Kupotea bila kujijua

Hii ya majani ni kweli katika jamii niliokulia imetokea mara nyingi matukio kama hayo. Hata mama yangu mzazi aliwai kupotea lakin mara nyingi lazima ukutane na mtu anae kujua ndio anakushtua we fulani unaena wap huko unazinduka
Au geuza shati ulilovaa nje ndani, unarudisha ufahamu, anayepinga hili ndo hao walozaliwa Hindu Mandal sio makosa yao...
 
Dunia ina mengi na asilimia kubwa yetu tunajua 'punje' tu ya mambo yote.
 
Niliambiwa sijui nmekanyaga mdudu anaesababisha kupotea. Huko nilikopotelea waliniambia nigeuze shati, na kweli ilinichukua muda mfupi kufika home[emoji4][emoji4]
wengine wamesema eti unazabwa kofi zito la mgongoni unazinduka
 
Mim mawazo yangu nahisi ni imani potofu.
Kukanyaga mti flani kunahusiana na nin kupotea kwa mtu pengine tu kuna kitu nyuma ya hayo majani.
 
Sasa kama umeshindwa kumuamini Mama mzazi utamuamini nani tena humu?
 
Na hamukupewa katika elimu ila kiasi kidogo sana (qur an 17:85)

And they ask you, [O Muhammad], about the soul. Say, "The soul is of the affair of my Lord. And mankind have not been given of knowledge except a little."
 
Hiyo tuliopitia maisha ya kijijini imeshatutokea,

Mimi nilikua na rafiki yangu tukaenda kuzulula porini huko tukapotea tukawa tunaelekea tusipopajua nikamuiliza mwenzangu tunaenda wapi, akanijibu ye mwenyewe hajui, tukasema hapa tayari tumesharuka mdudu,

Tukabadilisha nguo, tulikuwa tumevaa kaptula ikabidi tuzigeuze chini juu...juu chini kisha tukatembea kama dakika tano hivi ile kutokea njiani tu vichwa vikakaa sawa, tukavaa kawaida huku kila mmoja akijiwazia jome atajitetea vipi
 
bahati yenu mngelala huko
 
Haya mambo yako miaka fulani hiv kuna mzee mmoja alikuwa na hii michezo.yaan anachokifanya anakuuliza haswa wale wageni kuwa anapajua stand automatically mgeni anaijua stand vile unamuelekeza pita njia hii anakwita njoo unioneshe ila unaenda ndo basi unakuwa unamfata yeye anakupeleka ambapo wewe haupafahamu.kupona kwako atokee mtu anayekufahamu akikwita tu unastuka na ufahamu wako unaludi.ila ya mungu mengi alikufaga yule mzee.
 
Mimi nafahamu ya mdudu anaekua kama ana taa ,usiku hung’aa kwa namna anavyoonekana,
Wanasema ukimkanyaga bila kujua utapuyanga saana na hadi ukutane na anaekufahamu ndipo fahamu zinakurudia
 
Paul dirac bwege tu, alicopy idea ya quantum electrodynamics
 
Paul dirac bwege tu, alicopy idea ya quantum electrodynamics
Ali copy idea gani, wapi, lini, vipi, kwa ushahidi gani, wewe umejuaje hilo, umehakiki vipi?

Umesoma kitabu gani cha maisha ya Dirac ku conclude kwamba ni bwege?

Unajua kwamba equations za Dirac zinatumika kufundishia mpaka leo, huyo bwege gani anatumika kufundisha mpaka leo?

Wewe equations zako zinafundishia wapi?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…