Paul mathew
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 275
- 60
- Thread starter
- #21
Nivea NAKUSHUKURU SANA KWA WARAKA WAKO Leo nikirud nyumbani nalianzisha darasa. Asante sana
mambo haya bana.....sasa kwa nini....?....khaa!!...
ka! Coments zingine bana, wakati namuoa mbona niliqualify iweje leo sina qualification?kama unabembeleza kama unaomba emplyment na unanyimwa basi hau-qualify kwenye hiyo position!!!:bange:
Hahahahaaaaa!!!............pole sana, katafute kazi inayokufaaa.........!!!!:happy:
[h=2]Re: Kupewa mara moja tu kwa mwezi.[/h]Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.1. Je, ninajenga nyumba yangu au naibomoa?
2. Je, ninawekeza kwenye ndoa yangu? Natumia uwezo wangu kuiboresha?
3. Je, naonyesha kumthamini na kumjali mume wangu?
4. Je, natumia nguvu zangu na uwezo wangu kwa ajili ya familia yangu?
5. Je, natengeneza mazingira kwa maneno na matendo yangu yakumfanya mume wangu afurahie na kupenda kuwa nyumbani?
6. Je, naridhika na kuihudumia familia yangu?
7. Je, hisia zangu na upendo wangu ni kwa ajili ya mume wangu au mtu mwingine? Je, muonekano wangu, maneno mazuri na ushawishi mwema ni kwa ajili ya mume wangu au watu wengine?
8. Je, natimiza mahitaji ya mume wangu?
9. Je, ni mwaminifu kwa mume wangu? Nina uhusiano wowote wa siri ambao sitaki mume wangu ajue?
10. Je, mume wangu yupo huru kuwa muwazi kabisa kwangu hata kunikosoa?
11. Je, ninaruhusu mawazo ambayo siyo safi kuwa ndani yangu kupitia redio, televisheni au vitabu?
12. Je, nimekuwa kimbilio na faraja kwa mwanaume ambaye ndoa yake ina matatizo?
13. Je, natafuta ushauri na faraja kutoka kwa mwanaume mwingine (mchungaji, kiongozi wa kanisa, mshauri, mfanyakazi mwenzangu) na sio mume wangu kwanza?
14. Je, ninauhusiano wa karibu zaidi na mwanaume mwingine kuliko nilivyo na mume wangu?
15. Je, nimekuwa mkali na mwenye maneno yasiyo ya upole au ni mwenye maneno mazuri na yenye upole na unyenyekevu?
16. Je, naonekanaa rahisi rahisi kwa wanaume wengine au naonekana ni mtu mwenye msimamo? Je, naruhusu mizaha isiyofaa na watu wengine?
17. Je, kuna kitu katika mavazi yangu, muonekano au maongezi ambacho kinaweza kuwa kichocheo kwa wanaume kuwa na tamaa?
18. Je, ninavyoongea na wanaume kazini au popote naonyesha kuwa mimi ni mwanamke wa kristo au nakuwa nawaonyesha upendo na ukaribu wa kupitilizia ambao unapaswa uonyeshwe na wake zao?
19. Je, nimeweka mipaka katika mahusiano yangu na watu wa jinsia ya kiume? Ni mipaka gani hiyo?
20. Je, kuna mausiano niliyonayo ambayo yanaweza kuleta utata kwa watu?
21. Je, mume wangu na watu wengine wanao nifahamu wanaweza kusema kuwa mimi ni mwanamke mwenye busara na anayejiheshimu?
22. Je, nimeazimia moyoni mwangu kuwa safi mbele za Mungu? Je, ni mfano wa kuigwa na wanawake wengine wanaoishi maisha ya kumfuata Mungu?Mithali 31:10 Mke mwema, ni nani awezaye kumuona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
PRINT HII KARATASI MPELEKEE AJIBU MASWALI YOTE HAYO HAPO JUU TENA WEWE UKIMUULIZA MWENYEWE
Habari zenu wana jf, nimeoa na nina miaka 4 ya ndoa yangu, kadri siku zinavyokwenda napunguziwa dozi ya mapenz, zilizopita ilikuwa 5 mpaka 6 per month sasa hivi ni 1per month na anakua mkali yaani mpaka nibembeleze kama naomba employment ukipewa unaambiwa utapata tarehe kama hi next month nampenda sitaki kumsaliti naheshim ndoa yangu. Naombeni ushauri nifanyaje walau niongeze doz.
Pole sana Mtoa mada
Nadhani kuna tatizo kaeni chini muongee
Kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha.
mambo haya bana.....sasa kwa nini....?....khaa!!...
hahaha,anataka gangster love huyo,Habari zenu wana jf, nimeoa na nina miaka 4 ya ndoa yangu, kadri siku zinavyokwenda napunguziwa dozi ya mapenz, zilizopita ilikuwa 5 mpaka 6 per month sasa hivi ni 1per month na anakua mkali yaani mpaka nibembeleze kama naomba employment ukipewa unaambiwa utapata tarehe kama hi next month nampenda sitaki kumsaliti naheshim ndoa yangu. Naombeni ushauri nifanyaje walau niongeze doz.
hayaaaa kaaribu kabisaaaaaaaaaaaaaaAfya ya akili yako itaharibika punde.Fanya haraka ukae nae chini muone tatizo liko wapi.Akileta ubishi wewe mwanaume bwana hushikwi mkono kuvuka barabara.
kweli we bongolala username yako inafanana na mchango wakomkuu ndio maana mwanaume kuwa na mke mmoja ni ngumu,tafuta kidumu mkuu utakufa kwa presha bure!
nachukizwa sana na hali hii.....na ninalaani kitendo hiki....mimi kama mwanamke ninakemea ukiukwaji wa haki za binadamu.....