Nimekuwa kwenye harakati za kutaka kuoa ila kila nikiangalia wanawake ninaodate nao wengi wamezidi umri kuanzia 2 yrs; hili suala linanichanganya sana inakuaje naoa mwanamke aliyenizidi umri?? Je ni gape gani ni sahii? Mimi ni under 25; wadada wengi under 24 wanakuwa hawapo tayari kwa kuolewa na wengi bado wanaona wanapenda kuendelea kukaa kwa wazazi; ila 27+ wengi wanakuwa wanajielewa sana yaani natokea kuwakubali ile mbaya sema ndo hivyo wamenizidi umri. Tupeane uzoefu mlioingia tayari kwenye hii taasisi ya ndo uzoefu wenu ni muhimu wakuu.