Kupatwa kwa Jua: Sayansi imethibitisha Mungu hayupo

Ngoja ukose uwezo wa kupumua ndiyo utamtafuta alipo Mwenyezi Mungu

Kukosa uwezo wa kupumua ni dalili ya kutokuwepo Mungu. Si dalili ya kuwepo Mungu.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote angekuwepo, kungekuwa hamna kifo.

Kwa nini Mungu mwenyewe uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao kifo kinawezekana?
 
Ngoja likufike la kufika ndiyo utaimba Mungu wangu wee
1473293933778.jpg
 
Wanabodi
Salaam;

Kwa muda hapa watu wamekuwa wakibishana juu ya uwepo wa Mungu. Wengine wakisema Mungu hayupo na wale wanaoamini uwepo wa Mungu.

Binafsi nikiunganisha hoja za wale wanaosema hakuna Mungu na tukio la leo sept.mosi la kisayansi la kupatwa kwa jua,kwa kiwango kikubwa wamethibitisha Mungu hayupo!

Tukio la kupatwa jua,limetangazwa muda mrefu na wanasayansi wakieleza itakavyokuwa,sehemu,muda na hata siku itakapotokea tena hapa Tanzania na sehemu zingine.

Sayansi haiwajawahi kudanganya,lkn viongozi wengi wa Dini hakuna jambo hata moja ambalo wanaweza kueleza kwa wafuasi wao kwa uhakika km litatokea. Viongozi wa dini kazi yao ni kujaza watu uoga na hilo wamefanikiwa sana.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu tukio la kupatwa kwa jua,shekhe wa mkoa wa Dar. Alisema tukio hilo ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu na kwamba waislamu ktk tukio km hilo,wanapaswa kusali sana!

Alipoulizwa askofu mkuu msaidizi wa jimbo la Bukoba alisema kanisa halina kanuni yoyote inayoelezea tukio hilo nae akasisitiza watu kusali.

Kuna umuhimu wa kufundisha zaidi watoto wetu sayansi kuliko dhana isiyoaminika ya maandiko matakatifu.

Siku ambayo wanasayansi watatangaza kuwa kuna kimondo kitaipiga Dunia na kwamba itakuwa ndo mwisho wa Dunia,hakuna ubishi huo ndo utakuwa mwisho. Na wale wanaosubiri kurudi kwa Yesu kristu watabaki na hiyo hadithi isiyo na kikomo.

Nawasilisha...!

Umeshawahi kusikia tabiri ngapi zilizofeli za sayansi?...mtengeneza taa tu alifeli mara 999...Sayansi hata Ya sasa inatabiri vitu vingi sana ambavyo sio kweli.
Mfano ni ule utabiri wa kupotea kwa barafu kabisa antatika na aktiki na kuongezeka kwa joto zaidi duniani kote ifikapo miaka Ya 2000.Mpaka sasa kuna sehemu barafu imeongezeka.

Lakini labda suala la msingi zaidi ni kwamba, dini Ya vitabu vitakatifu inafuata Imani, kitu ambacho hakiitaji kuona ili kuthibitisha. Sayansi, inafuata majibu Ya majaribio yanayofanyika katika vitu vinavyoonekana (physical environment). Dini haiwezi kuielezea sayansi wala sayansi kuielezea Dini.Waongo ni wale wanajaribu kufanya hivyo.Na kwa bahati mbaya watu wa Dini ni wengi hapo.
 
Acheni kudanganya watu eti kwa ajili ya hiyo sayansi pasipo mungu kusingetokea hill tukio mungu yupo na mda ukifika atarudi kuwachukua wateule wake.
 
Nikiuliza "pembetatu duara ipo" ina maana pembetatu duara hiyo ipo?

Nikuliza "Papa wa Wakatoliki John Pombe Magufuli yupo" hilo lina maana kuna Papa wa Wakatoliki John Pombe Magufuli?

Nikiuliza "Mji Mkuu wa Marekani uko kwa Wagagagigikoko?" hilo lina maana mji mkuu wa Wamarekani uko kwa Wagagagigikoko?

Nikiuliza "Rais wa Tanzania ni Bulicheka" hilo lina maana rais wa Tanzania anakuwa Bulicheka?
Nimekuambia ukiona anauliyeulizwa(kwa maana waulizaji ni wengi)ujuwe aulizwaye yupo.
Hayo Maswali ya Pembetatu duara,nk,unauliza wewe peke yake yako.Hakuna mwenye akili timamu akauliza kitu peke yake,ila atakuwa ana kasoro fulani.
 
Me nafurahi sababu atheists wanamtangaza Mungu kuliko hata waamini uchunguzi umefanyika imedhibitika majority wasioamini Mungu wanamtaja Mungu kwa 94% na wanaoamini Mungu wanamtaja Mungu kwa 6% katika mazungumzo yao ya kila siku.

Hivyo congrats atheists keep saying God all the way till He come/ you die.
 
Wanabodi
Salaam;

Kwa muda hapa watu wamekuwa wakibishana juu ya uwepo wa Mungu. Wengine wakisema Mungu hayupo na wale wanaoamini uwepo wa Mungu.

Binafsi nikiunganisha hoja za wale wanaosema hakuna Mungu na tukio la leo sept.mosi la kisayansi la kupatwa kwa jua,kwa kiwango kikubwa wamethibitisha Mungu hayupo!

Tukio la kupatwa jua,limetangazwa muda mrefu na wanasayansi wakieleza itakavyokuwa,sehemu,muda na hata siku itakapotokea tena hapa Tanzania na sehemu zingine.

Sayansi haiwajawahi kudanganya,lkn viongozi wengi wa Dini hakuna jambo hata moja ambalo wanaweza kueleza kwa wafuasi wao kwa uhakika km litatokea. Viongozi wa dini kazi yao ni kujaza watu uoga na hilo wamefanikiwa sana.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu tukio la kupatwa kwa jua,shekhe wa mkoa wa Dar. Alisema tukio hilo ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu na kwamba waislamu ktk tukio km hilo,wanapaswa kusali sana!

Alipoulizwa askofu mkuu msaidizi wa jimbo la Bukoba alisema kanisa halina kanuni yoyote inayoelezea tukio hilo nae akasisitiza watu kusali.

Kuna umuhimu wa kufundisha zaidi watoto wetu sayansi kuliko dhana isiyoaminika ya maandiko matakatifu.

Siku ambayo wanasayansi watatangaza kuwa kuna kimondo kitaipiga Dunia na kwamba itakuwa ndo mwisho wa Dunia,hakuna ubishi huo ndo utakuwa mwisho. Na wale wanaosubiri kurudi kwa Yesu kristu watabaki na hiyo hadithi isiyo na kikomo.

Nawasilisha...!

Jinsi gani mwezi umefanyika?
 
Kwa nini wewe ndiye uwe na uamuzi wa kusema hiyo meli ni nini?

Hoja yako ni batili.

Unataka kuonesha kwamba Mungu yupo kwa sababu kitu chochote complex hakiwezi kujiendesha chenyewe, ni lazima kiwe na wa kukiendesha.

Mimi nakuambia Mungu ana complexity kuliko meli. Na yeye kuna anayemuendesha?

Utaona kwamba, ukikubali kwamba kitu chochote kilicho complex ni lazima kiwe na anayekiendesha, basi Mungu atahitaji wa kumuendesha, na huyo anayemuendesha atahitaji wa kumendesha, hivyo hivyo, ad infinitum, ad absurdia.

Katika ulimwengu huo, hakuna haja ya Mungu.

Ukisema kwamba Mungu hahitaji wa kumuendesha umeshafungua mlango wa kingine chochote kutohitaji wa cha kukiendesha, na hivyo Mungu kutohitajika.

Katika ulimwengu huo, hakuna haja ya Mungu.

Chochote utakachosema kinaonesha Mungu hayupo.

Hapo ndipo mlinzi wa Kimakonde aliposema "Ukikimbia nchale, ukichimama nchale".

Mungu hayupo, jinsi unavyotaka kuonesha yupo ndivyo unavyozidi kuonesha hayupo.
na hapa duniani tumekuja kufanya ni ni?? na nani alietuleta??
 
Me nafurahi sababu atheists wanamtangaza Mungu kuliko hata waamini uchunguzi umefanyika imedhibitika majority wasioamini Mungu wanamtaja Mungu kwa 94% na wanaoamini Mungu wanamtaja Mungu kwa 6% katika mazungumzo yao ya kila siku.

Hivyo congrats atheists keep saying God all the way till He come/ you die.
Atheists wanatangaza Mungu hayupo kama Mathematicians wanavyotangaza pembetatu duara haipo.

Hamjathibitisha kwamba Mungu yupo.

Mpaka hapo mtakapothibitisha, Mungu wenu amekuwa exposed.
 
Waislamu na wakristo kuamiani hizo sifa tatu za mungu sina tatizo ila hizo ni sifa tatu tu,kuna sifa zengine za mungu zaidi ya hizo tatu. Na wewe umejikita kwenye agano jipya je,unafikiri utakuwa hoja zako zitaenda sawa kwa uislamu na ukristo?
Hata kama sifa ingekuwa moja tu, Mungu hatakiwi kuwa na contradiction yoyote ile.

Kwa nini unasema nimejikita katika Agano Jipya?

Hizi sifa hazipatikani kwenye Agano la Kale na Quran?
 
Ulishauona umeme?
Ulishaona huzuni?
Ulishaona furaha?
Ulishaona kifo?
Mimi sijapinga kuwepo kwa Mungu kwa sababu sinamuona.

Sinaiona kesho lakinibnaamini inakuja.

Sijaiona Mbale lakini naamini ipo.

Napinga kuwepo Mungu wenu huyo kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe katika namna ambayo haileti mantiki.

Dhana ya kuwepo Mungu ina contradiction.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hakutakiwa kuumba ulimwengu ambao unaruhusu maovu kama huu. Ulimwengu huu unaoruhusu maovu unaonesha kwamba Mungu huyo hayupo.
 
Kuna mantiki kwenye andiko lako...lakini umetumia hoja nyepesi sana.....

Hebu fikiria umbo tata la mwili wa mwanadamu na uwiano wa utendaji kazi ww viungo hivyo je ni vitu vilivyojitokeza tu vyenyewe....!!!??
 
Unaweza kuthibitisha vimeumbwa na Mungu?

Unafahamu kwamba mfumo wowote unaotoa waste product ni inefficient?

Unafahamu kwamba mwili wa binadamu unatoa waste product?

Unataka kusema Mungu kaumba an inefficient system?
 
KAMA KUPATWA KWAJUA KUNAWEZA KUONGEZA KIPATO NAKUWAVUTIA WATALII KWA NAMNA ILE,TUWAOMBENI WANASAYANSI WALIFANYE JUA LIPATWE TENA KAMA MUNGU ALIVYOFANYA LIKAPATWA NA AKALIACHANISHA!!!!

"wanasayansi acheni kufanya watu matahila

Na nyie wanademocrassia mnao mkana mungu muumba
na kuwatukuza waungu bandia wana sayansi..!!!

Tukio la kupatwa kwa jua kutangazwa na
wanasayansi masiku kadhaa kabla kutokea sio
ajabu walaujuzi wa kustaajabishaa kwani ni sawa
na:-
-mvuvi anaye kwambia kuanzia kesho dagaa
watakufa kwa wingi,
-Na nahodha anaye sema tusisafiri muda huu kwani saa tisa usiku tutakuwa
sehemu fulani na eneo lile mida hiyo litakuwa na
upepo mkali,
-Na mkulima anaye kwambia mvua hizi za mwaka
huu mahindi yatakuwa machache lakini mtama
na viazi zitakuwa vingi sana na kweli ikawa hivo.
kwanini hawa hamuwatukuzi?

huwa kuna viashiria maalumu ambavyo vinavyo
ashiria hayo kama walivyo ona wanasayansi kwa
kupatwa na jua
kwahiyo mwanadamu atabakia kuwa mwanadamu
tu na hajui ghaibu (yaliyo fichika)
maswali ya kujiulizani kwa nyie mnao shereheka
na kuwasifia wana sayansi tu bila mungu kuhusika,
1-je wana sayansi wanaweza kulifanya jua
lipatwe tena ?
2-baada ya kupatwa wana weza kulitenganisha?
3-je wangeweza kuzuia lisipatwe?
4- wao waliona ishara je nani aliye zileta hizo
ishara za kupatwa ?

Hivi watu wamekuwa wajinga kiasi gani na
kuanza kuwasifia wanaasayansi tu bila mungu
kuhusika hata kidogo kusifiwa nakuogopewa?

HAKIKA DEMOCRASSIA NI USHETANI AMBAO
HATA IBILISI MWENYEWE ANASHANGAA,
Media zote za mapagani wakidemocrassia
ilikuwa wajibu wao wawarejeshe watu kwa
mungu ukubwa wake, uwezo wake, maamuzi
yake, miapango yake, nakuwa hii ni dalili watu
waache maovu na kumrejea mungu
badala ya hivyo ndio ushirikina na upagani unapewa
nguvu sana na kuwatukuza walio ona ishara za
kupatwa kwa jua kwa kutumia vyombo ila
wanashindwa kumtukuza aliye leta hizo ishara na
kukamilisha jua kupatwa kabisa bila vyombo.

##TANZANIA inashereheka kwa kugawana kondomo
milioni 2, huu ni zaidi ya upumbavu!!##
Ubarikiwe mno kwa mchango wako, mwenye kuelewa atakuwa kaelewa.
 
Pembetatu ipo na duara ipo,nivitu viwili vilivyotajwa pamoja,nisawa na kusema hakuna mkichaa mwenye akili.Akili zipo,na mkichaa yupo.
View attachment 395344

kwenye ulimwengu wa vipimo kuna ujazo mbalimbali kama robo nusu na kitu kamili nk.. nusu mbili hutengeneza kitu kamili robo mbili hutengeneza nusu.

Kuna kamchezo ukimtuma mtu asiye mwaminifu akuletee kitu kinachohusika na vipimo kupiga bao! Ukimtuma kilo moja yeye ataleta nusu na robo.

Duniani tuna imani mbalimbali kuanzia zinazoabudu Mungu mmoja,miungu vitu vinavyoonekana hata masanamu kwenye hizi imani kuna mitifuano na mikanganyiko mingi tuu..lakini kiboko ya imani zote ni hii isiyomwamini Mungu mmoja

Jaribu kumuuliza atheist yeyote kwanini huamini katika Mungu atakwambia kwakuwa hajawahi kumuona! Ila muulize kama alishawahi kuiona akili yake au roho yake...hatakupa jibu moja na la moja kwa moja

Hii ni imani isiyotimia isiyojua dhima yake mwanzo wake wala muktadha wa nini inasimamia

Ni imani chongo yenye kengeza barobaro...ikiamini isichokiamini..ikifuata isichokijua

Je atheism ni;
Kuabudu miungu?
Kuabudu shetani?
Kuabudu masanamu?
Kuabudu vitu ?
Ama kutoabudu chochote?

Kila imani ina maelezo fulani kwenye chochote na kila swali lina jibu lake tusiiweke sayansi kwenye kundi la imani..hili ni Somo kama masomo mengine

Kutoamini chochote ni mkanganyiko tu wa akili kwakuwa mwisho wa siku utajikuta unaangukia kwenye imani yoyote japo kwa kificho na imani ya kutoamini chochote ni imani isiyotimia

Atheists wanatangaza Mungu hayupo kama Mathematicians wanavyotangaza pembetatu duara haipo.

Hamjathibitisha kwamba Mungu yupo.

Mpaka hapo mtakapothibitisha, Mungu wenu amekuwa exposed.
 
Pembetatu ipo na duara ipo,nivitu viwili vilivyotajwa pamoja,nisawa na kusema hakuna mkichaa mwenye akili.Akili zipo,na mkichaa yupo.
Hoja ni kuwepo au kutokuwepo kwa kwa pembetatu duara, si kuwepo kwa pembetatu wala duara.

Umeelewa hilo?

Nikisema mji mkuu wa Tanzania si Washington DC hilo halina maana hakuna Tanzania wala hakuna Washington DC.

Hilo lina maana hakuna Washington DC iliyo mji mkuu wa Tanzania.

Umeelewa hilo?
 
Hakuna uongo wa kijinga kama kuamini Dini.
Hakuna kupatwa kwa jua wala mwezi ni uongo uliokithiri, mbona waliokuwa wanaagalia kupitia vile vifaa kulikuwa na vivuli? kama jua lingepatwa mwanga ungetoka wapi porini kama pale maana hakukuoneshwa hata genereta!!!
 
Back
Top Bottom