Kupotea bila kujijua

Kupotea bila kujijua

Hili suala la kupotea unapopafahamu sio jipya baba yangu limemtokea mwaka juzi alipokua anarudi nyumbani saa 2 usiku alijikuta haelewi anakokwenda aliishia kuzunguka mtaa tangu saa 2 usiku hadi saa 4 usiku bahati nzuri kuna jirani alipishana naye mara 3 hiyo ya mwisho alishindwa alimuuliza anatafuta nini alimjibu anaenda nyumbani akamuambia mbona nyumbani kwako pale na fahamu zikamrejea ila kikwetu wanasema ni mdudu sio majani ingawa haswa matatizo haya yanatokea kipindi cha masika
Baba yako ana umri gani?

Mara ya mwisho kufanyiwa check up iliyojumuisha tests za cognitive ability ni lini na zilitoa matokeo gani (kama alifanya).
 
Baba yako ana umri gani?

Mara ya mwisho kufanyiwa check up iliyojumuisha tests za cognitive ability ni lini na zilitoa matokeo gani (kama alifanya).
mkuu unajibu hoja kwa hoja..kudos. [HASHTAG]#GreatThinker[/HASHTAG]
 
Baba yako ana umri gani?

Mara ya mwisho kufanyiwa check up iliyojumuisha tests za cognitive ability ni lini na zilitoa matokeo gani (kama alifanya).
Ukijua sana muda mwingine ni matatizo, hivi unahisi alipagawa? Sikuwahi kumsikia kumtokea jambo hilo na lilitokea siku moja na halijamtokea tena. Kwenye hii dunia kuna mengine hutoyajua mpaka yakukute, naishia hapa.
 
mimi niliwahi potea huko Vijijin kwetu.
siku moja nilikuwa na wenzangu tukitoka kijiji kama cha 4 hv kutoka kijijini kwetu(tulienda kwenye zahanati ya kata kupata matubabu ya UTI). Basi wakat tunarudi si nkahis tumepotea. Yaani njia naijua ya kurudi home.. lkn kila nikiangalia huko mbele naona njia sio yenyewe,kule tunakotoka ndio naona kwenye njia ya kwenda home.,(nahis nilikanyaga hizo nyasi). wenzangu kila wakiniambia njia ni hii,mm naona kama tunarudi nyuma tulikotoka. ile nakaribia kukifikia kwenye kijiji chetu ndio akili inafunguka na kusema kweli huku ndio kwetu.

so toka siku hyo nikaamini kuwa hizo nyasi kweli zipo,na ukizikanyaga utapotea njian. hasa ukizingatia huko vijijin hakuna usafiri kama mijini. so wengi tulikuwa tunatembea kwa miguu ama kwa baiskeli.
sasa ndo ungekua hauko na hao wenzako .
pole sana mkuu
 
Katika kazi zangu huwa naenda sana mapolini muda mwingine unabeba GPS unaingia msituni kutafuta point ilipo, nimekuwa nikikutana sana na hizi stori huko vijijini unaweza kuchukua mtu akupeleke ila mnazunguka ukiuliza anasema pale kati kuna majani mabaya tunaweza kukesha polini
JAMANI mbona dunia ina mambo
 
Me imesha nitokea kama mara 2 hivi. Mara ya kwanza nilikuwa na bi mkubwa jioni moja tumetoka sokoni tunaelekea nyumbani sasa njia tunayoelekea kukawa na majani hivi na hayo majani yanasemekana yana macho mawili ukilikanyaga hilo jani basi ufahamu unapotea utajikuta unapitiliza unakokwenda, mimi na bi mkubwa tulijikuta tunakaribia kufika mwisho wa makazi ya watu ndipo akakumbuka kuwa huenda tumekanyaga hayo majani na dawa ya kurejesha fahamu kama upo na mtu unampiga mwenzako kofi la mgongoni ndipo unakuwa umerejesha fahamu. Siku ya pili nilikuwa mwenyewe polini aisee kapori ambaka sio kakubwa hauwezi amini nilimaliza siku nzima mpaka usiku ndo fahamu zinarudi
pole sana mkuu
 
Hizi ni zile hadithi za utotoni eti wamasai wakiaba ng'ombe wanageuza viatu vyao ili kuwa hadaa wanao fuatili muelekea wa nyayo zao. Sijui makanyagio ya hao ng'ombe walio ibiwa wali ya geuza je?
Labda walikuwa wanawabeba mgongoni.
 
Katika nchi ambayo access na afya ya akili ni ndogo, hata mtu akipotea kwa kuwa ana dementia au ugonjwa mwingine wa akili tutasema kakanyaga majani fulani.
Hivi mkuu Tangu umeanza maisha yako umegundua nini hadi sasa hivi?
 
Ukisema mambo yote yanawezekana ukiamini, hilo linajumuisha wale wanaoamini mambo yote hayawezekani katika kuamini.

Sentensi yako inajiachia kutafsirika kwamba vyote vinawezekana katika kuamini, hata vyote kutowezekana katika kuamini kunawezekana katika vyote vinavyowezekana katika kuamini.

Kwa kifupi, hujasema kitu.

Ukisema namba yoyote ni sawa na namba zote, hujatengeneza mfumo mzuri sana wa namba. Umepoteza maana ya namba yoyote.

Ukisema mambo yote yanawezekana katika kuamini, hujakuoaza kuamini kuwe juu.

Siyo tu umekuondokea kuamini maana.

Umeondoa maana ya maana, kabisaaa.
Kulalek
 
Hayo mambo yapo na yametokea sana vijijini huko;
Mvuha kuna kijiji kinaitwa magogoni 2005 kuna majamaa walikwenda kuwinda mbugani,wakat wanarud na mizigo yao ya nyama wakiwa jirani na kijiji wakatawanyika ili kupunguza msongamano wa watu maaana wakionekana watu kama10 harafu na mifurushi ya nyama watu watahamaki kidogo na km unavyojua maliasiri nao hawa chezi mbali.
Sasa ktk ule mtawanyo kwamb watakutana nyumban watu wamefika yule jmaaa bado hajafika,wakasubiria sana hawakumuona so ikabid watu walale kesho asubuh wakaanza kwenda kumfuatilia hawakufanikia walimtafuta kutwa nzima,wakarudi.
Siku ya pili inabid watafute ngoma ili wakipiga jamaa aweze kusikia walitoka pale saa kumi usiku jamaa walimkuta zaid ya km80,maaana walimkuta juu ya mti kabisa hata nguvu hana.
NB:HAYA MAMBO YAPO,ILA KWENYE USIBITISHO WA NN AMEKANYAGA HAPO HUONGELEKA VINGI,KUNA WANAOSEMA KUNA KADUDU UKIKAJAGA BAS NAWE UTATEMBEA TU,WENGINE HUSEMA MAJAN NA HATA WENGINE USEMA NDEGE,UKWELI WA SABABU HAMNA
ila mysterious yapo
 
Hizi habari nyingine zinaweza kuwa ni myths ambazo zinahitaji uchambuzi wa kifasihi.

Naweza kukuambia

Mboga ni mazao.

Kuchuma mboga ni kutafuta mazao. It is no coincidence kwamba kuna style ya kufanya mapenzi inaitwa "chuma mboga". Kwa maana nyingine ya lugha ya tafsida kutafuta kuzaa.

Mwanamke ambaye yupo kwenye siku zake hizo, ukitaka kutafuta mtoto (mazao, mboga) wakati wa siku hizo, zitanyauka tu (mimba haitashika). Uwezekano wa mwanamke kupata mimba akiwa katika siku zake ni mdogo sana.

Kwa hiyo, inawezekana watu wanaongea kitafsida mwanamke aliye katika siku zake asichume mboga, zitanyauka.

Ukisoma moja kwa moja unapata maana tofauti.

Ukitafsiri ki myth na tafsida unapata tafsiri tofauti.

Inanikumbusha Kunta Kinte katika tamthiliya ya "Roots". Alikuwa anamlalamikia Fiddler kwamba hana mbegu ya kupanda apate mazao (nafikiri alikuwa ana miss maembe ya kwao Gambia).

Fiddler alivyo muhuni akatafsiri vingine kabisa. Akamwambia Kunta, weee kijana mdogo bado. Mbegu unazo nyingi. Tafuta mwanamke tu.

Huo ndio ukawa mwanzo wa Kunta Kinte kuoa.

Naonesha tu sehemu nyingine pale mazao ya kilimo yalipolinganishwa na mazao kwa maana ya watoto.

The good thing (or bad thing if you are a Paul Dirac) with myths is that they are subject to interpretation.

Nimetoka kumaliza kijitabu cha Claude Levi-Stauss "Myth and Meaning: Cracking the Code of Culture".

A very interesting perspective. Especially for a skeptic.
Unadhani wewe ndie mwenye kufikiri na kuwaza zaidi ya wanajamii wengi kutoka maeneo tofauti ya nchi hii?!

Ama wewe ndo mnadadavuaji kwa mifano ya vitabu na nadharia za kusadikika kutoka kwa maandiko ya watu kama wewe?!

Wale waliokulia katikati ya milio ya bundi na ndege kwijo ndio wanaeza kukupa mifano ya matukio ya aina hiyo mana njia nyingi zitumikazo huko vijijini ni nyembamba na si ajabu kukuta majani yamejiotea.

Kama umewahi kujikunguta umande ahsubuhi ama wakati wa mvua kuisha huwezi kosa majani aina ya (Kisokoro)yakiwa yametanda njiani kwa kusambaa chini.

Kuna mengi yapo huko vijijini kuliko ngano chache zilizofika mjini

Nachelea kusema utaona uzushi ikiwa tu hata mbuzi hujawahi kwenda mfunga kwenye majani,namaanisha kama hujawahi kuishi maisha yale ya ndani ya zile jamii ambazo Radio tu ipo kwa mwenyekiti,sio hivi vijiji vilivyojaa taa za umeme.

zitto junior ,hearly, Da'Vinci
 
Me imesha nitokea kama mara 2 hivi. Mara ya kwanza nilikuwa na bi mkubwa jioni moja tumetoka sokoni tunaelekea nyumbani sasa njia tunayoelekea kukawa na majani hivi na hayo majani yanasemekana yana macho mawili ukilikanyaga hilo jani basi ufahamu unapotea utajikuta unapitiliza unakokwenda, mimi na bi mkubwa tulijikuta tunakaribia kufika mwisho wa makazi ya watu ndipo akakumbuka kuwa huenda tumekanyaga hayo majani na dawa ya kurejesha fahamu kama upo na mtu unampiga mwenzako kofi la mgongoni ndipo unakuwa umerejesha fahamu. Siku ya pili nilikuwa mwenyewe polini aisee kapori ambaka sio kakubwa hauwezi amini nilimaliza siku nzima mpaka usiku ndo fahamu zinarudi
Duuh!natamani initokee hii
 
Hili suala la kupotea unapopafahamu sio jipya baba yangu limemtokea mwaka juzi alipokua anarudi nyumbani saa 2 usiku alijikuta haelewi anakokwenda aliishia kuzunguka mtaa tangu saa 2 usiku hadi saa 4 usiku bahati nzuri kuna jirani alipishana naye mara 3 hiyo ya mwisho alishindwa alimuuliza anatafuta nini alimjibu anaenda nyumbani akamuambia mbona nyumbani kwako pale na fahamu zikamrejea ila kikwetu wanasema ni mdudu sio majani ingawa haswa matatizo haya yanatokea kipindi cha masika
hata mama namuuliza hapa anasema kipindi cha masika. na mvua iliwanyeshea masaa ma5 ,walitembea mpaka mto fulani watu Masasi wanaujua unaitwa Myesi
 
Kama umekulia mjini na ukaishi mjini haya mambo utayasikia tu kama ni ngano flani hivi za kizamani,ama ukifika vijijini ukakutana na haya mambo utasema ni kwa sababu watu wa huko hawajastarabika ila sivyo ilivyo haya mambo yapo na tunayaishi baadhi yetu hasa tuliozaliwa na kukulia vijijini na elimu zetu kupatia huko huko vijijini tena kwa kutembea km kadhaa tukiwa peku.

Kama umewahi kung'oa kucha kisa huna viatu ama umewahi kushonewa mfuko wa kitambaa wenye kamba moja tu kwa sindano ya mkono kisha ukautumia kubebea daftari,basi huwezi kubishana na hili kabisa.

Kweli watalamu ukiwafikia wanaeza kukwambia maelezo mengi ya vitabuni ila bado ukweli utabaki palepale ya kuwa kuna mazingira ukiyafikia lazima utaathirika kwa namna moja ama nyingine.

Mfano ni mimi mwenyewe nimeyaishi sana mazingira haya,tangu nakuwa hadi nabalehe na kuja mjini kuhangaika bado mambo hayo yalikuwapo,kupotea tulishapotea sana iwe usiku ama mchana.

Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo tukiwa shule ya msingi tuliwahi kutoroka na kwenda kucheza kwenye pori la Mwitongo,yalipo makazi ya Nyerere na lengo lilikuwa ni kuona sehemu iliosadikika kuna makazi ya mizimu ya Nyerere na siku hiyo ilikuwa ni Alhamis ambayo wakazi wengi wa Butiama wanajua mzimu wa Nyerere hutoka kwenye makazi yake na kwenda kwa demu wake ambae nae ni mzimu yuko ng'ambo kidogo.

Hivyo tukalazimika kwenda siku hiyo ili kuona maajabu ya hilo eneo analoishi huyo mzimu

Tukiwa katikati ya msitu,nikiwa mbele mwenzangu nyuma,tukayavuka majani flani hivi na bila kujua tukazidi kwenda mbele,lakini azima yetu haikutimia na tukajikuta tukizunguka msitu bila uelekeo maalumu.

Baada ya jua kuzama,taarifa zikagfika kijijini ya kuwa tuliingia Mwitongo,hivyo wanakijiji wakaja kututafuta na tulikutwa yalipo mabaki ya ndege iliodondoka miaka kadhaa huko nyuma.

Mbali ya kuambiwa chanzo ni yale majani,lakini pia tukaambiwa mmoja kati yetu ni mtoto aliezaliwa pacha na sikuwa mimi alikuwa ni mwenzangu.

Tukaambiwa kwa kuwa ni wadogo mzimu umetuonea huruma mana hadi wakati unarudi sisi tulikuwa bado tunazurura mle.

Na kisa hiki ndo kilifanya Nyerere aombe kutuona (alikuwa bado yu hai)
Tulipelekwa na akatuuliza kwa nini tulienda msituni peke yetu?! Tukamwambia shida yetu na akatuchukua na kutupeleka hapo tulipohitaji kupaona.

Tukawa watoto wa kutolewa mfano kama sisi ni wajinga,wengine wakisema mashujaa na wengine wakiwaasa watoto wao wasituige sisi.

Huo ni mfano kati ya mifano mingi sana nilioshuhudia japo sehemu zingine hatukutakiwa kwenda na watoto waliozaliwa pacha ama wanawake waliomwezini ama kama umelala na mke wa mtu ama,umeiba cha mtu nk nk
Duuh
mlikiona kitu mbona
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom