Kupiga na kutesa wanyama wasio na hatia wala akili ni kiashiria moja wapo cha kuwa na upungufu wa akili (Mbwiga)

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Na ni hasa kwa jamii nyingi za kiafrika, mtu unakuta tu anapenda kuwatesa wanyaa na kuwadharau, ni mtu huyp huyo hujivika unafiki wa kwenda kanisani / msikitini wakati hutesa viumbe vya Muumba

Ng'ombe anayechelewesha msafara yuko mbele lakini unakuta mtu anamtia bakora ng'ombe wa nyuma aliyezuiwa na wa mbele, huko ni kukosa akili

Mbwa anajipitia zake hana habari na wewe, unaanza kumtupia mawe, una dalili ya uchizi.

Paka anapita zake hana habari na wewe, unaanza kumfukuza na kumtukana, una utindio wa ubongo.

Mbwa unaishi nae lakini humuogeshi na banda lake ni chafu hujali usafi wake, wewe ni Mbwiga.

Kuku umemnunue kumchinja humpi hata maji wewe wawaza kusali tu kabla hujamla, wewe ni mluga luga

Paka ama mbwa kala chakula ulichokiacha wazi, ndivyo alivyoumbwa, wewe waanza kumpiga, si ajabu siku moja utamkata kiganja mtoto asiejitambua kisa kakinyea.
 
FB_IMG_16947575703832409.jpg
 
Ukatili wa Wanyama: Jamaa Mlebanoni(Mwaarabu) Paka awekwa ndani ya Oven
Animal Cruelty Put cat in microwave

Pia, kuna Video zingine utaziona Wazungu, Waarabu, Wahindi wakitesa na wakitesa Wanyama nchini Mwao.

View: https://m.youtube.com/watch?v=106eEsiU5kI&pp=ygUYQW5pbWFsIGNydWVsdHkgaW4gZXVyb3Bl

View: https://m.youtube.com/watch?v=TdCny5EennI
===================

View: https://m.youtube.com/watch?v=K7XzvfwwNT4

Suala la kutesa Wanyama sio la Watanzania au Waafrika peke yao. Tukiondoa lengo zima la kutoa elimu juu ya Ukatili wa Wanyama, mleta mada hakupaswa kuwashambulia Watanzania au Waafrika. Uwasilishaji wake umekaa kutukana, kudhalilisha na kusimanga Watanzania. Ukemewe.
 
Kuna watu niliwakuta wamebesha punda magunia ya mkaa huku punda wana vidonda migongoni mwao, haitoshi wanawachapa fimbo. Niliwapiga mkwara mzito kuwa nitawashitaki mahakamani kwa kuwatesa wamyama. Nilitoa onyo kali wakawatibu majeraha haraka sana iwezekanavyo na wawe wanawawekea sponji migongoni mwao wanapowabebesha mizigo
 
Endelea na moyo huo. Punda wa Tanzania wanahitaji mtetezi
 
Na ni hasa kwa jamii nyingi za kiafrika, mtu unakuta tu anapenda kuwatesa wanyaa na kuwadharau, ni mtu huyp huyo hujivika unafiki wa kwenda kanisani / msikitini wakati hutesa viumbe vya Muumba

Mbwa anajipitia zake hana habari na wewe, unaanza kumtupia mawe, una dalili ya uchizi.

Paka anapita zake hana habari na wewe, unaanza kumfukuza na kumtukana, una utindio wa ubongo.

Mbwa unaishi nae lakini humuogeshi na banda lake ni chafu hujali usafi wake, wewe ni Mbwiga.
Ng'ombe anayechelewesha msafara yuko mbele lakini unakuta mtu anamtia bakora ng'ombe wa nyuma aliyezuiwa na wa mbele
 
Sheria ya kulinda wanyama ilikuwapo tangu Enzi za mkoloni na ndio alieleta sheria hiyo
Mzee wangu alikuwa na mamlaka hayo ya kuwakamata mpaka wanaobeba kuku vichwa chini na kuwapeleka kituoni kulipa faini
Hiyo miaka ya nyuma wakati tulikuwa na utu

Kuna siku nilimuona jamaa anampiga punda sana huku akivuta tela lililojaa matikiti
Nilimfokea sana nikamuambia hayo matikiti ungeweza kuyabebe kichwani? Na je huyu Punda si ndio anaekuingizia riziki na unapeleka mboga nyumbani? Sasa kwa nini umpire na hata maji hujampa siku nzima

Siku nyingine unatoka kijijini hakikisha umemkatia majani ya kula na dumu la maji sawa
Maana ndie anaekulisha
Alihuzunika sana na kujiona jahili na kuomba samahani

Tujaribu kuwaelimisha pindi tunapowqona wanatesa viumbe
Na sio Tz tu ni Dunia nzima wapo watesaji mpaka wale wa sarakasi wanaotumia majoka na nyani na hata Dubu

Wafugaji wabaya wapo pia kwa kuwatesa ng'ombe kisa kala mahindi au anatembea polepole wakemeeni sana
 
Hata kumpigq MWANAMKE ni tatizo maana na yeye anafall kwenye hilo kundi.

Tusiwapige hawa watu.
 
Back
Top Bottom