Sidhani kama watuhumiwa wanaofanya vitendo vya ulawiti kwa watoto wanachukuliwa hatua stahiki

Mchaga Tajiri

Member
Mar 14, 2023
10
16
Vitendo vya ulawiti vimeendelea kujitokeza katika maeneo mengi hapa nchini Tanzania. Licha ya Serikali na wadau mbalimbali kupiga kelele kuhusu vitendo hivi bado vimeendelea kushamiri kwenye maeneo yetu.

Vitendo hivi vinapotokea wazazi/walezi wamekuwa na tabia ya kufumbia macho kwa kutokutoa taarifa kwenye mamlaka husika ili hatua zichukuliwe. Na hata taarifa zikitolewa na hatua kuchukuliwa watuhimiwa wa makosa haya baadhi yao huachiwa huru.

Mtoto mmoja wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 8 anayesoma katika moja ya shule ya msingi mkoani Morogoro wilayani Kilosa amekutana na kadhia hiyo akiwa na mdogo wake wa umri wa 6 anayesoma chekechea ambao walikuwa wakifanyiwa vitendo vya ulawiti na baba yao mdogo.

Anasema “Bamdogo George huwa anakuja usiku anazima taa anapanda kitandani anakuja kutubaka alianza siku nyingi alikuwa anasema tukisema tena anatufanya tena.’’

Mzazi wa watoto hawa alisema mwanzo hakuwa anafahamu kwamba watoto wake wanafanyiwa vitendo hivyo vya ulawiti alifahamu kupitia mgeni aliyekuja nyumbani kwake.

“Mimi kama mzazi wa hawa watoto wangu kuna shemeji yangu ndio aliwafanyia hilo tukio la kuwabaka. Nilikua sijagundua kwa haraka .Lakini kuna mtu alikuja kulala na hawa watoto shemeji yangu alichelewa kurudi nyumbani alivyoingia ndani kazima taa alivyozima kaingia kitandani alikuwa anapapasa wale watoto. Yule mgeni akashituka na yule shemeji yangu akakimbia chumba kingine.”

Mbali na mtuhumiwa kukamatwa na kufikishwa kwenye mamlaka husika lakini ameachiwa huru na yuko mtaani.
 
Back
Top Bottom