Natafuta mke wa kumuoa ili tusaidiane maisha maana ni magumu peke yangu

waterproof

JF-Expert Member
Aug 14, 2020
387
348
Katika vitabu vya dini mbali mbali na misemo ya mababu zetu inasema ya kwamba

1. Mwanaume bila mke hajakamilika
2. Wenye akili wote wameoa
3. Ndoa ni kipimo cha akili n.k

Yapo mengi mno ambayo hata Mimi siyafahamu na wewe waweza kuwa unafahamu mengine.

Niingie moja kwa moja kwenye pointi ya Uzi huu, kiukweli umri wang naona unazidi kwenda na sijabahatika kuwa na mke/msaidizi katika maisha. Mungu aliumba kila kitu kwa kufanana(pair) hivyo natafuta pair(mke) wa kuishi nae akubaliane na tabia zangu nami nizikubali zake.

VIGEZO VYANGU VYA KUZINGATIA

1. Anipende kwa dhati hata kwa asilimia 45 tu kwangu zinatosha

2. Awapende ndugu zangu bila kujali wao watampenda au laa. Nikisema ndugu namaanisha kuanzia kwa wazazi

3. Awe na kiu ya maendeleo. Katika vitu ambavyo humsukuma mwanamume kupigana kwa hali na mali ni msukumo wa mwanamke/mke kumhimiza na kumpa support na kumtia moyo ikibidi kumsaidia katika shughuli za kuleta maendeleo katika familia na wanawake wengi wa karne ya 21 hawana hilo wao huwaza starehe.

4. Awe na umri usiopungua miaka 28 na usiozidi 30. Katika kuoa au kuchagua MTU sahihi wa kuwa mshauri wako, mlezi wa familia yako inatakiwa uzingatie umri pia. Kwangu mimi naamini katika umri huo mwanamke huwa ameona au kupitia mambo kadha wa kadha hivyo kumfanya ajitambue kuwa yeye sio mtoto tena na kufanya awe na molari ya kutafuta maisha yaliyo bora ingawa kina wanawake wana umri mkubwa lakini ubongo wao ni under 18.

5. Awe tayari kuishi mahali popote duniani. Hii ni kama ziada tu maana kuna wanawake wengine huchangua mahali pa kuishi na kusahau kuwa maisha ni popote. Hivyo basi kama uko tayari huu ya hilo usisite kunitafuta.

NB:
Nimeandika Uzi huu nikiwa namaanisha nia ya dhati ya kutaka mwanamke wa kuoa, atakae ona sifa hizo anazo basi asisite kunitafuta maana ya Mungu mengi.

Asante
 
HONGERA sana kwa uwazi huo, nikushauri kwenye sifa tajwa jitahidi nawewe uwe nazo, hii utakujengea kujiamini, wengi tunatabia ya kuweka vigezo ambavyo binafsi huwezi kuziishi, jambo la MUHIMU kuliko yote ni kumtegemea muumba kwani bila Mungu utabaki kutafuta kila siku mwenye vigezo na kamwe hutompata, jiamini, jisahihishe wewe kwanza, kuwa mpya, penda ndugu na jamaa wa mwanamke utakayekuja kuishi naye, kuwa na hofu ya Mungu .

Na imani utafanikiwa!!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hongera kwa kujitambua na kuona umefikia mahali pa kuhitaji mwenza.

Mungu akuongoze upate unayemtaka.
Tahadhari; Mke hatafutwi kwa mtindo ulioweka hapo, huo ni utaratibu wa kutafuta mfanyakazi ambapo unaweza kumfukuza wakati wowote atakaposhindwa kutimiza hayo masharti.

Kwa upande wa kutafuta mke unaanza kwa kumwona akakuvutia, ukampenda.
Mkiafikiana mnaanza kila mmoja kujifunza tabia za mwingine na kurekebisha mapungufu (uchumba). Mkiona mmekaa sawa mnaoana.
Huu mtindo mpya wa mitandaoni ni nadra sana kupata atakayeujaza moyo wako..Mungu tu aingilie kati.
 
Unatafuta mke wa kusaidiana maisha? Mimba pia utasaidia kubeba?

Wake ni wa kuwaoa na kuwahudumia tu. Kama maisha ni magumu ukiwa peke yako jua yatakua magunu zaidi ukioa na kuongeza watoto.

Katafakari tena dhumuni lako la kutafuta mke.
 
Kila mtu hupata wa kufanana naye
 
Katika vitabu vya dini mbali mbali na misemo ya mababu zetu inasema ya kwamba

1. Mwanaume bila mke hajakamilika
2. Wenye akili wote wameoa
3. Ndoa ni kipimo cha akili n.k

Yapo mengi mno ambayo hata Mimi siyafahamu na wewe waweza kuwa unafahamu mengine.

Niingie moja kwa moja kwenye pointi ya Uzi huu, kiukweli umri wang naona unazidi kwenda na sijabahatika kuwa na mke/msaidizi katika maisha. Mungu aliumba kila kitu kwa kufanana(pair) hivyo natafuta pair(mke) wa kuishi nae akubaliane na tabia zangu nami nizikubali zake.

VIGEZO VYANGU VYA KUZINGATIA

1. Anipende kwa dhati hata kwa asilimia 45 tu kwangu zinatosha

2. Awapende ndugu zangu bila kujali wao watampenda au laa. Nikisema ndugu namaanisha kuanzia kwa wazazi

3. Awe na kiu ya maendeleo. Katika vitu ambavyo humsukuma mwanamume kupigana kwa hali na mali ni msukumo wa mwanamke/mke kumhimiza na kumpa support na kumtia moyo ikibidi kumsaidia katika shughuli za kuleta maendeleo katika familia na wanawake wengi wa karne ya 21 hawana hilo wao huwaza starehe.

4. Awe na umri usiopungua miaka 28 na usiozidi 30. Katika kuoa au kuchagua MTU sahihi wa kuwa mshauri wako, mlezi wa familia yako inatakiwa uzingatie umri pia. Kwangu mimi naamini katika umri huo mwanamke huwa ameona au kupitia mambo kadha wa kadha hivyo kumfanya ajitambue kuwa yeye sio mtoto tena na kufanya awe na molari ya kutafuta maisha yaliyo bora ingawa kina wanawake wana umri mkubwa lakini ubongo wao ni under 18.

5. Awe tayari kuishi mahali popote duniani. Hii ni kama ziada tu maana kuna wanawake wengine huchangua mahali pa kuishi na kusahau kuwa maisha ni popote. Hivyo basi kama uko tayari huu ya hilo usisite kunitafuta.

NB:
Nimeandika Uzi huu nikiwa namaanisha nia ya dhati ya kutaka mwanamke wa kuoa, atakae ona sifa hizo anazo basi asisite kunitafuta maana ya Mungu mengi.

Asante

Pambana kwanza kutafuta pesa ili kipato chako kiongezeke zaidi ya hapo ulipo. Hakika baada ya hapo, utajichagulia mwanamke mzuri na mwenye sifa uzipendazo.

Wanawake walio wengi sidhani kama wanavutiwa na hayo maisha yako unayoishi sasa ya kutaka eti aje msaidiane ugumu wa maisha!! Huwa wanavutiwa na wanaume ambao tayari wana maisha mazuri au wale wenye muelekeo wa hayo maisha mazuri, na siyo maisha magumu.

Ukweli unauma. Ila na mimi kama Mjumbe, nimeona nitie neno.
 
Ni kweli maisha mazuri wanayapenda Ila so wrote wanaopenda kukuta mwanaume ameanza kwa kila kitu hvyo WAP kufka na kukaa tu

But kuna wengine wanapenda kwanza chini kwa ushirikiano then maisha yakaendelea me nataka kama hao
 
Unatafuta mke wa kusaidiana maisha? Mimba pia utasaidia kubeba?

Wake ni wa kuwaoa na kuwahudumia tu. Kama maisha ni magumu ukiwa peke yako jua yatakua magunu zaidi ukioa na kuongeza watoto.

Katafakari tena dhumuni lako la kutafuta mke.
Kila MTU huja na bahat yake maana kuna mengine walikua na maisha magumu kabla ya kuoa then baada ya kuoa maisha yaka change na kua mazuri
Labda niseme hyo dhana ya kwamba ukioa ukiwaasikini me naikataa na ndio maana nkaandika sifa ambazo mwanamke akiwa nazo kutoboa ni asbh tu
 
Ni kweli maisha mazuri wanayapenda Ila so wrote wanaopenda kukuta mwanaume ameanza kwa kila kitu hvyo WAP kufka na kukaa tu

But kuna wengine wanapenda kwanza chini kwa ushirikiano then maisha yakaendelea me nataka kama hao

Kwenye kigezo hicho nimekielezea pia. Unatakiwa uoneshe muelekeo wako/mipango yako ya baadae, kwa sasa unafanya kazi/shughuli gani, nk.

Lakini ukiegemea tu kwenye kigezo cha kutaka aje msaidiane kupambana na ugumu wa maisha, aisee watakukimbia. Hayupo mwanamke anayependa kuishi maisha ya shida! Huo ndiyo ukweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom