Kupeleka watoto wachanga chekechea imekuwa kama fasheni

"Waleeni watoto katika njia iwapasayo"
Wakati mwingine unaweza kuwa mtu mzima kabisa lakini usiwe mzazi bora!...
Mtoto mdogo mwenye umri Wa mwaka mmoja, au mmoja na nusu Leo hii imekuwa fasheni wazazi kumwandikisha kuanza chekechekea au babycare center!
Kiukweli kumwanzisha mtoto mdogo shule mapema kiasi hiki ni kumharibu mtoto pasipo kujua; anaichoka shule mapema na baadaye kuigharimu familia!
Wazazi badilikeni...
Tumeona hayo pia had Kwa wasanii .kina Aunt nani cjui na vichanga vyao chekechea cjui vinasoma nini.
***************
Kuna mdada mmoja nimemshuhudia kiila anaamka saa 11 na kukasumbua katoto kake alfajil kwenda shule huku kanasinzia"
Mwisho serikali itatoa tamko kisa wazazi kama hawa"
Ndio maana tunakuwa na kizazi cha ajabu sana siku hizi na vijitabia visivyo vya kawaida vinazidi kukita mizizi kwenye jamii. Wazazi hawalichukulii tena jukumu la malezi kama jukumu lao la msingi. Kitoto kinapelekwa boarding muda ambao inabidi kikae na wazazi kijifunze mambo ya msingi kabisa katika ukuaji wake. Hii ni aina ya ukatili, hakuna mwenye muda na rasilimali za kukulelea mwanao mdogo katika misingi inayotakiwa huko boarding as a result wanajilea wenyewe na kujiamulia ipi ni njia sahihi na anakua hivyo hivyo.
 
Kelele nyingiii tuacheni na watoto wetu jamani, Mimi mwanangu ana miaka mi 2 na Shule nimemuanzisha, majukumu yanatubana ndio, huyu wa miaka mi 2 ana mdogo wake wa miezi 7 na bado nina majukumu ya kikazi , sasa mnataka tuwaachie Dada wa nyumbani watoto wote hawa? Ataweza? Bora aende Shule tu
 
Najiuliza, huyu mtoto mzazi asipojishughulisha atakula nini?? Likizo inatambulika kuwa ni miezi 3 tu. Kazini, mama haruhusiwi kutoka toka tena mbaali. Kongowe na ofisi Posta Mpya. Kama mama ni golikipa, ni ushamba kumpeleka mtoto chekechea kabla ya 5yrs. Lakini kama ni mfanya kazi, apeleke huko day care.
 
kama wewe sio mwanamke, hujapata adha ya mabeki tatu, una mtoto mdogo na ni mfanyazi.....ruksa kuongea
Evy acha kabisaa asikwambie mtu yaani mabeki tatu sijui nani kawaloga maana tangu nimeanza kukaa nao naona ni kama vile akili zao zinafanana. aisee utaongea na kuelekeza jambo mpaka utahisi ya kwamba ww ndo tatizo. Mpaka kuna siku wife aliwahi kuniuliza labda sisi ndo tunatatizo maana kila beki 3 tunaempata ni majanga tuu. Tatizo ni kwamba watu wengi hupinga kitu ambacho hawakijui,ubishi ni asili kwa baadhi ya watu ila ukishapitia changamoto ndo utajua nini maana ya daycare,
Na kule sio kwamba watoto wanakwenda kusoma wengine ni kwenda kulelewa tuu kwa kuwa mzazi anakuwa bize na kukimbizana na pesa kulingana na kasi ya dunia ilivyo.
China hawakukosea kupunguza idadi ya watoto wa kuzaa
 
Kelele nyingiii tuacheni na watoto wetu jamani, Mimi mwanangu ana miaka mi 2 na Shule nimemuanzisha, majukumu yanatubana ndio, huyu wa miaka mi 2 ana mdogo wake wa miezi 7 na bado nina majukumu ya kikazi , sasa mnataka tuwaachie Dada wa nyumbani watoto wote hawa? Ataweza? Bora aende Shule tu
Ulizaa kwa bahati mbaya?hukujua kuna hayo majukumu kabla ya kuzaa?Jione mjanja ila gharama yake ni kubwa hapo baadae;kuna dogo mama yake alimuacha kwa bibi sababu ya kazi sasa hivi mama yake analalamika kwamba hamjali na hana mapenzi na mama yake kuliko mkewe na bibi
 
Kwenye ndoa hua hatuzai kwa bahati mbaya,futa kauli yako.
Alafu maisha hayafanani huyo Dogo unayemzungumzia hawezi kufanana na wanangu,usi force kufanaisha maisha
 
Kwanza day care sio shule ni Tanzania tu ndo tunajifanya shule ma watu wengi wamaanzishaga day care alafu zinakua shule wanakua wanakimbia gharama za kuanzisha shule na kwa vile day care ni bure bas unajikuta mwanao anaishia kwenda shule nchi za wenzetu day care ni sehemu ambayo mwanao anaenda kulelewa during the day unapotoka kazini unamptia..kama mama mwenye majukumu ni bora mwanangu akakae day care nyie mnashangaa mwaka wakati ata miezi 6 unampeleka mtoto day care akalelewe unasema mtu aache kazi alee mtoto uyo mtoto si atapata utapia mlo tutakula nini kwa maisha haya..hamjapata adha ya kukaa na wadada wa kazi nyie na kuwatafuta..kingine sasa watoto wa day care wana akili kama nini maana mtoto anaajamiana na wenzie basi wee maendeleo fasta fasta mtoto ata kusoma na kuongea anawahi mnoo na anakua anachangamka mkisema tabia mbaya ujue hata we mzazi tabia yako mbaya shirikiana na wafanyakazi wa kwenye kituo na unapomchukua mwanao mfunndishe tabia njema....au kama vipi serikali na sekta binafsi zitengeneze nursery kila ofisi unaenda na mwanao unamuacha apo unaendelea na kazi unakua unamchungulia chungulia tu basi.ila day care wala haina shida ninachokataaga kila siku ni kumpeleka mtoto boarding wakati bado mdogo
 
Evy acha kabisaa asikwambie mtu yaani mabeki tatu sijui nani kawaloga maana tangu nimeanza kukaa nao naona ni kama vile akili zao zinafanana. aisee utaongea na kuelekeza jambo mpaka utahisi ya kwamba ww ndo tatizo. Mpaka kuna siku wife aliwahi kuniuliza labda sisi ndo tunatatizo maana kila beki 3 tunaempata ni majanga tuu. Tatizo ni kwamba watu wengi hupinga kitu ambacho hawakijui,ubishi ni asili kwa baadhi ya watu ila ukishapitia changamoto ndo utajua nini maana ya daycare,
Na kule sio kwamba watoto wanakwenda kusoma wengine ni kwenda kulelewa tuu kwa **** mzazi anakuwa bize na kukimbizana na pesa kulingana na kasi ya dunia ilivyo.
China hawakukosea kupunguza idadi ya watoto wa kuzaa
Mm mtoto wa pili na watatu wamelelewa na madada hawapungui 25 mpaka nilipoamua kuchukuwa mtoto wa wifi kutoka kijijini na kuamia kumsomesha huku Dar ndio amekuwa msaada mkubwa kwangu mpaka sasa huyu watatu ametimiza miaka 4.
 
nawe pia mkuu .. nipo mkuu tunawaharibu watoto basi tu tuaniga vitu vya ajabu ajabu tu ila madhara yake ni makubwa badae.. wanabeba na matabia ya ajabu huko
asee nakuunga mkono kabisa dadaangu....
nlimtembelea rafkiangu ilkua mchana mda kidogo mtt anamiaka2 anatoka shule ana Bonge la nundu kichwani kuumuliza mtt anasema kupigwa na mwenzie ambaye ni mkubwa kupiga cm kwa Mwalimu wake anatwambia et mtt kaanguka
Wengine wanaongea matusi ad unajiuliza aka katt veepe

Skumwambia chochote mshkaj Ila lilkua somo kwangu

tena aspokua nunda mkorofi bas atapata kibiongo maana hayo mabegi wanayobeba Mhh!!!!!!!!
 
Mm mtoto wa pili na watatu wamelelewa na madada hawapungui 25 mpaka nilipoamua kuchukuwa mtoto wa wifi kutoka kijijini na kuamia kumsomesha huku Dar ndio amekuwa msaada mkubwa kwangu mpaka sasa huyu watatu ametimiza miaka 4.
Nakubaliana nawe mkuu kwa % zaidi ya 100. Me nishapoteza pesa za kuwasafirisha hawa wadada wa kazi toka huko kwao na kuwarudisha mpaka kichwa inachemka. Mwanzomwanzo atajifanya mtulivu ngoja amalize kama mwezi tuu utashuhudia chengachenga, Utashangaa na yeye atataka kufanana na mama mwenye nyumba.
Dah na me nitajaribui kufanya hivyo labda itasaidia jamani maana eeeehh
 
Huyo mtu mzima nae inawezekana akawa na watoto wake, kama wao ni bora sana kwann na yeye awaache na kuja kunilelea wa kwangu!
Tafuta mtu mzima ambaye hana majukumu kama hayo.
Ila ukiangalia kwa makini kila sehemu ina weakness zake,hizo daycare sometimes nazo zina mambo ya ajabu sana ambayo ni afadhali mtoto abaki nyumbani na beki 3,lakini pia mtoto akikaa nyumbani atajifunza bongo fleva mpaka basi....
Hakuna kizuri kisicho na faida.
 
Back
Top Bottom