Kutengeneza Kipato Endelevu Kupitia Kukodisha Majengo Ya Kituo Cha Kutunzia Watoto (Daycare Center)

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Uzoefu wangu.

Kituo cha chekechea (daycare center) kipo chini ya ofisi ya wilaya (afisa maendeleo). Hivyo taratibu zote za kufungua zinaishia hapo. Wakati shule ya chekechea (nursery school) ipo chini ya wizara ya elimu. Hivyo taratibu za kufungua Nursery school zinatofautiana na zile za kufungua daycare.

Mimi nimefokasi na kufungua daycare kwa sababu zifuatazo:-

✓ Haina changamoto nyingi za utaratibu wa kufungua.

✓ Huhitaji kiasi kidogo cha mtaji fedha. Hivyo inaweza kuwa ni sehemu nzuri sana ya kuanzia.

✓ Jengo moja tu linaweza kutosha na utatengeneza fedha nzuri tu.

Vifaa Vinavyohitajika.

✓ Mipira.

✓ Midoro.

✓ Kufaa cha kusllide.

✓ Bembea za watoto.

✓ Madarasa matatu (sio lazima utakomaa na afisa maendeleo mpaka mfikie muafaka).

✓ Viti, ubao, vitabu na chaki.

✓ Televisheni ndogo kwa ajili ya kuangalia katuni muda wa mapumziko (hii nayo sio lazima kama mfukoni haupo vizuri). Mtakuwa mnaimba nyingi tu kama mpo ibada ya watoto. Hakikisha mwalimu ana nyimbo tamu kwa watoto na viwe nyimbo za maneno machache na ya kujirudia rudia.

Sababu Tatu (4) Za Uwepo Wa Fursa Hii.

Moja.

Changamoto ya wafanyakazi wa ndani.

Hii hupelekea wazazi kukosa sehemu salama ya kuwapeleka watoto wao wakiwa kazini au shughuli mbalimbali.

Mbili.

Ongezeko la hamasa ya kufahamu kiingereza.

Wazazi wengi wanaonekana kuvutiwa sana na watoto wanao ongea kiingereza. Hili hupelekea kupambana kwa hali yoyote ili mtoto aende shule za awali ili afahamu lugha ya kiingereza akiwa ni mdogo.

Tatu.

Wazazi kuwa na imani kubwa kwa watoto.

Watoto wadogo huaminiwa zaidi kuliko watoto ambao wanakaribia utu uzima. Hii ni kwa sababu watoto wakubwa wanakuwa wameonyesha udhaifu ambao hupelekea wazazi kuondoa imani ya kufanya makubwa kielemu.

Nne.

Ni sehemu ya maandalizi ya kujiandaa kwenda shule ya msingi.

Kwa sasa kuna msisitizo mkubwa kuwa mtoto ni lazima apitie chekechekea ndipo aweze kuingia darasa la kwanza. Kuna chekechea za shule za serikali na zile za kulipia. Hizi za kulipia zinaaminika zaidi kuliko zile za serikali ambazo huaminiwa kuwa mtoto anaenda kukua na sio kujifunza.

Mitaa/Kata Zenye Masoko Mazuri Ya Majengo Ya Chekechea.

Moja.

Kata zenye idadi kubwa ya wakazi kama Kihonda, Lukobe, Mkundi, Tungi na Mwembesongo.

Mbili.

Mitaa ya changanyikeni (Uswahilini).

Panafaa zaidi kwa kumiliki majengo ya chekechea (daycare center).

Gharama Zinahitajika.

✓ Kodi ya nyumba. Lazima uilipe hata kama umejipangishia.

✓ Bembea tofauti tofauti za watoto.

✓ Mwalimu mmoja (kwa kuwa unaanza). Mshahara utamlipa kati ya Tshs.150,000 hadi Tshs.250,000 kutegemea na makubaliano na idadi ya wanafunzi.

✓ Mdada wa kazi za usafi na upishi wa chakula cha watoto.

✓ Viti viwe vingi (unaweza kwenda kununua kwa bei ya jumla kwenye maduka makubwa au unaenda viwanda vya plastiki kama vipo karibu na wilayani kwako.

Jinsi Ya Kukusanya Malipo.

✓ Ada huwa inalipwa kwa mwezi. Lakini ninapendekeza mzazi awe analipa kila siku au kwa wiki. Wazazi wengine ni wasumbufu sana hapa mjini.

✓ Hela ya chakula iwe inalipwa kila siku mtoto anapohudhuria kituoni.

✓ Ada ya shule igawe katika makundi mawili; wanaowahi kuwachukua watoto wawe wanalipa kiasi kidogo cha ada kuliko wanaowachukua watoto muda wa jioni (kwa kawaida saa 12 kamili jioni).

Changamoto Za Kuendesha Kituo Chekechea.

✓ Baadhi ya watoto kulia muda mwingi.

✓ Baadhi ya wazazi/walezi kusumbua kulipa ada ya watoto wao.

✓ Watoto kutoroka kituoni.

✓ Watoto kupotea kituoni au muda wa kuwarudisha nyumbani kwao.

✓ Wazazi/walezi kuchelewa kuwachukua watoto wao.

✓ Kupungua kwa idadi ya watoto mara kwa mara.

Hivi ndivyo tumeweza kuifikia wilaya ya Morogoro mjini. Wiki ijayo tutakuwa mkoa gani rafiki?. Karibu utoe taarifa za wilaya yako tuweze kujifunza pamoja.

Muhimu; ninakaribisha maoni na mapendekezo kuhusu programu hizi zinazoendelea kwenye makundi yetu ya TZ REAL ESTATE TEAM ili tuweze kunufaika wote.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711

MUHIMU; Jiunge BURE na kundi la whatsapp liitwalo TZ REAL ESTATE TEAM. Ukiwa hapa utapata masomo na mijadala kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo (real estate investment).

Nitumie ujumbe usemao "WORKSHOP"...

Natumai wahusika wamepata muongozo
 
Back
Top Bottom