Kupatwa kwa Jua

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Kupatwa kwa jua hutokea mara baada ya Jua mwezi na dunia kukaa katika mstari mmoja ulionyooka na kupelekea kutokea kwa kivuli katika eneo moja wapo la duniani.

Mwezi huziba eneo fulani la mwangaza wa Jua unaofika huku duniani na kupelekea kutokea kwa giza katika wakati wa mchana na hali hiyo huwa ni tofauti kabisa kwa vile tulivyozoea wanadamu.

Kupatwa kwa Jua huwa ni nadra sana kutokea tofauti na lile tukio la kupatwa kwa mwezi ambalo hutokea zaidi ya mara 5 au zaidi kwa mwaka.

Mwezi huzunguka dunia yetu hivyo si kila mzunguko wake huweza kusababisha mwezi kukaa katika mstari ulionyooka na dunia na jua ili kusababisha tukio hili kuweza kutokea.

Pichani ni muonekano wa kupatwa kwa Jua unavyokuwa kama utakuwa huko anga za mbali.

Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili
FB_IMG_1674845397686.jpg
 
Back
Top Bottom