Kupeleka watoto wachanga chekechea imekuwa kama fasheni

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,252
21,345
"Waleeni watoto katika njia iwapasayo".

Wakati mwingine unaweza kuwa mtu mzima kabisa lakini usiwe mzazi bora. Mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja, au mmoja na nusu leo hii imekuwa fasheni wazazi kumwandikisha kuanza chekechekea au babycare center.

Kiukweli kumwanzisha mtoto mdogo shule mapema kiasi hiki ni kumharibu mtoto pasipo kujua anaichoka shule mapema na baadaye kuigharimu familia. Wazazi badilikeni.

Tumeona hayo pia hadi kwa wasanii, akina Aunt nani sijui na vichanga vyao chekechea sijui vinasoma nini. Kuna mdada mmoja nimemshuhudia kiila siku anaamka saa 11 na kukasumbua katoto kake alfajiri kwenda shule huku kanasinzia.

Mwisho serikali itatoa tamko kisa wazazi kama hawa.
 
Upo!!heri ya mwaka mpya...tena unakuta kanachukuliwa na gari alfajiri eti kwenda shule...mtoto anaamshwa saa 11 au hata 10 alfajili ili asichelewe basi...halafu basi linafika shule saa 2!!
nawe pia mkuu .. nipo mkuu tunawaharibu watoto basi tu tuaniga vitu vya ajabu ajabu tu ila madhara yake ni makubwa badae.. wanabeba na matabia ya ajabu huko
 
Kuwapeleka watoto babycare center ni kukimbia majukumu ya kumlea hasa wakina mama. Huko kina mapungufu mengi Sana hawawalei watoto katika maadili. Mtoto anakosa haki ya msingi ya kulelewa na wazazi katika umri mdogo.Isitoshe anakosa mpenzi ya mama.
 
Chagua kuacha kazi za kuleta malezi mazuri kwa mtoto au baki naye akuimbie nyimbo zote zizizo za staa zinazosikilizwa hapo nyumbani wakati haupo. Hakuna kitu kuchoka shule mtoto ubongo unauwezo wa kujifunza kuanzia siku ya kwanza kwahiyo weka mbegu nzuri mapema anze kuandika unashangaa nchi za watu mtu 18 amemaliza chuo sasa wewe mpeleke mtoto shule na miaka mitano halafu chou miaka 26 uone huko baadaye inakuwaje. Mabadiliko ni lazima kizazi mpaka kizazi


hata Mimi wananichefua Sana.
vitoto vidogo miaka miwili wanavikomaza bure.
watoto wanaenda Shule hawajui shule ni nini, ndio maana wanafika miaka mi4 wanakataa shule.. maana wamechoka .
wangoje hata angalau miaka mi5 kidogo wanajitambua kwa mbaali.
 
"Waleeni watoto katika njia iwapasayo"
Wakati mwingine unaweza kuwa mtu mzima kabisa lakini usiwe mzazi bora!...
Mtoto mdogo mwenye umri Wa mwaka mmoja, au mmoja na nusu Leo hii imekuwa fasheni wazazi kumwandikisha kuanza chekechekea au babycare center!
Kiukweli kumwanzisha mtoto mdogo shule mapema kiasi hiki ni kumharibu mtoto pasipo kujua; anaichoka shule mapema na baadaye kuigharimu familia!
Wazazi badilikeni...
Tumeona hayo pia had Kwa wasanii .kina Aunt nani cjui na vichanga vyao chekechea cjui vinasoma nini.
Tena wanafanyiwa na interview kabisa kabla ya kuandikishwa hahahaha.
Wazazi wako busy kuyasaka maisha.
Nilimkuta binti mdogo tu amevaa T-shirt imeandikwa kifuani FACEBOOK IS MY MOTHER.
Huyu yawezekana amakosa mapenzi ya mama. Asiweza kuwa na t-shirt ya aina hiyo kama anampenda mama yake.
Halafu tunakaa tunalamika eti kizazi hiki hakina maadili mema.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom