Kupita bila kupingwa - is this democracy too?

Look at this one!

Tukio la kuenguliwa kwa mgombea wa Chadema kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo la Songwe ndio lililotawala vituko vilivyojitokeza wakati wagombea wa nafasi hizo wakirejesha fomu.

Utata wa mgombea wa Chadema ulijitokeza baada ya ofisi ya makao makuu ya chama hicho kutengua uteuzi wa awali wa Habel Mwaniyonde na kutaka nafasi hiyo igombewe na Paul Ntwina.

Msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Chunya, Maurice Saponya aligoma kumpa fomu Ntwina akitaka arudishiwe fomu aliyoitoa awali kwa Mwaniyonde.

Agosti 13 ofisi ya Chadema ya wilaya ilimthibitisha Mwaniyonde kuwa mgombea Jimbo la Songwe na alichukua fomu. lakini leo asubuhi (jana), nilipokea barua iliyosaniwa na Dk Slaa ikisema kuwa wametengua uamuzi wa Mwaniyonde na nafasi yake apewe Ntwina," alisema msimamizi huyo.

Nikawaambia ni sawa, lakini ili kuepusha mgogoro waniletee fomu ya kwanza ili nisiwe na fomu mbili nikaja kuaibika.
 
Mchezo wa kununua wagombea wa upinzani ulikuwepo sana siku za nyuma mfano mwaka 2005 aliyekuwa mgombea waCUF jimbo la serengeti MOSSENA NYAMBABE alisema kuwa aliambiwa na mgombea wa CCM <wanyancha>kuwa akubali kuchukua milion 50 then amwachie jimbo lakini mgombea yule alikataa na hatimaye inakadiriwa wanyancha alitumia zaidi ya million 300 katika uchaguzi ule kuhonga na kucheza rafu nyingine kushinda, katika jimbo la MUSOMA mjini MATHAYO MANYINYI alitumia kiasi cha 700 million kushinda mpaka leo kesi yake ya wizi wa kura haijaisha, mchezo wa kununua wagombea upo sana ukitaka nenda kagombee kwa MKONO utaitwa ili upozwe.
 
Look at this one!

Tukio la kuenguliwa kwa mgombea wa Chadema kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo la Songwe ndio lililotawala vituko vilivyojitokeza wakati wagombea wa nafasi hizo wakirejesha fomu.

Utata wa mgombea wa Chadema ulijitokeza baada ya ofisi ya makao makuu ya chama hicho kutengua uteuzi wa awali wa Habel Mwaniyonde na kutaka nafasi hiyo igombewe na Paul Ntwina.

Msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Chunya, Maurice Saponya aligoma kumpa fomu Ntwina akitaka arudishiwe fomu aliyoitoa awali kwa Mwaniyonde.

"Agosti 13 ofisi ya Chadema ya wilaya ilimthibitisha Mwaniyonde kuwa mgombea Jimbo la Songwe na alichukua fomu. lakini leo asubuhi (jana), nilipokea barua iliyosaniwa na Dk Slaa ikisema kuwa wametengua uamuzi wa Mwaniyonde na nafasi yake apewe Ntwina," alisema msimamizi huyo.

"Nikawaambia ni sawa, lakini ili kuepusha mgogoro waniletee fomu ya kwanza ili nisiwe na fomu mbili nikaja kuaibika.''

Hili ni tatizo la kutofanya mawasiliano kwa wakati na kuchukulia maswala kirahisi au kijuujuu! Na litawa-cost sana! Jamani Siasa na taratibu zake ni muhimu kuzingatiwa kwa umakini wa hali ya juu! Uteuzi wa kufanyika kwenye simu una mashaka mengi bandugu! Hapa washirika hizo buti mnavaa ni muhimu kuzikaza ile mbaya! Hili ni moja...mpaka kampeni ziishe msipokuwa waangalifu hao wagombea wote mnatamba nao watakuwa wamepukutishwa woooooote! Maneno ya ...tulifikiri....tulijua...there is nothing like obvious when it comes to sheria na taratibu!
 
Hi si sawawa wala si demokrasia. hata mi wazo hili limenisumbua na linanikera sana. watanzania tubadilike upinzani unahitajika
 
Angalizo kidogo tu mkuu. Hizo reds (lower cases) ni redundant. Upper case ( 's ) ina-miss. Jukwaa la wachunguzi hili naogopa tusije tukawaboa!

Wewe ni zero kabisa!! Yaani unataka kuniambia kwenye 'American politics' kunatakiwa kuwe na apostrophe kwenye American na iwe "American's politcs"? You can't be serious.
 
Hi si sawawa wala si demokrasia. hata mi wazo hili limenisumbua na linanikera sana. watanzania tubadilike upinzani unahitajika

Wapinzani hakuna kitu!wengi wapo JF na keyboards!Washabiki wa Upinzani hapa sawa sawa na aliyekuwa Waziri wa Habari wa Iraq Al sahaf aliyekuwa waziri wa Sadam Hussein ,wanajeshi wa Marekani wameshaingia Baghdad yeye anajigamba tutawamaliza wamerakni mpaka akakimbia,hapa JF usanii mtupu oooh ccm safari hii watakoma JK hamna kitu !Tayari ccm wameshapata Viti zaifi ya kumi bila upinzani kata zaidi 100 ,kampeni hazijaanza anza hapo !Tusubirie 31 Oct
 
MWENYEKITI Mwenza wa Taasisi ya Utafiti ya Demokrasia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Redet), Dk Benson Bana amesema hatua ya kujitokeza kwa mgombea wa chama kimoja kupita bila kupingwa ni kudumaza demokrasia na sio jambo la kujivunia katika nchi yenye mfumo wa vyama vingi.

"Hili sio suala la kujivunia katika demokrasia ya vyama vingi," alisema Dk Bana na kutoa mwito kwa vyama vya siasa kuhakikisha vinajiimarisha ili viwafikie wananchi walio wengi zaidi.

Hata hivyo alikiri uwezekano wa kuwepo wagombea wanaokubalika na kusema kuwa anatambua kuwa sauti ya wengi ndio sauti ya demokrasia na kwamba yawezekana kuna wagombea baadhi ambao wamepita bila kupingwa kutokana na kukubalika kwao katika jimbo na kwa wananchi wa eneo husika.

Lakini pia aliweka shaka kwa baadhi kwa kutoa ushauri kwa vyombo vya dola, ikiwemo Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kufuatilia kama hao waliopita bila kupingwa hawatumii ushawishi au mbinu chafu.

Alisema haitoshi kwa jamii kuridhika kuwa wagombea hao wa CCM wamepita bila kupingwa bila kufanyika kwa uchunguzi wowote.

"Siwezi kusema kuwa wametumia rushwa kwa vile sina ushahidi, lakini kuna haja ya Takukuru kufuatilia suala hili kwa kina, kujua mazingira ya mgombea kubaki peke yake," alisema msomi huyo ambaye taasisi yake imekuwa ikitoa utabiri wa matokeo ya utafiti unaokaribiana na ukweli.

"Hili linawahusu Takukuru na vyombo vingine vya dola, mgombea anapita bila kupingwa kwa sababu gani, yawezekana kuna mizengwe inayomfanya mtu ajiondoe," alisema Dk Bana.

Hadi sasa CCM ina jumla ya wabunge 17 waliopita bila kupingwa.

Habari Leo.
 
Nilikuwa nasoma kuhusu January Makamba kurudisha fomu peke yake na Moe Dewji kupita bila kupingwa, nikawa nafikiri hivi hivi.
 
Mi kilichonishangaza zaidi ni pale zaidi ya wapinzani watano wa Nimrod Mkono kujitoa (baada ya kurudisha form), kwa wakati mmoja na sababu zinazofanana!
 
Mi kilichonishangaza zaidi ni pale zaidi ya wapinzani watano wa Nimrod Mkono kujitoa (baada ya kurudisha form), kwa wakati mmoja na sababu zinazofanana!

Wameishapewa fungu lao na kuona bora ndege mmoja mkononi kuliko kumi walio porini ( a bird in hand is worth ten in the bush!)!
 
Siasa ni mchezo mchafu.Mbinu kila aina zinatumika za wazi na siri.Kupita bila kupingwa si jambo zuri kwa ustawi wa demokrasia lakini ikiwa watu wenye hadhi hawakujitokeza kutoa ushindani,yule aliyebaki anakuwa ni mshindi halali.

Na wapinzani wanakuwa kama wamelala doro vile,hawana matayarisho ya maana katika kupanga mikakati yao,siju wana mapungufu gani..?
 
Habari kuwa baadhi ya wagombea ubunge kwenye baadhi ya majimbo kuwa wamepita bila kupingwa zimenishangaza na kiasi fulani kunichukiza pia. Kwa mtazamo wangu tunapozungumzia demokrasia sitarajii katika karne hii mtu mwenye akili timamu akadai eti mgombea fulani amepita bila kupingwa. Kiukweli ni njia ya kudumaza demokrasia na sijui kwa mwendo huu kama nchii hii tutafikia hatua ya kukomaza demokrasia....Lawrence Masha, Bernard Membe na wengine inadaiwa wamepita bila kupingwa katika majimbo yao hivyo wanasubiri kuapishwa tu.....Kweli????????????:ballchain::ballchain::ballchain:
 
Labda niseme ni kweli kwani ndivyo ilivyo. Ila hayo yote yanatokea kwasababu zifuatazo:
  1. Tume ya uchaguzi na wasimamizi wake si huru.
  2. CCM inatumia vyombo vyake vya dola kudumaza demokrasia ikidhani ni fahari kumbe inajiandalia TIMING BOMB!
  3. Angalia vyombo hivi; polisi, jeshi, taasisi za elimu ya juu, balozi zetu nje ya nchi, ofisi mbalimbali za serikali zote zina-ikampenia CCM.
  4. Leo hii yapo matawi ya CCM kwenye vyuo karibu vyote vya elimu ya juu, na wakuu wa hivyo vyuo wako salama kabisa. Je, vp kama CHADEMA ikifungua matawi kwenye vyuo hivyo hivyo unadhani ni rahisi?
  5. Ndo maana hata wale wanachama wa vyama vingine wanapojitokeza kugombea dhidi ya wale wa CCM vitisho, hujuma na uonevu wa kila namna vinafanyika dhidi yao. Mfano jimbo la Nyamagana Mwanza, jinsi Masha alivyokuwa akimpigia mgombea wa CHADEMA simu za vitisho. Huu ni mfano mmoja lakini iko mingi kweli kweli.
  6. .................
 
Domhome, Sijaelewe ni kwa kiasi gani watanzania tunaiangalia hii demokrasia hapa nchini. Vinginevyo ieleweke tu kuwa hii nchi ni ya chama kimoja. Kwani kwa jinsi hali ilivyo sidhani kama demokrasia itakuwepo pasipokuwa na vyama pinzani. Yote usemayo ni kweli tupu. Kinachonichekesha zaidi ni jinsi CCM inavyokesha kutafuta mbinu za kuuwa upinzani ili iendelee kuwaburuza wadanganyika....For sure time will tell...
 
Wapendwa jana nimesoma gazeto moja likitaja majina ya wabunge wateule ambao awana shida ya kupiga kelele kuomba kura moja wapo ni mama tibaijuka prof wetu
kwa kweli sina ubaya kukupongezakwa hili na mungu akubariki katk maisha haya mapya ya mjengoni tukumbuke hata kwenye udereva wa lile shangingi letu lijalo mzazi
 
Shukrani kwa kufungua macho wengi. Naamini barua hiyo itafungua wengi ufahamu wao kuhusu suala hilo kuliko kuendelea kujipigia makofi. Ni imani yangu kuwa tume ya uchaguzi itaizingatia. Thanks
 
Back
Top Bottom