchi walivyoliponda na kulishambulia kwa kuliita kanisa la shetani lisilokuiwa na imani-Hii inchi imejaa majimaji warriors wengi mnooo,kuwabadilisha ni kazi ngumu sana
Upo sahihi. Lakini Kanisa lisikate tamaa katika kuunena ukweli. Ukweli siku zote husimama.
 
Soma huu ujumbe wa Kwaresma 2018, tena katikati ya utawala wa hayati JPM, halafu urudi tena kusema kama hayo uliyoandika ni halisi ama la. Kama utaweza, soma document yote, kama unaona ni ndefu, basi walau soma Sura ya Tatu

Nashukuru. Kuna mengine yanapita bila ya kuyafuatilia. Na hasa kutokana na uminywaji wa vyombo vya habari.

Pale ambapo sipo sahihi, nisamehewe maana sikuwa na dhamira mbaya. Haya niliyoyandika, yanasemwa na wengi au baadhi ya waumini. Yawezekana ni kutokana na njia za upashanaji habari ziliminywa sana wakati wa awamu ya 5.

Kanisa liangalie namna ya kuhakikisha ujumbe wake unawafikia waumini wake kama vile, waraka ukitolewa, basi iwe lazima kuusoma ujumbe huo kwenye makanisa yote na jumuia ndogondogo, na baada ya kuusoma, kuwe na ufafanuzi ili ujumbe uwafikie waumini kwa usahihi.
 
Tangu kale, tangu enzi za manabii, Kanisa Katoliki lilisimama katika ukweli, lilifundisha, lilikemea na kuwaonya watawala dhidi ya dhuluma. Mifano ipo mingi.

Muelekeo huo wa Kanisa uliwaongezea imani kubwa waumini, wasio waumini na hata watawala waliheshimu sana kauli za Kanisa kwa sababu waliamini kuwa wakati wote Kanisa lilisimama katika haki na ukweli ambao msingi wake mkubwa ni Kristo mwenyewe. Kristo, hata alipokuwa pekee yake dhidi ya maelfu ya wayahudi, aliendelea kusimama katika ukweli. Kuna maneno mawili ambayo yametokea mara nyingi katika biblia kuliko mengine yote. La kwanza ni upendo (mara 320) na la pili ni ukweli (mara 222).

Kanisa Katoliki katika mataifa mengi liliweza kuwasemea wanaodhulumiwa, na hata hapa kwetu, wakati TEC ilipokuwa ikiongozwa na baadhi ya viongozi (Rais wa TEC), kanisa lilikuwa na msimamo na kauli zilizo thabiti kwa watawala dhidi ya dhuluma.

Kanisa Katoliki lilianza kuwa kimya kabisa, na kwa namna fulani kuonekana kubariki matendo ya dhuluma kama vile kupotezwa watu, kutekwa, kuuawa, kubambikiwa watu kesi tangu TEC iliporidhia kumchagua kiongozi wake mwenye mahusiano ya karibu na watawala, eti kwaajili ya kupunguza tension kati ya Serikali na Kanisa. Kanisa limeondoka kutoka kwenye jukumu lake la msingi la kuwa sauti ya wasio na sauti wanapoonewa, mpaka kuwa mwandani wa Serikali hata pale serikali inapofanya dhuluma. Hali hii inaendelea kudhoofisha sana imani yetu kwa kanisa la Kristo na viongozi waliostahili kuyaishi maandiko.

Kuhusu haki za wananchi, Kanisa la Ulimwengu linasema yafuatayo:

The dignity of human life

Christians believe that all human life is sacred, unique and God-given. They also believe that all humans are made in the image of God.

Then God said, “Let us make mankind in our image, in our likeness, so that they may rule over the fish in the sea and the birds in the sky, over the livestock and all the wild animals, and over all the creatures that move along the ground.Genesis 1:26-27

Christians believe this to mean that many of the characteristics of God are reflected in humans. As a result, Christians believe that all human life should be treated with respect and dignity.

The belief that all humans are special can be seen in a document known as The Universal Declaration of Human Rights, which sets out all the different rights that every human should be entitled to.

As a result of the belief that all human life is special and God-given, Christians will try to do all they can to promote human rights. Human rights refer to the basic freedoms and rights of every human being in the world. Christians do this in many different ways including supporting charities such as Amnesty International who campaign for human rights.

Kanisa Katoliki la Tanzania, kwa kutokemea matendo yasiyo ya haki, limeendelea kuwa sehemu ya familia ya wakatoliki Duniani au limejitenga na jamii nyingine za wakatoliki?
Rais wa tec wa sasa ni kibaraka wa watawala, ameshusha hadhi ya kanisa. Angalia mfano huko drc kanisa linavyosimama na wanyonge dhidi ya watawala dhalimu
 
Ni kweli kanisa langu limefeli sana. Hasa kwenye kuhimiza demokrasia. Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 likituli kimyaaa na kufuatia na uchaguzi mkuu 2020. Hata kusema kupita bila kupingwa ni makosa, wao kimyaaaaa. Ila baadhi ya mapadree waliunga mkono juhudi
 
Sasa kama anayetawaliwa kwa dhulma anaona sawa,kanisa lifanyeje sasa ndugu yangu? Wanaopaswa kusimama kwa dhati haswa ni wananchi
Na hatupo tayari kusemewa sasa sisi tunalalama pembeni wakija tunawshangila wacha Kanisa lisepe zake na mambo yake ya Kikanisa, sisi tudungweeee mpaka tukome.
 
Tangu kale, tangu enzi za manabii, Kanisa Katoliki lilisimama katika ukweli, lilifundisha, lilikemea na kuwaonya watawala dhidi ya dhuluma. Mifano ipo mingi.

Muelekeo huo wa Kanisa uliwaongezea imani kubwa waumini, wasio waumini na hata watawala waliheshimu sana kauli za Kanisa kwa sababu waliamini kuwa wakati wote Kanisa lilisimama katika haki na ukweli ambao msingi wake mkubwa ni Kristo mwenyewe. Kristo, hata alipokuwa pekee yake dhidi ya maelfu ya wayahudi, aliendelea kusimama katika ukweli. Kuna maneno mawili ambayo yametokea mara nyingi katika biblia kuliko mengine yote. La kwanza ni upendo (mara 320) na la pili ni ukweli (mara 222).

Kanisa Katoliki katika mataifa mengi liliweza kuwasemea wanaodhulumiwa, na hata hapa kwetu, wakati TEC ilipokuwa ikiongozwa na baadhi ya viongozi (Rais wa TEC), kanisa lilikuwa na msimamo na kauli zilizo thabiti kwa watawala dhidi ya dhuluma.

Kanisa Katoliki lilianza kuwa kimya kabisa, na kwa namna fulani kuonekana kubariki matendo ya dhuluma kama vile kupotezwa watu, kutekwa, kuuawa, kubambikiwa watu kesi tangu TEC iliporidhia kumchagua kiongozi wake mwenye mahusiano ya karibu na watawala, eti kwaajili ya kupunguza tension kati ya Serikali na Kanisa. Kanisa limeondoka kutoka kwenye jukumu lake la msingi la kuwa sauti ya wasio na sauti wanapoonewa, mpaka kuwa mwandani wa Serikali hata pale serikali inapofanya dhuluma. Hali hii inaendelea kudhoofisha sana imani yetu kwa kanisa la Kristo na viongozi waliostahili kuyaishi maandiko.

Kuhusu haki za wananchi, Kanisa la Ulimwengu linasema yafuatayo:

The dignity of human life

Christians believe that all human life is sacred, unique and God-given. They also believe that all humans are made in the image of God.

Then God said, “Let us make mankind in our image, in our likeness, so that they may rule over the fish in the sea and the birds in the sky, over the livestock and all the wild animals, and over all the creatures that move along the ground.Genesis 1:26-27

Christians believe this to mean that many of the characteristics of God are reflected in humans. As a result, Christians believe that all human life should be treated with respect and dignity.

The belief that all humans are special can be seen in a document known as The Universal Declaration of Human Rights, which sets out all the different rights that every human should be entitled to.

As a result of the belief that all human life is special and God-given, Christians will try to do all they can to promote human rights. Human rights refer to the basic freedoms and rights of every human being in the world. Christians do this in many different ways including supporting charities such as Amnesty International who campaign for human rights.

Kanisa Katoliki la Tanzania, kwa kutokemea matendo yasiyo ya haki, limeendelea kuwa sehemu ya familia ya wakatoliki Duniani au limejitenga na jamii nyingine za wakatoliki?
Ila kwa sasa sababu ya Rais wa Nchi hii ni Muislam utalisikia kanisa likikemea na kutoa waraka kama upendavyo
 
RC limekuwa ovyo kabisa..
Mimi ni muumini wake lakini lazima niseme ukweli RC limepotea kabisa na Viongozi wetu wa Kanisa hapa Tz wamekuwa ovyo kabisa.
Presented too general. Afadhali mleta mada alikuwa specific katika maeneo aliyokuwa ameyaona hayakukaa vizuri. By the way, kuna mikutano ya kawaida na mikuu katika Halmashauri ya walei, kama wewe kweli ni Mkatoliki, basi una mwakilishi katika mikutano hiyo, na kama haumjui, basi hiyo ni kutokana na kutoshiriki kwako, na pengine unadhani ukienda kanisani jumapili unakuwa umemaliza. Kuna watu wengi tu wa dizaini yako, kazi yao kubwa ni kulalamika, lakini kumbe hata jumuiyani hawaendi na hawajui kinachoendelea!
 
Back
Top Bottom