Kupata mtoto

Nakesha kumsaidia kumuogesha mtoto na kumbembeleza usiku maana najua mchana ni zahama la kunyonyesha hivyo mama anachoka sana.

Itakuwa vyema nikiongeza darasa kwako

Haya sasa kwenye menejimenti miting mzungumzie jukwaa la watoto na malezi kama ilivyotanabaishwa na Karucee
 
Last edited by a moderator:
Heading hapo juu inasomeka kama haijakamilika vile.

Inawezekana kila mwanaJF akawa amejenga picha yake na uelewa kuhusu hili neno Kupata Mtoto

Mtoto ni tunu na furaha ya wazazi, ingawa inawezekana wazazi hao wakawa wapo
ktk mahusiano rasmi ya ndoa, mchepuko na kadhalika. Lakini si mara zote mtoto anafurahisha wazazi. Pata picha ya wazazi ambao kwanza ni wanafunzi kisha tegemezi kwa wazazi/ walezi wao ambapo inawezekana walitamani kuuchoropoa ujauzito bila mafanikio lakini hatimaye wamepata mtoto ambaye labda mzazi mmoja kamkana tangu alipotaarifiwa ama wote hawana amani na ujio huo.

Hakika pia ninashangazwa na wingi wa watoto kwa wazazi ambao uchumi wao ni tia-maji tia-maji na cha kushangaza ni kuwa hawakosi chakula cha kuwalisha watoto wao na kadhalika. Hivyo naamini sasa kwamba mtoto huja na baraka maalum. Sishawishi uzazi usio na mpango.

Pamoja na hayo mtoto anabaki kuwa na haki zote za msingi yaani ulinzi na malezi kutoka kwa wazazi/ walezi wake.

Ninafuraha kuwatabainisha kwamba nimekuwa miongoni mwa wazazi rasmi wenye furaha iliyotajwa hapo juu.


Mkuu ungefunguka we uko kwenye kundi gani hapo baada ya kuzunguka sana, bythe way, hongera.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Kumbe na wewe ulikuwa unafanya ngono zembe!!! Atii!? Hongereni na muandalieni mazingira mazuri asijejutia kuletwa ulimwenguni na nyie wazazi wake
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Paw hongera kwa majaaliwa hayo, pia jitahidi baada ya mwaka unaongeza mwingine...! weka malengo endelevu...nami nilifanya hivyo!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Paw
Hongera Paw
Watoto ndio furaha ya nyumba hasa wachezapo na kumita baba (Hii ni heshima kubwa sana kwako kwani wawapo na wenzao hutamba Baba yangu mmi .......................................)
Ndio Urithi wako hata kwa Jina kwani umeongeza uzao na familia nyingine ambalo ni tawi toka kwako
Watoto watakupatia Wajukuu utakaocheza nao na watakushikia mkongojo (fimbo)
Hongera
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Paw
ningekuwa na bunduki ningekupiga ujue?!

Unadhani kuwa na mimba raha? Unakuwa kama juisi za yeboyebo.

Paw hongera kwa majaaliwa hayo, pia jitahidi baada ya mwaka unaongeza mwingine...! weka malengo endelevu...nami nilifanya hivyo!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom