Kupata maendeleo katika MAISHA yako hakutegemei aina ya kazi pekee bali Malengo, hivyo ualimu pia ni kazi inayoweza kukuvusha

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
18,014
45,536
Katika MAISHA Kazi pekee haitoshi kukufanya kufika hatua kubwa ya MAISHA pasipo wewe mwenyewe kuwa na Malengo .

Hivyo linapokuja swala la kuijenga kesho yako iliyo bora kinachotangulia ni malengo na sio Aina ya Kazi unayofanya.

Kazi yoyote iwe decent Job (Kazi ya heshima ) au Kazi isiyo ya heshima bado inaweza isikupe MAFANIKIO Makubwa ikiwa wewe haujaweka maelengo kuwa wapi unahitaji kufika.

Ndiyo maana wapo Wanasheria Masikini Sana pia wapo wanasheria wanapesa Sana as the same wapo wafanyabiashara Masikini na wapo wafanyabiashara matajiri same apply kwa kada ya ualimu wapo walimu ambao wapo well financial stable as the same wapo walimu ambao wapo broke.

Ushuhuda , Mimi mjomba wangu ni Mwalimu wa sekondari anafundisha Bukoba , kapata Ajira mwaka 2015 kasoma BAED History na Kiswahili.

Hivyo uncle wangu kupitia hii kazi yeye aliitumia kama stepping stone yaani hakuiona hii kazi Kama MAFANIKIO bali aliichukulia kama kianzio Cha MAFANIKIO hivyo kitu alichoanza nacho ni kuwa na money literacy (Financial Education) kwa kuweza kutofautisha Kati ya Asset na liabilities . So baada ya kukopa mkopo wake wa kwanza aliwekeza ziwani huko majini kwa Kununua vifaa vya kuvulia samaki na dagaa na kuanza kuwakodisha wavuvi

Then hela nyingine alikodi nyumba na kuigeuza hosteli maana anapofundisha wanafunzi wanatembea umbali mrefu hivyo yeye wale wanafunzi wanotoka mbali wanakaa katika hostel yake na Chakula anapika yeye .

Hivyo wazazi wanalipia hosteli. Kiufupi uncle wangu kupitia hostel yake hakosi 1M kwa mwezi na ziwani hakosi 1Million pia yupo na Biashara ya mbalimbali nyingi .

Hivyo huyu Uncle wangu ndoto za yeye kuwa well Financial stable alikuwa nazo muda tu ila alitumia Kazi ya ualimu kutimiza ndoto zake.

Mpaka sasa Uncle wangu yupo hatua za mwisho kununua Costa na yupo hatua za mwisho kwenda kufundisha Kiswahili marekani Kama Lectururer.

Kila njia inaweza kukufikisha popote ikiwa utafata mwelekeo sahihi
 
Kina Joel Nanauka, Mwamposa, Mwakasege wanavyofundisha watu kuhusu mafanikio, na kuwala vichwa, si ualimu huo?

Ualimu ni fani pana na ina hela.
 
Kiswahili ambacho watu wanadharau ndo kinaenda kumfanya uncle kukunja zaidi ya mil 20 kila mwezi Pamoja na benefits kibao nyumba na Gari.
 
Hivi kwa uzoefu, kwenda kufanya kazi nje ya nchi mfano USA huwa ni umri gani mwisho ambapo mamlaka za huko hupendelea?
 
Hivi kwa uzoefu, kwenda kufanya kazi nje ya nchi mfano USA huwa ni umri gani mwisho ambapo mamlaka za huko hupendelea?
Sina ABC kwa sasa ila kufundisha Kama Lectururer unahitaji uwe na Kuanzia masters hadi PhD ila ila Kupata ile udhamini unabidi uwe below 30 hiyo program huitwa Full bright ambayo ukifika uko unaweza kusoma na Kupata fursa za Kiswahili

Mmimi nafatilia za kwenda Japan kwanza Maana nasikia huko Japan pia PESA ipo
 
Back
Top Bottom