Baada ya mimi kuondoka huku home ilikuwa hivi
Mama yangu alikuwa ni mfanyabiashara, na hiyo siku ndio alikuwa amerudi, hapo hatujaonana karibia miezi 3, nilikuwa nikiishi kwa babu na bibi mzaa mama,
Nilitafutwa kuanzia mida ya kula yaani saa 7, sikuonekana na sio kawaida yangu, sa 10 mida ya madrassa sikuonekana, saa 12, sikuonekana, wakaanza ingia wasiwasi, taarifa zikaanza kusambazwa kijijini kuwa mjukuu wa fulani haonekani, likapigwa mpaka lile la mgambo, kuna watu hawakulala wananitafuta, kesho yake, taarifa zikapelekwa kwenye vituo vya karibu vya polisi, mpaka mkoani watu wakaenda, ikapita, siku ya tatu ikabidi sasa watu waanze kuhisi pengine nilienda mtoni nimeliwa na mamba ama ndio mambo ya kuwekana misukule maana kijiji chetu uchawi ulikuwa si haba, ndipo babu akaamua waweke hitima basi udhia uishe, kwamba nimekufa